Nape anahusika vipi na Matukio ya Oktoba 29 hadi Tume kukutana naye? Au aliandamana pia?

Nape anahusika vipi na Matukio ya Oktoba 29 hadi Tume kukutana naye? Au aliandamana pia?

Siri yangu

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2023
Posts
2,252
Reaction score
4,839
TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 27, 2026, imekutana na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye.

Mkutano huo wa Tume na Nape umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ikiwa na lengo la kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.

46069.jpg


IMG_2009.jpeg
IMG_2008.jpeg
IMG_2007.jpeg
IMG_2006.jpeg
 
TUME ISISAHAU KULIHOJI NA KANISA KATOLIKI...MAANA WANASEMA WANADAI VIJANA WAO WAELEZE KINAGA UBAGA KUWA WALIWATUMA WANGAPI WAINGIE ROAD??
Mlio wauwa hapo tarehe 30 na kuwazika kwenye makaburi ya pamoja waliandania wapi?
Wale walipigwa risasi chooni je walikuwa wanaandamana?
Acha ujinga wako
Wauwaji wakubwa nyie
 
Tume inajua inachokifanya..

Wewe hujiulizi kwann hawajamuhoji kenani kihongozi? Hao watu wote wanao hojiwa wanacho cha kuiambia Tume, Kama ina masikio ya kusikiliza
 
Waenezi wote hata kama ni chawa kindakindaki ama waliwahi kuwa wajiandae kuuimba ulewimbo pendwa wa aaacha waisome namba eeehhh,kibano mbele kwa mbeleee.Hii ni sera mpya ya chukua chako mapema.Mwendoni kugawa urithi kwa wanagamilia.Kwani maisha yenyewe mafupiii acha mimi nitafune vyoootwee!
 
Hilo genge la vibaka limekutana na kibaka mwenzao ambae alisema uchaguzi mtu kushinda hutegemea na anayehesabu kura.


View: https://youtu.be/bsMYAk6cWaE?si=6b2zdnxtUwaH45HF

Vijana walioandamana walikua na lengo la kuzuia uchaguzi haramu na tume haramu maana kwa maigizo yale walioshinda sio chaguo la wananachi bali tumeccm na policcm.
 
Hiyo tume haina maana kabisa ni kufuja hela za wananchi tu huku huduma kama mashule na hospitali zikiwa hoi bin taabani.
 
Back
Top Bottom