Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba

Kitu pekee kinachonipa faraja ni kwamba Nape ana umri mdogo,atazeeka na majuto na masikitiko kwa kusimamia uongo na uovu..malipo ya unafiki hapahapa duniani.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hski ya Mungu sikujua kama Nape ana akili ndogo hivyo! Yaani MABORESHO NI KUONGEZA CHUMBA- kwa mfano wake aliotoa! Ni mtu wa kufikiria uwingi na sio viwango (yaani Quantity na sio Quality) Bure kabisa. KUBORESHA KAMWE SIO KUBADILI na hili halina utata katika lugha zetu mbili kiingereza na kiswahili. Unaweza kubadili mtaala kwa maana ya kufanya kitu kipya kabisa lakini unaboresha kwa kuongeza au kupunguza baadhi ya masomo au muundo wa kufundisha! Huyu ni aibu kwa Chama Cha Mapinduzi! CCM wamekosa watu wenye akili zaidi ya huyo? puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 

Si umeona pumba zake hapo!
 
Waache wapige kura zao, ikipigwa kura ya maoni na Wananchi tutaikataa tutoke bila bila waanze upya.
Sidhani kama CCM hawalijui hilo, inaelekea kuwa hata huko kwenye kura ya wananchi wamejiandaa kisawasawa ikiwemo wizi wa kura.

Sasa hivi aidha kwa kujua au kutojua kivyovyote vile CCM wanampiga vita ya kisaikolojia Warioba (na wenye mawazo yake) ili wamshinde kisaikolojia kabla ya kuanza kwa bunge la katiba.

Wakifanikiwa kumshinda sasa hivi kabla ya bunge basi kazi itakayobakia itakuwa ni ndogo.

Ilitegemewa viongozi wanaotaka serikali tatu nao wakajitupa ulingoni sasa hivi na kuzitetea hoja za Warioba kabla ya bunge kuanza lakini wapi..
 
umbo la mwili la huyu mtoto na akili yake vitu viwili tofauti. maana yake kimo chake na hekima ni kama chumvi na mchanga!
 
Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa
Hilo sahau, labda kura kama hazitakuwa za siri... Wana CCM wengi chama ndo kinawabana..... Kwani Nimrodi Mkono na wenzie hawakupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu..?? kama ni mimi, hela nachukuwa na kura hupati...
 
Aliyo ongea Jaji Warioba juzi

"Kazi ya Bunge la katiba sio kubadili Rasimu" Joseph Sinde Warioba aliongea juzi haya

Majibu ya Nape jana


Nape Nnauye “Mchakato wa Katiba unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba; Bunge linaweza kuboresha na hata kubadilisha Rasimu.”

WE REPORT, YOU DECIDE
 
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
 
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Nape ni vuvuzela, unategemea mtu aliye pata div four awe na mchango wa maana kwenye hili taifa??
 
Mwisho wa nape utakuwa wa aibu sana! Hicho "cheo cha msimu" kimempa kiburi sana, sasa anafikia hadi hatua ya kutukana wazalendo wa kweli wa taifa hili.!
 

Aliyosema NAPE ni kweli, kama bunge lisingekuwa na mamalaka ya kubadili Rasimu kusingekuwa na haja ya kutumia pesa za walipakodi kwenda kupoteza muda wa miezi mitatu kujadili kitu ambacho hakiwezi kubadilika. Waryoba amemaliza kazi yake atulie sasa na bunge lifanye kazi yake.
 
Sasa jamani tulitegemea aseme nini wakati chama chake kinaamini kwenye serikali mbili na ufisadi?Tumsamehe bure ila tumuelimishe tu.
 
Mwisho wa nape utakuwa wa aibu sana! Hicho "cheo cha msimu" kimempa kiburi sana, sasa anafikia hadi hatua ya kutukana wazalendo wa kweli wa taifa hili.!

kwa hiyo wewe uko pamoja na yule mvuta sigara namba moja Tanzania(WARYOBA). Yule kalewa pesa za walipa kodi na kujiona yeye ndiyo kila kitu kwenye Katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…