Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Umemaliza kwa ghadhabu na ukweli mtupu

Kweli wizi hautaisha maana sio kwa hali hiyo
Na tatizo ni ajira pia kwani kama kuna kazi nyingi na mishahara ingepanda na hata kazi zingine hazihitaji elimu kihivyo
Akili ya blackman ni utumwa yaani kuuza mda wake Kwa muhindi, mwarabu, Mzungu au Mchina.
Ukitoka kwenye huo utumwa wa kuajiriwa ndipo mengi yatafunguka.
Kama Hakuna kamba ulipoajiriwa wewe unayasindikiza maisha
 
Hio laki 3 kama haina ya ziada achana nayo. Jitoe kwenye utumwa wa kuajiriwa.
Msimu wa mavuno ya mahindi unakaripia tengeneza au nunua mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga,mtama, maharage, ngano,nk mashambani, kavune pesa mikoani.
Gunia moja KWA malipo ya debe moja,
Hadi msimu unaisha ukosi gunia elf 1000, Mtaji tosha.
Weka stop, msimu wa njaa uza mahindi, nunua mifugo kusanya boresha KWA kunenepesha uza kwa bei ya juu, ndani ya mwaka tu we ni wa tofauti.
Huu mzunguko unaweza ukaufanya mwaka mzima, kama ndio ajira yako ya kudumu.
Duuuh Maisha yangekuwa rahisi hivi.!
Kwahiyo yeye hali Wala haishi hana matumizi yoyote na pia ni sehemu gani mtu anapukuchua gunia moja kwa debe moja.?

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Kama moja ya hii idea, ukitaka business plan yake utapata.

IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kuwatengeneza kucha wadada
80.Utengenezaji mkaa
81.Udalali
82.Ufundi chuma
83.ufugaji nyuki
Umesahau betting
 
Duuuh Maisha yangekuwa rahisi hivi.!
Kwahiyo yeye hali Wala haishi hana matumizi yoyote na pia ni sehemu gani mtu anapukuchua gunia moja kwa debe moja.?

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Maisha ni rahisi ukiwa na ability ya kuzisolve equation.
Nimeweka malipo ya debe sababu KWA vijijini mlipano wa cash wengine hawana.
Inatakiwa kupukuchua mahindi ujaze gunia moja ulipwe elf 2000 kila gunia.
KWA Saa mashine inapuchukua 2 au gunia 20.Mashine ni mobile unamaliza Kazi unaita pikipiki inavuta una hamia location ingine.
Ni project tayari pana mtu anafanya.
Mazao karibu mikoa yote wakulima utumia mikono kupukuchua au wanapiga kwa fimbo in primitives ways.
Atashindwa vipi kumeet daily cost wakati anaingiza pesa kwa pesa.
 
Ajira ninayoifanya ni sawa na bure ujue.

Maana ni saa moja asubuhi hadi saa nne usiku.

So kwa siku lazima nitumie Elfu 5
Chakula 2000
Nauli 1000
Dharura 1000

So Elfu 5 kwa mwezi ni kama 150000

Hapo kodi 60000
Umeme 10000
Maji bili 10000

Jumla kama ya 230000

Nabakiwa na 70000

Kumbuka hapa nina mke njlimweka aende kwao akajifungue.
Bro hutoboia hakika utoboi kazi si tatizo je mahesabu yanakubali? Au unafanya kazi mwisho wa siku unakuwa sawa tu na yule asie na kazi!
Kama expenses ni kubwa kuliko mshahara then hutoweza kusave,hutoweza kufanya investment, laki tatu ni nzuri kama ukishatoa matumizi yote

Mjomba fanya uchambuzi yakinifu then ingia mzigoni jiajiri uko unatumia akili zako zote


Ushauri wangu fanya kazi mwaka mmoja then kajiajiri save sana mshahara uo miezi iliyobaki iyo ndo utaanzia biashara
 
Zunguka vijijini ulizia migodi ya feldspar mwenye nayo hasa grey and shine ..Kama kashindwa kuendesha njoo inbox uniambie iwe na leseni tufanye kazi🏃🏃
 
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.
Acha ujinga wewe kitoto.
Tuliza akili kusanya kidogo kidogo uwe na capital ya kutosha kujiajiri sio matako kuwa kila mtu anayo

Jichunguze utaweza na je una passion n hayo mambo sio badae uanze kutupa story za mikono ya watu kwenye mikono yako
 
Tulia Kwanza kaka
IMG_20230221_184408_473.jpg
 
Mshahara wako hauna tofauti na askari magereza.
Ila maisha haya njiani unamuona mtu kaulamba suruali kali shati imenyooka kiatu kikali ila Kichwani stress tupu mshahara kidogo +masaa ya kazi mengi.
Ndiyo iko hivo mkuu, ila bora huyo aliye ulamba hivo.
 
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.

Ukiona huwezi fanya maamuzi mwenyewe ya kuacha kazi na kujiajiri ujue mda bado na usiache, unachopaswa kuuliza ni, nimeacha kazi, nimeamua kufanya biashara ya machungwa, wajuzi wa biashara nipeni ushauri.
 
Back
Top Bottom