Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nina wasiwasi na NAPE ndo walewale wanaoshikiwa akili zao kama NDUNGAI ambaye anaburuzwa kama mtoto ambaye hajui katoka wapi, Yuko wapi na anaenda wapi. Tena NAPE ajue kabisa Tanzania ya Jana sio ya Leo na ya Leo sio ya kesho. We are mature enough now!
 
Kama ni kweli CHADEMA wamepewa fedha kusaidia kukomesha hila za ma CCM kutaka kutuvurugia mchakato wa katiba mpya kwa kutaka kutuletea katiba ya CCM,binafsi nichukue fursa hii kuwapongeza sana hao wahisani na kuwaombea Mungu awazidishie moyo wa imani na Mapenzi katika kusaidia katika harakati za kumng'oa Nduli CCM.
Kama wa Tanzania tulio na Mapenzi mema na nchi yetu,tuwaunge mkono wahisani hao katika kufanikisha mpango wa Mungu wa kumng'oa Nduli CCM Tanzania
 
Aache kutuhada, umbea umbea tu.,kazi ipo 2015, majimbo 93% kwenda chadema.
 
MIMI naamini vyama vyote vikubwa nchini vina wafadhili toka nje ya nchi, tofauti hapa ni matumizi tu, kwani kutokana na fedha hizo wengine wameingia mikataba feki katika sekta mbalimbali kama vile madini, nishati, wanyama pori na kadhalika.
LAKINI MIMI naunga mkono chama chochote cha upinzani kitakachotumia fedha hizo kuhakikisha CCM inatoka madarakani kwa sababu ni janga la taifa, imesababi wananchi kukata tamaa na kuamini kuwa kwa sasa haiwezekani kupatikana kiongozi muadilifu. HUDUMA za jamii zimezolota wenye pesa tu ndio wenye haki.
 
NAPE NADHANI AKILI YAKE SIO NZURI KWA KUWA NAPE HUYU HUYU....NDIE YULE YULE ALIKUJA NA TAHARUKI KUBWA KUHUSU SWALA LA KATIBA AKILALAMIKA SIO SERA YA CHAMA,MARA HAWATAKI SERIKALI TATU ..YANI HUYU JAMA NI KIGEUGEU KULIKO MAELEZO..HAYA ANADIRIRKI KUDANGANYA WANANCHI ETI CDM WAMEHONGWA HELA NA MATAIFA YA NJE ..HII NI AKILI FINYU..AKUMBUKE HATA WANANCHI WENYEWE WANAJUA SIO WALE WA MIAKA YA TISINI ,SIKU HIZI HADI VIJJINI WANA MIREJESHO YA YOTE YANAYOFANYIKA..WANA ACCESS YA MAIL,WA INTERNET ..MITANDAO KM HII YA KIJAMII KM JAMII..YUTUBE,TWITER MABLOGS NA N.K KWA HIYO THERE IS NO ROOM TO CHEAT PEOPLE BHANA..SECOND PROPAGANDA ZA KITOTO ACHE...HATA HAO CUF,NCCR NAO WEMEHONGWA NA NANI??<PIA ANGALIE HATA MH.JK ANAVYOJUA SIASA HANA ADUI SASA WAO WANABEBA VISASI MIOYONI NA KUONGEA KWENYE MAJUKWA KAMA WATU AMBAO HAWAJAENDA SHULE..MFANO MFUPI NA WAKUIGWA NI KAMA ULE MH.RAIS ALIONYESHA KULE MWANZA..NDIO UKOMAVU WA SIASA,..NA PIA ANAJUA HAWA WAMECHAGULIWA NA WANANCHI WAKE HAO HAO.KWA HIYO CHA KUJIFUNZA HAPA KWA NAPE NA TIMU YAO WAWE WANASOMA ALAMA ZA NYAKATI..



Everything that can be counted does not necessarily count; everything that counts cannot necessarily be counted
 
Sassa nimeamini ndani ya Tanzania kuna baadhi ya wananchi wasio jua kwanini wanaitwa wananchi? Haiwezekani karne hii mtu asimame na kuhutubia wananchi na kueleza mambo bila kufafanua na kutolea ushaidi alafu wanachi wampigie makofi na kumwamini. Huyu nape anaona amefanya sawa kupotosha wananchi ila kwa vile akili zake ni zakiccm shauri yake kwani Watanzania wengi tunaelimu na aliofanikiwa kuwadanganya ni asilimia ndogo. Endelea nape alafu utapima ubora wa kazi yako 2015
 
Nape mbona anaidhalilisha serikali inayoundwa na chama chake?.Nape anadhihilisha kuwa serikali yake ya CCM ni dhaifu mpaka basi, kama kuna pesa chafu zinaingia na zinafikia hatua ya kutumika kuvuruga mchakato wa katiba bila mamlaka husika kujua na udhaifu wa hali ya juu sana wa serikali iliyopo madarakani.Suala la Madawa ya kulevya,pembe za ndovu limewashinda na sasa mmekuja na CD nyingine ya FEDHA HARAMU!!!!!!,, CCM achieni wapinzani waiongoze hii nchi nyie mume prove failure.
 
