Napataje mawazo mazuri ya kuanzisha biashara? Kufikiria mwenyewe haitoshi kunipa wazo sahihi kwa asilimia 100.

Naona idea unazo ila ni ile jinsi ya kuanza unaanzaje wakoloni wanaita starting point ndio inakusumbua hapo Tafuta mentor au mzoefu kwenye hiyo Biashara unayotaka Kufanya akupe ABC

Kwa mfano hapo umesema unataka kufanya Biashara ya nafaka , Kuna dada Instagram anaitwa vale Nafaka ndio mambo yake hayo ya Nafaka ana uzoefu nayo na huwa anatoa na madarasa na mentorship , anatoa muongozo machimbo ya Nafaka, usafiri , n.k Kulingana na mtaji ulionao unaweza kumchungulia insta vale Nafaka ukaona. Hiyo Biashara ya Nafaka usikurupuke

Kuna Biashara zingine unaweza ukaanza tu , ila Kuna nyingine zinataka muongozo na connection fulani.

Kwahiyo ndio Kama hivyo. Kila la Kheri.
 
1. Biashara gani inalipa ?;

-Karibuni kila biashara inalipa inategemea unaifanya wapi na Kwa mfumo/utaratibu upi na wateja wako ni wakina nani.

2. Kwanini biashara fulani hufa mapema baada ya kufunguliwa ?;


Hizi ni baadhi ya sababu ninazo zijua.
A-usimamizi mbovu.

B-kukopa mtaji Kwa ajili ya kuanzisha biashara.

C-kukosa uzoefu kwenye biashara husika.

D-kubadili badili biashara, kushindwa kustiki kwenye biashara Moja Hadi kuielewa vizuri kujua faida utaipatia wapi.

E-kuwa na mshirika au msimamizi ambaye sio mwaminifu

F-kukopesha kopesha ovyo. kazi ya kukopesha tuwaachie waha na watani wao wakurya.
 
Jiepushe sana na mambo ya kuomba omba ushauri unapotaka kufanya jambo fulani.
Uzoefu ni mwl mzuri kuliko ushquri.
 
Asante, mkuu
 
Nimefanya kidogo biashara ya nafaka,kitu cha kuzingatiaa ni wapi unachukulia mzigo na wapi solo lako na je faida yake ni asilimia ngapi? Usidhani kila nafaka ukiitoa kijijini utanunua Kwa bei ya chini na ukiileta mjini utaiuza bei ya juu na kupata faida,bei ya mazao shambani na sokoni usipokuwa makini unaweza dhani ni kubwa,mfano unaweza kuta mchele unauzwa kamsamba Kwa 2000 ukileta Dar unauza Kwa 2800 sasa faida ya 800 Kwa kilo sio ndogo inategemea Una kilo ngapi,zingatia hicho kitu pia ubora WA bidhaa yako! Ukiweza Kwa hiyo 1.5 kununua mpunga Kwa wakulima Kwa bei ya chini then ukobowe ulete sokoni Ila zingatia tofauti ya bei uliponunulia na bei gani utaenda kuuza sokoni,na je soko lipo kweli ni uhakika? Nimesha wahi nunua mahindi singida vijinini Kwa 45000 gunia alafu mpaka siku naleta sokoni nakuta bei imeshuka watu wananunua Kwa 43000, hasa Dar,usilete bidhaa mpaka umejua soko la uhakika,mchele unaweza kuwa adimu huko shamba ukahisi Kwa kuwa umeadimika huku shamba Basi Dar au sokoni ukadhani huku ndio hamna kabisa,kumbuka Dar kuna mchele WA kutoka kila sehem Tanzania ila kamsamba hamna mchele unaoingia toka nje ya kamsamba zaidi ya kamsamba yenyewe! Fanya tafiti vizuri,cheza na namba vizuri utafanikiwa! Huwa nasikia pia mchele Zanzibar unalipa japo sina hakika! Kwa huo mtaji Anza na zao Moja Kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…