Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
~ Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ Aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga
~ Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.

"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza Nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema Nape

Nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.

Nape alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji Nape.

Akiendelea kufafanua Nape anasema,"Katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!
 
Katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nauye amedai kuwa fujo na vurugu zilizotokea bungeni pamoja na mikutano ya CHADEMA iliyokuwa ikifanywa kwa Helkopita,chanzo chakeni Pesa mabilioni yaliyotolewa na nchi za magharibi(Wazungu)kwa chama cha CHADEMA ili kuwawezesha kuvuruga mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya!

Source; Magazeti karibu yote ya leo.

Namuuliza NAPE kama Chadema wamepewa fedha na vipi kuhusu Cuf na Nccr?
 
Duh kumbe fedha toka ughaibuni ndizo zinarusha chopper angani?

Pamoja na anti-money laundering measures zote hizo pesa zinaingiaje hapa nchini? Serikali si izi freeze kama kweli zinakuja kwa nia ya kuharibu mchakato wa katiba.
 
mfa maji huishia kutapatapa... Nape ni janga la taifa, ccm kimeushiwa sera wanabaki kuropoka tu.. Tanzania ya sasa sii ile ya zamani wasome alama za nyakati kuwa watanzania hawaitaki ccm tena...
 
ni bora wanao pewa kuliko nyie mnao haha sasa hivi na SEMBE ili mpate pesa za uchaguzi 2015.
harafu hata kama wanavuruga wanalodai na kulivurugia lina mashiko kwa watanzania wengi
 
Huyu Nape akili mbovu tu kama za Ritz na post yake ya uongo jana kuwa Dr. Slaa anakwepa kodi.
Hovyo kabisa mtu mzima tena mwanaume unakuwa mmbeya! Kwahiyo ndio CDM walimroga Ndugai akawa mpuuzi na kutoa maamuzi ya kijinga kama yale? Aisee....Ndio maana alifeli Civics huyu.
 
Duuh!! Nchi yetu inayo watu wa ajabu sana. Hivi hayo maneno alikuwa anazungumza na wananchi wa ngazi gani au mrengo upi?

Pia, wakati anasema hayo maneno, hakukuwa na maswali, mfano; je, kati ya CCM na CDM nani aliweka suala la Katiba kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010?


Hata hivyo, NAPE NNAUYE, ni propagandist wa hovyo na tena ni mwongo anayetaka huruma ya wananchi wasiokuwa na taarifa sahihi juu ya mchakato wa katiba na wajibu wa CCM na vyama vya upinzani ktk kuhakikisha tunapata Katiba bora au mbovu.
 
Mwenzako Mwigu Kachamba alijipanga kuimaliza CDM imkala kwake sasa na ww albino naona unajitahidi nikuambie this time ni anguko lako
 
Wacheni kumtukana nape kaleta mada yake bora mujadili muhoji hizo hela anazo sema zimekuja kwa kuharibu katiba mpya zimeandikwa wapi?muu lizeni vizuri wazungu gani wametuma pesa na kwenye account ya nani?aweke data zote sisi wananchi tujadili na kama ni hela haramu bank kuu ipo lazima wanavielelezo vyakutosha tusikurupuke tu
 
Uongo mwingine uchukuliwe kama uchochezi. Ni zaidi ya propaganda. Sijui nieleze nini zaidi ya hapo. Hawa watumishi wa ccm hawana jema tena na nchi hii. Ni sikio lisilosikia kuielekeza tnz pasipotakiwa.

Kama karibia magazeti yote yana taarifa kama hiyo then we are trouble. Wameandika hivyo ktk uchunguzi upi wa kina.
 
Nape.....tafuta mbinu mpya kujibu hoja za washindani wako, hayo majibu kama ya polisi, nimekuwa nikiyaskia kwa zaidi ya mika 40 sasa, ...... hoja za Upinzani haziitaji kupewa hela, ni uelewa wa watanzania juu ya haki zao, ....nape unamaani kila jipya linaibuliwa na serikali ya CCm ni mawazo ya wazungu? maana ndio sera ya CCM, hatuwezi kuendelea bila uwekezaji! manaeo yamewafanya mnashindwa kifikili kabisa
 
Back
Top Bottom