Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria


Katika hili, Nape yupo sawa.

Mitandao ya simu inaweza kuamua ikafuta hizi huduma za bando maana huko zamani hazikuwepo. Tulikuwa tunaweka Vocha tunatumia hivyo hivyo.
Wafute alfu dah sijui wengine siyo watz hao nyinyi mmetoka Burundi ambako raia wenye smart phone hawafiki elf 50

Sas wee unataka kurudi huko nyuma Bora bao la Bab ako angepiga pool tu Kama ndio akili zako hz
 
Nape anapaswa kuwa upande wa wananchi .

Kwanini anawasemea waendesha makampuni ya mawasiliano? Sisi tunalalamika kwamba huduma za internet zimekuwa ju Sana, hata vile vifulushi tulivyo kuwa tunatumia awali kwa bei inayo endana na uchumi wa wananchi wengi vimebadilishwa na kuwa ghari.

Sasa iweje awajibie hao anawao waita wawekezaji? Ndiyo kusema wamepandishiwa gharama za uendeshaji karibu marambili kama walivyo ongeza gharama hizo kwa wananchi?
Binafsi naona majibu ya waziri yako sawa. Dando ni bidhaa iliyoko sokoni, uamuzi ni wako kuinunua au kuacha. Labda wadau tutoe mapendekezo swala hili litungiwe sheria itakayowaelekeza Hawa wenye makampuni taratibu za kufuata kwenya hivi vifurushi. Unless that, hawa wanafanya biashara halali.
 
Akiwa mwenezi wa ccm ndio hapo nilikuja kumuona huyu jamaa alikuwa hazipo bas kawa waziri katukuzwa na jpm

Akijikomba komba akenda kuomba msamaha

Amekuja amepewaa wizara tukajuwa Safi timepata mtu kumbeee Ni kiazi kitamu vibaya

Andelee tu na huu ujinga wake yaani
 
sasa wewe kodi unalipa? 😂 😂 😂 😂 hata ingekua mm, mtu anatoa mabilioni kila mwezi kwenye kodi peke yake alafu na wewe kutoa hata buku jero ya tozo unataka kwenda kufungua kesi mahakamani
Na lipa tozo mkuu😂
 
Wafute alfu dah sijui wengine siyo watz hao nyinyi mmetoka Burundi ambako raia wenye smart phone hawafiki elf 50

Sas wee unataka kurudi huko nyuma Bora bao la Bab ako angepiga pool tu Kama ndio akili zako hz
Najaribu kukuelewa mkuu, wala hakuna haja ya kejeli au lugha zisizofaa katika hili.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba, huduma za vifurushi ni huduma zinazotolewa kama hisani tu, mitandao ya simu hailazimiki kuwa na vifurushi hivyo ni ngumu kuwapangia.

Ni sawa na mtu alikuwa anatakiwa kukupa chai ya rangi kama wajibu wake ila ghafla akaanza kukupa chai ya maziwa, akiongeza au kuweka maziwa kidogo hakuna wa kumbana.

Hivyo ndivyo nilivyomuelewa Nape.
 
Hoja ya mbunge ipo sahihi kabisa bado lisiishe muda wake, maana umenunua kwa gharama husika.
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

 
Mbona kama vile wewe ni kichwa ngumu!! Umeelewa alichomaanisha kweli? Unaenda kununua bando promo yake ni 1GB, ila ukilinunua tu unajikuta unapewa mb 800 kwa bei ileile. Au umenunua sms 200, unatuma sms 10 tayari ujumbe wa kubakiza sms chini ya 7, ukituma 2 tu tayari zimeisha. Wizi huu upo hata kama wewe hujakutana nalo.
Upo sawa juu kichwa ngumu. Yeah, ni kweli mi wizi huo sijakutana nao ila nilipata kusikiliza voice clip flani ikieleza hivyo na mhusika yaonyesha ni mteja wa Zantel/Tigo. Hiyo siyo sahihi hata kidogo. Kwa mujibu wa voice hiyo, sababu kubwa ni kuto harmonize baina ya system mbili hizo ( promotion, makato na bando); japo hiyo bado si excuse kabisa.

Hata hivyo kilio cha watu kiasi cha Nape kujibu alivyojibu sio kwa mfano huo hapo juu.
 
Bamwe bashobora kwibaza bati ‘niba Imana ari Umuremyi mwizakandi urangwa n’urukundo, ni gute yashoboraga kurema ikiremwa cy’umwuka kibi, ari cyo Satani NAPE?’
 
sasa wewe kodi unalipa? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hata ingekua mm, mtu anatoa mabilioni kila mwezi kwenye kodi peke yake alafu na wewe kutoa hata buku jero ya tozo unataka kwenda kufungua kesi mahakamani
Hakuna asielipa Kodi hii nchi kila MTU analipa Kodi

Ukinunua hata Pipi dukani umelipa Kodi au hujui wewe taahira
 
Huyu kifutu bora wale wahuni wa Makonda wangemvunja kiuno tu mpuuzi sana
 
Mkuu Nape

Bando Sio huduma ya ziada,ni muhimu Sana KWA ajili ya kupashana habari,maoni na kujenga nchi yetu!

Hata AJALI ya juzi ni matokeo ya Bando ndugu zetu wakapona,hata ushauri mbalimbali wa kusaidia Serikali Bando hutumika,pia linasaidia mzunguko wa fedha na uchumi!

Nguvu ya Bando Sio ya kubeza ,jitahidi Sana KILA mwananchi apate bando nafuu coz faida yake ni kubwa Sana kuliko kuipiga pin iwe KWA WACHACHE!

Mungu ibariki TANZANIA Mpya!
 
Ina maana kati ya salio la kawaida yaani vocha na kifurushi kipi kipo kisheria na kipi ni promotion.?
Hebu nielewesheni
Salio la kawaida lipo kisheria kifurushi ni promotion
Sasa sisi Watanzania tunataka kama umeamua kunipa ofa basi unipe milele usibadilike
 
Back
Top Bottom