Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Isikilize Sauti iliyopo ndani mwako. Niliwahi kumshirikisha mke na dadaangu kwamba Nataka kuacha kazi nitumie akili yangu kujijenga kiuchumi. Nilipata vitisho vizito sana na nikatishika lakini baadae Nikaja kugundua kwamba yanahitajika maamuzi magumu kuacha kazi na kipindi hicho nilikuwaga nalipwa laki6 take home. Lakini nikaingia kufanya mishe zangu kwa maamuzi Binafsi , baadae mke na dada wakaja kunishangaa maana Nikawa na limitless income Halafu muda Nikawa ninao wa kutosha kulea familia pia Nikawa huru kusimamia vitu vyangu. So Amua mwenyewe from your heart. Kama Sauti ya ndani hairidhiki uache kazi basi usiache ila kama ile Sauti imeridhia 100% hakuna kitakqchoharibika achana na hicho kikazi tengeneza pesa zako. Huo muda spend kutengeneza business.
Asante sana kaka .

Kwanza natumia muda mwingi sana kwenye kazi nisiyojua future yake .

Na ikiwa nimetoka kufanya kazi nyingi tu za kueleweka.
 
Wewe kwenye kujiajiri,vyote unavyo kasoro kimoja tu,uthubutu wa kuamua kuanza,
Unao mtaji,chombo Cha usafiri kukurahisishia mishemishe unayo,bado uthubutu wako na wazo la n nini ufanye ndo umekosa,
Unatakiwa usiogope kuamua ,watu wanaendesha biashara mtaji milioni,pesa inayozunguka kwenye uchuuzi Ni laki 4 tu na daily uhakika kukunja 15 Hadi 30
Asante sana kwa ushauri
 
Wewe ni volunteer halafu unasema unalipwa mshahara!!!!

Nyie vijana; kazi mnayo.
 
Habari zenu humu me ni kijana wa kiume umri wangu 24 ni fundi umeme wa magari nimejiajiri ila game ni ngumu sana huku mtaani hvyo natafuta kampuni au taasisi yoyote yenye uhitaji na fundi umeme wa magari pia nipo tayar kufanya kazi popote na pia kwa mwenye kazi hata nje ya taaluma yangu pia nina uwezo wa kusimamia magari, mradi pia ni fundi ambae ninayo mashine ya kupimia magari( Diagnosis machines). Hvyo nimekuja kwenu kuomba ajira kwa wenye fursa pia kama ww ni dalali wa kazi na unayo nafas ya kazi usisite nipigie 0653 271 318 malipo yako baada ya kupata kazi nitakupa pia kwa wenye uhitaji wa fundi wa umeme wa magari nipo nafanya kazi masaa 24 mda wowote na mahalii popote karibuni pia kwa services za gari zenu zenye matatizo ya umeme nipigie 0653 271 318 kwa kunipa kazi na kwa ajili ya mate matengenezo ya gari pia kama utahitaji msimamizi wa gari zako ili ziwe salama kwa muda wote pia me ni dereva wa pikipiki magari pia nina leseni yenye madaraja A A2 B D na E

Napatikana dar es salaam ila popote nafanya kazi

0653 271 318 piga au sms ntakujibu
Ungeingia katika site ya job ya Yapi merkez ukatupia maombi ingekuwa poa sana hasa kwa LOT 3 na 4 kwa ulivyojieleza ukashindwe wewe tu kwenye usaili.
 
Ndo fuatilia ili ujue hicho unacholipwa ni mshahara au ni kitu gani. Itakisaidia hata kwenye maamuzi yako unayotaka kufanya.
 
Ndo fuatilia ili ujue hicho unacholipwa ni mshahara au ni kitu gani. Itakisaidia hata kwenye maamuzi yako unayotaka kufanya.
Shida ni taasisi kubwa nimefuatilia kwa haraka haraka watu wengi waliiondoka hapa...wakapigiwa simu na kupewa mkataba
 
NSSF uliambatanisha vielelezo gani wakakulipa na pesa wanalipa kwenye akaunti au ni unapewa open cheque? Na vipi kuhusu makato hawana? Mkoa gani uliombea NSSF?

NAOMBA KUWASILISHA!!

Sent from my OPPO R11s using JamiiForums mobile app
 
Mshahara wako hauna tofauti na askari magereza.
Ila maisha haya njiani unamuona mtu kaulamba suruali kali shati imenyooka kiatu kikali ila Kichwani stress tupu mshahara kidogo +masaa ya kazi mengi.
Askari jela anaweza pata zaidi ya mshahara wake akiamua jilipua
 
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.
Wazo zuri kama una uhakika kutakuwa na maendeleo
 
Biashara gani ume plan kuifanya kwa 3mil.?

Mil 3 inaweza kutosha kabisa ukafanya biashara vizuri

au inaweza isitoshe na biashara ikashindikana kutegemea na gaharama za kuendesha biashara yenyewe ,
 
Biashara unayotaka kufanya, itachukuwa muda gani kukuingizia Tshs 300,000 kama faida kila mwisho wa mwezi..?
 
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.
 
Back
Top Bottom