Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri

Nape ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya 5 ilikopa mikopo mingi huku asilimia 40 ya mikopo hiyo ikiwa ni ya kibiashara hivyo kuwa na riba kubwa

Ameongeza kwa kutaka uchunguzi ufanyike juu ya mikopo hiyo na ilinganishwe na thamani ya miradi ambayo mikopo hiyo ilifanya

Ameipongeza Serikali ya awamu ya 5 kwa kuweka wazi mkopo wa 1.3 trilioni iliyokopa kitu ambacho hakikuwepo kipindi kilichopita na kutaka uwazi huu uigwe

 
Nape asisahau waliokuwa viongozi waandamizi wa hiyo serikali anayoilaumu ndio hawa waliopo kwenye serikali mpya anayojipendekeza kwao ili apate teuzi.

Na msilete zile sababu za kukariri kwamba wasingeweza kumzuia Magufuli kwasababu alikuwa katili, kama waliona tatizo lipo na halifanyiwi kazi wote wangetakiwa kujiuzulu ili kuonesha kutokubaliana nae, lakini kukaa kwao kimya maana yake walimuunga mkono.

Anyway, nimemkumbuka Nape siku ile aliyoenda pale ikulu baada ya kuomba msamaha, alipopiga picha na Magufuli akiwa ameweka mikono yake karibu na paji la uso kama vile anamsujudia mwanadamu yule anayemuita leo mwizi.
 
"Wapinzani walitukawiza Sana kuleta maendeleo" ilisikika minong'ono ya mamluki waeneza ujinga vichwan mwa wadanganyika.

Walivuruga chaguzi mbalimbali kwa tamaa za Madaraka, ili wajilimbikizie ufisadi watakavyo!

Walimfukuza aliyekuwa CAG, kwa chuki binafsi za kuwaumbua hadharani juu ya T.1.5 zilizoonekana hazielewek ziliko, wabunge CCM wote walikua wakifurahia!!

CCM Ni hasara kubwa kwa Taifa, hiki chama ndicho kinachelewesha maendeleo, kwa kufuga viongozi lukuki waroho wa madaraka na wezi wakubwa!
 
Safari hii lazima CCM wagawane mbao, chama kimepasuka ndani kwa ndani, kila mmoja anamsaka mchawi wake.
Hii ndio CCM Ina democrasia ndani yake sio Ile saccos ya chadema mwenyekiti alikuwa anawakata mishahara na posho wabunge wa wake na ni marufuku kuhoji na mpaka sasa hazijulikani zilienda wapi hizo pesa
 
Wachunguzeni wote Wanaolalamika KWA Sasa baada ya mwendazake kuondoka alafu rudini KWA historia zao za nyuma,mtapata picha halisi kwann wanalalamika sasa
Hii hali inayojijenga miongoni mwa wafuasi wa watawala, ya kutokutaka utendaji kazi wa Rais uhojiwe . Ni upumbavu .

Tunawachagua wanaadamu wenye mapungufu na ma Rais ni miongoni mwao. Acheni mambo yawe wazi
 
Huyu na ndugu zake nyumbu wa Chadema ni pete na kidole ,wote wanafanya siasa za maigizo huku wakiwaibia waTZ.

Awamu ya tano ilizibiti mijizi yote,sa hivi imeanza kuamka na kupiga kelele hoja mfu.Uzuri aliyepo ni mlengo wao ndo Mana wanapayukwa tu
1.5 trillion mlizikwapua
 
Nape asisahau waliokuwa viongozi waandamizi wa hiyo serikali anayoilaumu ndio hawa waliopo kwenye serikali mpya anayojipendekeza kwao...
Tanzania ya sasa hakuna kiongozi yeyote mwenye uthubutu wa kuwachia ngazi maana wote wanapigania matumbo yao.
 
Back
Top Bottom