Until_The_End
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 1,456
- 2,202
Wewe kama ni mgalatia, nimekusogezea hapa sheria kali;
Law 18:5-23 SUV
[5] Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA. [6] Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. [7] Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. [8] Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. [9] Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. [10] Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. [11] Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. [12] Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. [13] Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. [14] Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. [15] Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. [16] Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. [17] Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. [18] Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. [19] Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. [20] Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. [21] Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. [22] Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. [23] Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.