Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wengi watakumbuka katika vita vya uvamizi vinavyoendelea huko Ukraine wakati vinaanza ilikuwa Ukraine akijibu mashambulizi kwa kushambulia eneo lolote ndani ya Russia au maeneo ya Ukraine yaliyotekwa na Urusi kama vile Crimea basi jeshi Urusi litajibu maradufu kwa kuvurumisha mvua ya makombora hadi ya supersonic kila mahali ndani ya Ukraine, Kyiv na miji mingine ilikuwa inashambuliwa sana kuanzia hospitali hadi shule za nursery za watoto.
Nimeshangaa kuona kuona kuna uvamizi au SMO ya wiki mbili sasa ndani ya mipaka ya Urusi katika eneo la Kursk majeshi ya Ukraine yakijivinjari ndani ya mipaka ya Urusi na kupelekea wakimbizi wa ndani wa Urusi zaidi ya 20,000 huku tukiwa hatujaona majibu ya majeshi ya Urusi mpaka sasa! Hii sio kawaida ya Putin kabisa ukizingatia mbele kidogo ya eneo hili kuna bomba la gesi linalopitisha 50% ya gesi kupeleka nje ya nchi.
Labda Putin ameisha amekuwa mdebwedo kabisa baada ya mipango yote ya uvamizi kuvurugika na kwenda mrama. Vinginevyo kuna uwezekano mkubwa anaandaa shambulizi "barbaric" la nuclear.