Napata wapi muongozo unaoonesha ni ndugu gani hawaruhusiwi kuoana na ambao wanaweza?

Napata wapi muongozo unaoonesha ni ndugu gani hawaruhusiwi kuoana na ambao wanaweza?

"Mmeharamishiwa {kuwaoa} mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na ndugu wa kike wa mama zenu {mama wadogo na wakubwa}, na binti wa kaka, na binti wa dada, na mama zenu waliowanyonyesha, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia, ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu, na {pia mmeharamishiwa} wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa pamoja dada wawili{mtu wa mdogo wake kwa pamoja} isipokuwa yale yaliyokwishapita, hakika amekuwa Allah ni mwingi wa kusamehe mwenye kurehemu.."

Qu'ran 4:23

Hivyo wale ndugu wa kunyonya pia wanaingia hapo, yaani kaka, baba, mjomba, mtoto wa kaka, mtoto wa dada n.k, wanakuwa haramu kwa kunyonya kama wanavyokuwa haramu kwa nasaba, haya ndio yaliyotajwa kwenye sheria ya kiislamu, na Allah ndiye mjuzi zaidi.

Braza Kede
 
wazee ndo wana miliki muongozo?
Wanajua Mila na desturi zenu. Kuna washindi watoto wanaolewa toka wadogo, waarabu baba mkubwa na mdogo, baadhi ya makabila binamu wanaoana.
Wao ndio wanaweza kukupa mwongozi kutokana na Mila zenu.
 
sasa haya wameandikiwa waarabu uko yanakupataje wewe mmatumbi wa ligangabilili mkoa mpya wa itilima?

Kwa sababu Qur'an ni Muongozo kwa watu wote hata kama ni wamatumbi. Qur'an haikuja kwa ajili ya waarabu peke yake, bali kwa watu wote. Ni Maneno ya Mola Mlezi wa Viumbe vyote na ni Muongozo kwa watu wote.
 
Usiteseke sana sheria ya ndoa ya 1971 imewataja watu ambao huruhusiwi kuoana nao.

Kama sijasahau ni Kifungu cha 14 cha hiyo sheria ya ndoa. Hicho ukikisoma utapata majibu ya uhakika kabisa

CC: Braza Kede
 
Wakuu sote tunajua kaka na dada hairuhusiwi.

Mtoto wa anko kuna jamii haziruhusu ila wengine wanaruhusu.

hivi kuna muongozo wowote mahali wa ndugu gani unaweza kuoana naye na yupi haurusiwi?

Je ni utashi tu au haya yameandikwa mahali?


Sijui utaratibu za kijamii, lakini kisayansi haishauriwi ndugu au watu wenye uhusiano wowote wa damu kuoana. (Binamu, mjomba, kaka, dada nk)

Hii ni kwa sababu kama ndugu au wenye uhusiano wowote wa damu wakioana wanaweza kuzaa watoto wenye matatizo ya aina fulani kiafya mfano magonjwa yanayotokana na VINASABA vya damu (Genetical diseases/disorders) kama vile Seli mundu (sickle cell disease), hemophilia, saratani (cancer) nk.

Kama ndugu wataoana basi kuna hatari ya kuwa na jamii yenye watu wanaosumbuliwa na aina fulani ya magonjwa yanayotokana na vinasaba. (Genetical diseases)

Mfano tuseme dada na kaka wakaoana na wote pengine wakawa na vinasaba vya ugonjwa wa Seli mundu (tuiite hivyo vinasaba "a") kwenye damu zao, yaani wao hawana Seli mundu bali ni wabebaji tu wa vinasaba hivyo ( yaani vinasaba vyao viko hivi: "Aa", ambapo A-ni kinasaba cha kawaida lakini "a-ni kinasaba cha Seli mundu). Hao ndugu wakioana basi miongoni mwa watoto wao watazaliwa na ugonjwa wa Seli mundu ( yaani watoto wote watakaokuwa na vinasaba vya "aa" watakuwa na huo ugonjwa wa Seli mundu (Sickle cell disease). Lakini watoto wenye vinasaba vya "AA" hawatakuwa na ugonjwa huo.

Dada (vinasaba: Aa) x Kaka (vinasaba:Aa) = watoto (ambayo vinasaba vyao ni: AA, Aa, Aa, aa)

(Aa x Aa) huzaa watoto (AA, Aa, Aa, aa)

Katika watoto hao yeyote mwenye vinasaba vya "aa" ni wagonjwa wa Seli mundu.

Kama hao watoto (AA, Aa, Aa, aa) wataendelea kuoana wao kwa wao basi ndivyo ugonjwa huo utakavyoendelea, yaani hautaisha.