Mbona madawa ya kulevya hamyasemei majukwan huko,wakat vijana wanaangamia,washa geuzwa PUNDA wa watu?nyie mnajadil cdm tuuuu!!
 
Hii ni failure nyingine kwa CCM. Nyie mlivyo na chuki hivyo na CDM, mshindwe kweli kujua ujio wa hizo pesa kabla hazijatumika???.Ila kwa udhaifu wa serikali yenu ulivyo sishangai sana kwa maneno aliyoropoka NAPE,,, Kama madawa ya kulewesha yanapitishwa airport na bandarini bila nyie kujua??,huu ni udhaifu wa hali ya juu mno na hamstahili tena kuwa madarakani kwa vyovyote vile.
 

Nape Nape; kama debe tupu lisiloisha kutika!! kwa nini asiende mbele zaidi awataje hao wafadhili wa CDM wanaohatarisha mustakabali wa katiba na nchi?!

Nape akiitwa kwenye midahalo ya wazi anapata tumbo la hiari! kila mara anatafuta safe zones; ama kwenye vikao vya CCM, mikutano ya hadhara na press conference ndio analialia ovyo kwa sababu sehemu hizo hawezi kukabiliana na maswali magumu!!?

Nape if you are man enough; come forward and substantiate your allegations against CDM vinginevyo kulalamikia mvunguni mwa kitanda all the time does not help your cause to rescue your ailing CCM; grow up! you will soon be jobless>
 
Nape pia akumbuke hata bajeti ya nchi hii inayoongozwa na ccm ni tegemezi mpaka isaidiwe na wahisani,Chadema aiche kama ilivyo,mfa maji haaichi kutapata....
 
Haya ya NAPE ni majibu mepesi kwa maswali magumu mbona tumemzoea huyu Kiuno?

Nape kasahau kuwa unaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati mmoja lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote!!!

Kweli nimeamini CCM hawana tena jipya wamebakia tu na NGONJERA na HADITHI za Kusadikika!! CHADEMA NI KIBOKO na chama cha WANAUME na haijawahi kutokea tena CCM kupata UPINZANI MGUMU kama huu!
 
Duh kumbe fedha toka ughaibuni ndizo zinarusha chopper angani?

Pamoja na anti-money laundering measures zote hizo pesa zinaingiaje hapa nchini? Serikali si izi freeze kama kweli zinakuja kwa nia ya kuharibu mchakato wa katiba.

Nape anaropoka tu kuwadanganya wajinga wachache ambao hawajastukia utapeli wa ccm.
Kwa mtu yeyote aliye makini hawezi kuamini huu utumbo unaorushwa na Nape kila kukicha kwakukosa hoja mbele ya watanzania.

Serikali ni yao wenyewe kama kweli kuna pesa zinatoka nje kwa nia ya kutaka kuvuruga mchakato wa katiba wanashindwa nini kutumia government machinery kuzikwamisha?

Jambo la msingi hapa ni ukweli kuwa Ilani ya uchaguzi ya Chadema 2010 walikuwa wanakusudia kuanzisha mchakato wa katiba mpya wakiingia madarakani wakati ccm walitumia kampeni za 2010 kuikataa katakata hoja ya katiba mpya lakini walipoona nguvu ya umma kutaka katiba mpya inaongezeka wakaamua kudandia treni kwa mbele na lengo lao ni kuufanyia usanii mchakato wa katiba mpya ili tuendelee na katiba ya zamani kwa mgongongo wa katiba mpya ndio maana kwa kutumia wingi wao bungeni wamekuwa wakitunga sheria za kijinga zitakazowawezesha kuhakikisha kwamba nchi hii haaipati katiba mpya inayotokana na matakwa ya wananchi.

Kwa muktadha huo Chadema kama chama makini hakiwezi kukaa kimya na kuitazama ccm ikiharibu mchakato wa katiba kwa maslahi yao binafsi ni lazima kisimame imara kutetea maslahi ya wananchi wengi wanaotaka kuona nchi ikipata katiba mpya inayotokana na mawazo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…