Nape kutolewa uwaziri sababu ya kauli yake ya kweli ya"mbinu za ushindi" si haki, maana hata aliyemtoa uwaziri naye basi ilitakiwa awe amefutwa kazi ( na sisi tukiomuajiri) kwa ile kauli yake kwamba "hata ukipiga kura kwingine, CCM ndiyo itakayounda serikali", maana kauli zote zinafanana.
Nimeamini kuwa Tanzania kuongea ukweli ni dhambi na kosa kubwa sana.
Nape hana uwezo wa kiuongozi kama ambavyo wengi wa mawaziri wasivyokuwa na uwezo, lakini hili la kuongea ukweli lazima apongezwe sana na sisi wapenda ukweli.