Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Pure Scientific

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
716
Reaction score
643
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.
 
Kwani ukiendelea na ajira huko na biashara huku utashindwa kusimamia?.... Biashara sijui ni upande wangu lkn kwasasa naona ni nzito sana!... Usiache kazi kwanza fikiria namna bora ya kuendesha biashara huku ukiwa kazini.
Kwa mshahara wa laki 3, bora akapige mishe nyingine.
Laki 3 means kwa siku anapata elf 10
 
Kwa mshahara wa laki 3, bora akapige mishe nyingine.
Laki 3 means kwa siku anapata buku 1.
Hizo anazo enda piga ana uhakika nazo? Kumbuka hapo ni volunteer tena ana miezi 6 tu3... bora ajibane mbeleni anaweza kuajiriwa Kama atakuwa na juhudi kazini... huku mtaani ana mishe zingine.... Kikubwa aweze tu kusimamia.
 
Kwani ukiendelea na ajira huko na biashara huku utashindwa kusimamia?.... Biashara sijui ni upande wangu lkn kwasasa naona ni nzito sana!... Usiache kazi kwanza fikiria namna bora ya kuendesha biashara huku ukiwa kazini.
Ajira ninayoifanya ni sawa na bure ujue.

Maana ni saa moja asubuhi hadi saa nne usiku.

So kwa siku lazima nitumie Elfu 5
Chakula 2000
Nauli 1000
Dharura 1000

So Elfu 5 kwa mwezi ni kama 150000

Hapo kodi 60000
Umeme 10000
Maji bili 10000

Jumla kama ya 230000

Nabakiwa na 70000

Kumbuka hapa nina mke njlimweka aende kwao akajifungue.
 
Naona kama nia unayo lakini sababu hauna...

UShauri tu, kabla ya kuacha kazi panga jambo utalotaka lifanya na namna ya kulifanya...
Asante nimefanya biashara nyingi sana.

Nyingine zimetoa nyingine zmepoteza.

Ila najiona napoteza sana muda kwa ajira maana ndanj ya miaka 5 nafanya make time nyingi tu mjini.
 
Ajira ninayoifanya ni sawa na bure ujue.

Maana ni saa moja asubuhi hadi saa nne usiku.

So kwa siku lazima nitumie Elfu 5
Chakula 2000
Nauli 1000
Dharura 1000

So Elfu 5 kwa mwezi ni kama 150000

Hapo kodi 60000
Umeme 10000
Maji bili 10000

Jumla kama ya 230000

Nabakiwa na 70000

Kumbuka hapa nina mke njlimweka aende kwao akajifungue.
Kaka maisha unayo ishi unayajua wewe.... .. kama unaona ukiacha kazi ndo utafanikiwa haraka sawa we acha halafu ingia mtaani uone. Kila la heri.
 
Back
Top Bottom