Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Mkuu,

Naomba mchanguo Kama huu WA hiyo biashara unavyoenda kufanya?

Mpaka Sasa huu mchanganuo ni uhalisia Ila hiyo biashara yako Bado ni hisia Hauna uhakika Kama itakulipa ata iyo laki tatu Kwa Mwezi.

Mm nashauri iyo boda tafuta dereva mwingin uingie nae mkataba, piga miezi sita mwingine apo kazini na uwe na juhudi kweli kweli unaweza kuajiriwa mazima.

Kanunua nzuri ya kutoboa ni 1
1. Tafuta Nafasi
2. Ukishapata nafasi Onesha uwezo... Uwezo ni kufanya kazi Kwa bidii mara mbili ya inavyotakiwa. Ww Acha bidii yako iongee.
3. Ukionesha uwezo utaaminika.
4. Ukiaminika ndo mwanzo WA kupiga hela.

Siamini Kama utaendelea kuwa volunteer zaidi ya mwaka mmoja .
 
Kitu cha kwanza kabla kufanya maamuzi ya kuacha kazi ni kwamba, shughuli gani ambayo unataka kujishughulisha nayo na je, una mifano hai na tafiti za kujitosheleza kwa kufanikiwa kwake!!!??? Kuacha kazi ni suala jepesi sana ukiwa unajua wapi na ni kitu gani unakwenda kufanya na Una baadhi ya proves za unapokwenda kwamba kiasi gani unakwenda kufanikiwa. Usharudi wangu ni kwamba, usiache kazi kama hujui shughuli gani has unakwenda, kufanya, usibahatishe, bodaboda usiuze kwa kuongeza mtaji kama hujui shughuli yako ya kwenda kufanya ni ipi, mtaji mkubwa pekee si mafanikio, jua nini unataka kufanya na unahitaji kuwa na kiasi gani, fanya tafiti na ujiridhishe na unachotaka kufanya, jua mahali pa kufanya shughuli yako na usiwe dilemma kama ni Moro au Dom, yaani be specific, then amua, usiruhusu mawazo/ushauri mwingi kwenye maamuzi yako binafsi, maana wingi wa mawazo unakuondoa kwenye uhalisia wa njia yako ya mafanikio, jua ya kwamba katika huu ulimwengu kila mmoja ana jicho la mafanikio ambalo mwengine hubaki kipofu.
 
Biashara unayotaka kufanya, itachukuwa muda gani kukuingizia Tshs 300,000 kama faida kila mwisho wa mwezi..?
Sasa kwani mbona hesabu zako za kizamani.

Nikilipwa Mshahara wa laki 3.

Mahitaji ya Lazima.

Kulala 60000
Kula 100000 tuseme.
Nauli 40000
Sijavaaa.
Sina emergency.

Sasa wewe ukakadiria Laki 3 kama Faida umesahau hiyo hela ikija lazjma itoke.

Tofauti na nitakavyofanya biashara
 
Sehemu ninayojitolea kuna watu walionichoreea ramanj wamejitolea zaidi ya mwaka na hawajaajiliwa wameondoka wameenda Sehemu nyingine.

Mimi niliamua nifanye baada ya michongo yamgu kukwama tu.
 
Uko sahihi .. sasa basi hakikisha ukitoa gharama za kuendesha hiyo biashara mwisho wa mwezi ubakiwe na tshs 600,000.
Nasema hivi kwasababau kila biashara inahitaji backup mzee usijepata changamoto ukakwama .. trust me on this one
 
Shida ya vijana mmekuwa waoga sana wa kufanya maamuzi.

Mimi nilivyomaliza chuo ajira zilisumbua sana, nikaanza kufanya biashara nikafeli ikabidi nisambaze barua. Mungu saidia nikapata ajira ambayo haikunilipa vzr sana lkn after one year nikahama taasisi nika shoot salary ikafika mpaka 1m as take home... nimefanya hapo kwa miaka mitatu lkn nikaona maisha ni kama yale yale tu, yani ni kama kuna ka laana fulani kwenye kuajiriwa yani unapata mshahara lkn hausongi mbele ki maisha.

Nikachukua maamuzi nikasema naiacha 1m narudi kwenye biashara, Yes I did na nilikomaa kweli... sasa hvi nikiwaangalia wenzangu niliowaacha wanalipwa 1m na nikijiangalia na mimi niko mbali sana kulinganisha na wao, sana...

Nimefanikiwa sana sina shida ndogo ndogo. Thubutu bila hata kuomba ushauri hiyo ndio tafsiri ya kujitafuta.

Muombe Mungu ingia kwenye biashara, mtu akiingia vibaya kwenye anga zako malizana naye, usicheke na kima, akija kiswahili na wew malizana naye kiswahili, hakikisha unakua strict na biashara. Kwa sasa achana na pombe achana na wanawake. Narudia tena kwa herufi kubwa kwa sasa ACHANA NA POMBE ACHANA NA MADEM. Nyumbani baadhi ya isues funga vioo ukiona wameanza kukuita bahili ujue ndo mafanikio yanakaribia.

Kila la heri
 
Ningepata mtu kama wewe mwenye maono ya Mbali tukakaa tukashirikiana jambo flani naamini tungetoboa,

#enewei.
Kwakuwa umeomba ushauri, hata mm nliwah kupitia changamoto kama yako nkaachana na kazi ila mtaani ni pagum sana bro, usiache kazi kirahisi kwanza. Em tafakari kwa undani kwanza wewe kama wewe, pia umesema una mke je biashara ikibuma mama na mtoto itakuwaje,

Kwann hyo biashara unayotaka kuanzisha mke asiisimamie ww ukaendelea na kaz yako.

Bado najiuliza mengi japo najua kwa life hii 300k ni ndg.
 
Hakika kiongozi umeongea point nzuri sana kwa kweli mimi binafsi natendea kazi huu ushauri namshauri jamaa asome zaidi ya mara moja huu ushauri na imani atafnya makubwa kama anavyotarajia
 
Vp uliacha kazi? Tupe update
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…