Nape atishia kutoiunga mkono bajeti Wizara ya Ujenzi kisa barabara ya Kusini

Nape atishia kutoiunga mkono bajeti Wizara ya Ujenzi kisa barabara ya Kusini

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Akichanga mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma May 20, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, alisema amefika Bungeni akiwa na ujumbe mzito kutoka kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na maeneo mengine ya Kusini wanaotumia barabara ya Dar es Salaam–Kibiti–Lindi–Mtwara.

Alisema ameisoma randama ya bajeti hiyo na kubaini kuwa barabara hiyo haijatengewa fedha, hivyo akatangaza hataiunga mkono mpaka pale fedha hizo zitakapotengwa, kwani kuiunga mkono itakuwa ni kuwasaliti wananchi wa mikoa hiyo.
 
Kwahy ingepita kwao na wngn wangekosa angeipitisha? Wanasiasa bhana 😂
 
Back
Top Bottom