Kwa hiyo ni muhimu sana kuepuka kuoana ndugu kwa ndugu au na wowote ambao mna uhusiano wowote wa damu. Ni muhimu kuchunguza historia ya mwenzako ili kujua mapema kama mna uhusiano wa karibu kabla ya kuoana. Pia inaweza ikatokea kwa watu ambao hawana uhusiano wowote wa damu wakapata hali kama hizo kwa sababu ya vinasaba vyao tu lakini mara nyingi magonjwa kama hayo hutokea hasa pale ndugu wanapooana.

Kila la kheri.
 
sasa haya wameandikiwa waarabu uko yanakupataje wewe mmatumbi wa ligangabilili mkoa mpya wa itilima?
Uislamu ni dini ya watu wote na Qu'ran haikushuka kwaajili ya waarabu, anyways nilijua unataka kujifunza kumbe ulitaka kupotezea watu muda, kwa kukusaidia nenda kwa babu zako wanaoabudu kwa matambiko ya kiafrika wakueleze nani anafaa kuolewa na nani hafai, asante.
 
Tumia akili yako ya kawaida - Common sense.
 
Wakuu sote tunajua kaka na dada hairuhusiwi.

Mtoto wa anko kuna jamii haziruhusu ila wengine wanaruhusu.

hivi kuna muongozo wowote mahali wa ndugu gani unaweza kuoana naye na yupi haurusiwi?

Je ni utashi tu au haya yameandikwa mahali?
Mademu kibao mpaka ukaanze kumlala ndugu yako mzee...kama mna Maradhi ya kurithi hayataisha kamwe.
Na mkioana ndugu hata kinga za mwili zinakuwa dhaifu
 
Kuna sababu gani ya lazima inapelekea kuoa ndugu au upungufu wa akili
 
Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act) kifungu cha 14
Nakuwekea version ya kiingereza nikipata ya kiswahili nitaweka pia
Screenshot_20250102-094221.png
 
Wakuu sote tunajua kaka na dada hairuhusiwi.

Mtoto wa anko kuna jamii haziruhusu ila wengine wanaruhusu.

hivi kuna muongozo wowote mahali wa ndugu gani unaweza kuoana naye na yupi haurusiwi?

Je ni utashi tu au haya yameandikwa mahali?
Mwongozo wa uhakikia ni elimu sahihi ya genetics.
Yeyote unayemuita ndugu yako, achana naye.
 
Wanaofuata dini ya mwarabu wanafata Mila za ajabu za middle east hasa wahindi na waarabu. Mtoto wa dada yake anaona, mtoto wa mjomba anaona mambo ya ajabu sana
Acha Upimbi Uislamu Ndo Dini Yenye Kupanga Ustaraabu Duniani Soma Hapa Kwenye Hii Aya Inapatikana Kwenye Surat Nisaai: 22-23.Wala msiwaoe Wake Walioa Baba Zenu,Ila Yalio kwisha Pita Hakika huo Ni Uchafu Na Uchukizo Na ni Njia Mbaya.Mmeharamishiwa Mama Zenu ,Na Binti Zenu ,Na Dada Zenu,Na Shangazi Zenu,Na Khaalat Zenu,Na Binti Wa Ndugu Wa Mume ,Na Binti Wa Binti Wa Dada,Na Mama Zenu Waliokunyonyesheni,Na Dada Zenu Kwa Kunyonya, Na Mama Wa Wake Zenu,Na Watoto Wenu Wa Kambo Walio Katika Ulinzi Wenu Walio Zaliwa Na Wake Zenu Mlio Waingilia.Ikiwa Hamkuwaingilia Basi Hapana Lawama juu Yenu(Pia Mmeharamishiwa)Wake Wa Watoto Wenu Walio Toka Katika Migongo Yenu,Na kuwaoa Pamoja Dada Wawili Isipokuwa Yale Yalio kwisha Pita.Hakika Mwenyezi Mungu Ni Mwenye Kusamehe Mwenye Kurehemu.Haya We Kafiri Toa Andiko Kama Hili Kutoka Kwenye Kitabu Chochote Cha Dini Kinachofundisha Ustaarabu Kama Huu.
 
Unaweza kusoma kwenye biblia kitabu Cha walawi 18:6 nakuendelea utapata jibu lako .
Mambo Ya Walawi Haitoi Jibu Ya Swali Alilouliza Mleta Mada.Mtoa Mada Tafuta Komenti Yangu Ina jibu La Swali Lako.
 
Back
Top Bottom