Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Ajira ninayoifanya ni sawa na bure ujue.

Maana ni saa moja asubuhi hadi saa nne usiku.

So kwa siku lazima nitumie Elfu 5
Chakula 2000
Nauli 1000
Dharura 1000

So Elfu 5 kwa mwezi ni kama 150000

Hapo kodi 60000
Umeme 10000
Maji bili 10000

Jumla kama ya 230000

Nabakiwa na 70000

Kumbuka hapa nina mke njlimweka aende kwao akajifungue.
Kwa maelezo yako naona unaishi juu ya kipato,kwa kamshahara hako unathubutu kupanga kwa 60,000 kwa mwezi,duuh
 
Habari zenu humu me ni kijana wa kiume umri wangu 24 ni fundi umeme wa magari nimejiajiri ila game ni ngumu sana huku mtaani hvyo natafuta kampuni au taasisi yoyote yenye uhitaji na fundi umeme wa magari pia nipo tayar kufanya kazi popote na pia kwa mwenye kazi hata nje ya taaluma yangu pia nina uwezo wa kusimamia magari, mradi pia ni fundi ambae ninayo mashine ya kupimia magari( Diagnosis machines). Hvyo nimekuja kwenu kuomba ajira kwa wenye fursa pia kama ww ni dalali wa kazi na unayo nafas ya kazi usisite nipigie 0653 271 318 malipo yako baada ya kupata kazi nitakupa pia kwa wenye uhitaji wa fundi wa umeme wa magari nipo nafanya kazi masaa 24 mda wowote na mahalii popote karibuni pia kwa services za gari zenu zenye matatizo ya umeme nipigie 0653 271 318 kwa kunipa kazi na kwa ajili ya mate matengenezo ya gari pia kama utahitaji msimamizi wa gari zako ili ziwe salama kwa muda wote pia me ni dereva wa pikipiki magari pia nina leseni yenye madaraja A A2 B D na E

Napatikana dar es salaam ila popote nafanya kazi

0653 271 318 piga au sms ntakujibu
 
Sasa unateseka na nn wakati serving ni 70,000/= maaha ndo baki baada ya matumizi yote Sasa fanya uwekezaji nunua line za kufanyia miamala au fungya min stationary
 
Ajira ninayoifanya ni sawa na bure ujue.

Maana ni saa moja asubuhi hadi saa nne usiku.

So kwa siku lazima nitumie Elfu 5
Chakula 2000
Nauli 1000
Dharura 1000

So Elfu 5 kwa mwezi ni kama 150000

Hapo kodi 60000
Umeme 10000
Maji bili 10000

Jumla kama ya 230000

Nabakiwa na 70000

Kumbuka hapa nina mke njlimweka aende kwao akajifungue.
Hiyo laki 3 ni basic or take home?

Saa 1 mpk 4 uck aisee hiyo mbona ni kipengele?

Unapoishi kuna mzunguko wa watu? Kwamba ukifanya boda utatoboa? Kwa wewe unavyoona?
 
Sio upande wako tu, kwasasa biashara ni ngumu sana mali hazitoki kabisa. Toka huu mwaka uanze hali ni mbaya sana aisee
Kwani ukiendelea na ajira huko na biashara huku utashindwa kusimamia? Biashara sijui ni upande wangu lkn kwasasa naona ni nzito sana! Usiache kazi kwanza fikiria namna bora ya kuendesha biashara huku ukiwa kazini.
 
Kwani ukiendelea na ajira huko na biashara huku utashindwa kusimamia? Biashara sijui ni upande wangu lkn kwasasa naona ni nzito sana! Usiache kazi kwanza fikiria namna bora ya kuendesha biashara huku ukiwa kazini.
Kumbuka huyo anatoka kazini saa 4 uck.. mshauri ukilizingatia hilo
 
Mshahara wako hauna tofauti na askari magereza.
Ila maisha haya njiani unamuona mtu kaulamba suruali kali shati imenyooka kiatu kikali ila Kichwani stress tupu mshahara kidogo +masaa ya kazi mengi.
 
Hio laki 3 kama haina ya ziada achana nayo. Jitoe kwenye utumwa wa kuajiriwa.
Msimu wa mavuno ya mahindi unakaripia tengeneza au nunua mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga,mtama, maharage, ngano,nk mashambani, kavune pesa mikoani.
Gunia moja KWA malipo ya debe moja,
Hadi msimu unaisha ukosi gunia elf 1000, Mtaji tosha.
Weka stop, msimu wa njaa uza mahindi, nunua mifugo kusanya boresha KWA kunenepesha uza kwa bei ya juu, ndani ya mwaka tu we ni wa tofauti.
Huu mzunguko unaweza ukaufanya mwaka mzima, kama ndio ajira yako ya kudumu.
 
Halafu watu wanaponda diaspora
Hiyo laki 3 mbona mshahara wa masaa 5 tu nchi zingine?
Kweli maisha magumu sana
True wao mshahara wa masaa huku unalipwa mwezi.
Mshahara wa Saa moja kule,bongo mtu analipwa kwa wiki. Hata mshahara wa siku bongo haufiki wa nusu Saa kule, kwa siku bongo viwandani wanalipa kuanzia sh elf 4 hadi elf 6,mtaani deiwaka kuanzia elf 10 KWA siku haizidi 15 na zote hizi ni kazi za suluba hadi utajuta kwann ulikimbia shule.
 
True wao mshahara wa masaa huku unalipwa mwezi.
Mshahara wa Saa moja kule,bongo mtu analipwa kwa wiki. Hata mshahara wa siku bongo haufiki wa nusu Saa kule, kwa siku bongo viwandani wanalipa kuanzia sh elf 4 hadi elf 6,mtaani deiwaka kuanzia elf 10 KWA siku haizidi 15 na zote hizi ni kazi za suluba hadi utajuta kwann ulikimbia shule.
Umemaliza kwa ghadhabu na ukweli mtupu

Kweli wizi hautaisha maana sio kwa hali hiyo
Na tatizo ni ajira pia kwani kama kuna kazi nyingi na mishahara ingepanda na hata kazi zingine hazihitaji elimu kihivyo
 
Kama moja ya hii idea, ukitaka business plan yake utapata.

IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kuwatengeneza kucha wadada
80.Utengenezaji mkaa
81.Udalali
82.Ufundi chuma
83.ufugaji nyuki
 
Kama hiyo kazi inakufanya una-survive iache kwa umakini mkubwa sana. Biashara sio kitu cha mchezomchezo. Kwenye biashara kuna muda unajiuliza kama uliletwa duniani kuja kuteseka??
 
Back
Top Bottom