Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Nape yupo sahihi bundles ni uwema wa kampuni kuturahisishia Sisi wananchi
 
Mkuu Nape

Bando Sio huduma ya ziada,ni muhimu Sana KWA ajili ya kupashana habari,maoni na kujenga nchi yetu!

Hata AJALI ya juzi ni matokeo ya Bando ndugu zetu wakapona,hata ushauri mbalimbali wa kusaidia Serikali Bando hutumika,pia linasaidia mzunguko wa fedha na uchumi!

Nguvu ya Bando Sio ya kubeza ,jitahidi Sana KILA mwananchi apate bando nafuu coz faida yake ni kubwa Sana kuliko kuipiga pin iwe KWA WACHACHE!

Mungu ibariki TANZANIA Mpya!
Tatizo hujaelewa, Bundle ni added service ( Huduma ya nyongeza ) ambayo hiari kwa kampuni kutoa

Leo hii makampuni ya naweza kufuta vifurushi vyao, na wasiwe na kitu cha kufanywa.
 
... Nape kwa hili yuko sahihi. Bando ni added service yenye masharti nafuu ili kuvutia wateja na mojawapo ya masharti hayo ni kikomo cha matumizi.

Ukiifanya huduma hiyo iwe ya lazima kwa kuitungia sheria sio kivutio tena bali ni takwa la kisheria which is not right. Itadumaza ubunifu na kuondoa ushindani.
HAYUKO SAHIHI HATA KIDOGO , SIMU UNAYOTUMIA SIO YA CONTRACT KATI YAKO NA KAMPUNI YA SIMU. SIMU YAKO IPO KWENYE HUDUMA ZA PAY AS YOU GO, KWAHIYO KAMPUNI YA SIMU HAIWEZI KUKUPANGIA MATUMIZI YA BANDO HATA KIDOGO
 
Na matumizi yalikuaje hiyo zamani bila bando?
SIMU UNAYOTUMIA SIO YA CONTRACT KATI YAKO NA KAMPUNI YA SIMU , SIMU YAKO IKO KWENYE FORMAT YA PAY AS YOU GO HIVYO BASI HUNA MKATABA NA MWENYE SIMU, HAWAKUPANGII MATUMIZI . NI WEZI TU WAKUBWA
 
Hakuna sehemu duniani unapewa service bila kikomo cha matumizi.

Ili wapate wateja inabidi matumizi yawepo
TEMBEA UONE , KUNA MAKAMPUNI MENGINE KAMA DATA ZAKO HUJAMALIZA ZINA ROLL UP MWEZI UNAOFUATA
 
Bando sio ziada ni kifurushi cha mkataba. Kinachobanwa kwa mkataba . Mkataba unaomsaidia mwenye kutoa huduma kulazimisha hela yako iwe ktk hesabu zake za kipindi. Na mara nyingine ni kama kuuza bia zinazokaribia kuexpore kwa bei ya promotions .
 
Hata ile kununua muda na kupewa SMS na mb . Sio offer kihivyo Ila ni mbinu ya kukuomjesha kitu ili utamani kuingia katika huduma ingine au wakuibie kama hutumii. Ila Katika hesabu imeju.liahwa ndani.
 
Kipindi kile alivonyolewa na mwendazake alikuwaga na point sana karudishwa ameanza tena michongo
 
Back
Top Bottom