Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

... Nape kwa hili yuko sahihi. Bando ni added service yenye masharti nafuu ili kuvutia wateja na mojawapo ya masharti hayo ni kikomo cha matumizi.

Ukiifanya huduma hiyo iwe ya lazima kwa kuitungia sheria sio kivutio tena bali ni takwa la kisheria which is not right. Itadumaza ubunifu na kuondoa ushindani.
 
Nape buana ni hopeless ,wanacnhi tunalalamika ,how come umenunua GB 1 ,baada ya dakika moja unaambiwa umeshatumia 75% ya bando lako ,hata kama kuna kitu kilikuwa kinarun background ndio kimalize 750MB ndani ya dakika 1 kwenye network ya kobe(2G/3G)? Hata kama kwenye 4G ndani ya dakika 1 hauwezi kumaliza 750MB.

Makampuni yanachofanya ni kuset price vibaya ,ni kama kwenye dakika ,ukiambiwa dakika 1 kwao sio 60seconds bali ni 45seconds na hivyo hivyo kwenye price ya MB.
 
Katika hili, Nape yupo sawa.

Mitandao ya simu inaweza kuamua ikafuta hizi huduma za bando maana huko zamani hazikuwepo. Tulikuwa tunaweka Vocha tunatumia hivyo hivyo.
 
Sijawahi ona nchi yoyote dunia hii, eti wakupe bando alafu isiwe na kikomo cha muda.. Hilo halipo, ila ukiwa hutaki bando, baki na hela yako unatumia bila kununua bando, which is very expensive..!!

Uwizi mkubwa unafanyika kwenye bando kuisha, yaani GB 2 au 3 say, unakuta within 3 hours haipo, kwa kuperuzi tu, huja download au upload chochote..!!
 
Nape anapaswa kuwa upande wa wananchi .

Kwanini anawasemea waendesha makampuni ya mawasiliano? Sisi tunalalamika kwamba huduma za internet zimekuwa ju Sana, hata vile vifulushi tulivyo kuwa tunatumia awali kwa bei inayo endana na uchumi wa wananchi wengi vimebadilishwa na kuwa ghari.

Sasa iweje awajibie hao anawao waita wawekezaji? Ndiyo kusema wamepandishiwa gharama za uendeshaji karibu marambili kama walivyo ongeza gharama hizo kwa wananchi?
Bahasha,
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Nape anaweza vipi kuwa waziri? MKe sioni uspecial alio nao ni wa kawaida sana
 
Kuna uwezekano mkubwa Serikali inajua inachofanya kwa haya makampuni kila mwezi, hasa Mwigulu Nchemba.

Huenda kila mwezi wanapandishiwa kodi/tozo halafu wanapewa ruhusa ya kuihamishia kwa wananchi, manake wameona kuweka tozo direct kelele zimekuwa nyingi.

Hicho ndio kinachofanyika. Hizo hela, zote ni serikali inachukua ndio maana Nape anajibu kwa Nyodo. Wananchi tungekuwa na umoja tugomee hata siku tatu kununua huduma toka kwenye hiyo mitandao tutaheshimiana.
 
... Nape kwa hili yuko sahihi. Bando ni added service yenye masharti nafuu ili kuvutia wateja na mojawapo ya masharti hayo ni kikomo cha matumizi.

Ukiifanya huduma hiyo iwe ya lazima kwa kuitungia sheria sio kivutio tena bali ni takwa la kisheria which is not right. Itadumaza ubunifu na kuondoa ushindani.
Mfano Airtel kama una salio la kawaida haikubali Data lazima ujiunge bando, hapo unasemaje?
 
Nape buana ni hopeless ,wanacnhi tunalalamika ,how come umenunua GB 1 ,baada ya dakika moja unaambiwa umeshatumia 75% ya bando lako ,hata kama kuna kitu kilikuwa kinarun background ndio kimalize 750MB ndani ya dakika 1 kwenye network ya kobe(2G/3G)? Hata kama kwenye 4G ndani ya dakika 1 hauwezi kumaliza 750MB.

Makampuni yanachofanya ni kuset price vibaya ,ni kama kwenye dakika ,ukiambiwa dakika 1 kwao sio 60seconds bali ni 45seconds na hivyo hivyo kwenye price ya MB.
Juzi nanunua bango airtel bango linasoma 1000 mb 500.. nilichopata ni mb 400.. anyway nilipima matumizi ya simu yangu ya bando hayaendani ualisia na makato ya mitandao ya simu.
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

% haijawai Muacha mtu salama, Sio kosa lake shida %
 
Tangu

Tangu nione sijazaliwa
 
Back
Top Bottom