Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

~ Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ Aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga
~ Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.

"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza Nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema Nape

Nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.

Nape alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji Nape.

Akiendelea kufafanua Nape anasema,"Katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!

Kuyaamini maneno ya Nape inatakiwa uwe na akili ya nyongeza.
 
Kwa hiyo CHADEMA walipewa hela ili waingize ajenda ya katiba mpya kwenye ilani yao ya uchaguzi, Kisha wakapewa hela ili Waisukume ajenda hiyo japo wao hawakushinda uchaguzi, Basi wakafanikiwa kuisukuma kwa ufanisi mkubwa, na sasa wamepewa hela ili waivuruge, na sasa washaanza kuivuruga?

Pengine mwenye majibu ya maswali haya anisaidie na mimi nipate kufahamu; CHADEMA walianza kupewa hela toka walipokuwa wakiandaa ilani ambapo katiba mpya ilikuwa ndani yake au wamepewa juzi tu walivyotoka bungeni? Ikiwa walipewa toka mwanzo; aliekuwa kawapa awali ndo huyo huyo kawapa juzi au ni mtu wengine!

Kama majibu hayapo; Rejea dalili za CHAMA kinachoelekea kufa kwa maelezo zaidi kuhusu anachoongea Nape..

Hizi ni propaganda zao chafu zisizo na mashiko! Wamezua mengi sana dhidi ya Cdm na wameshindwa! Sasa ata hili swala la Katiba mpya wameanza kuona watashindwa kulihujumu ndo maana wanaongea uongo bungeni na kwenye mikutano Yao! Macho yamebaki kwa Mwenyekiti wao kuwaokoa au kuwaaangusha! Kusaini huo muswada na kua sheria au kuurudisha bungeni kujadiliwa upya!
 
mbowe alidhihirisha kuwa kuishia form 4 ni tqtizo kubwa. alionesha jinsi uelewa wake ulivyo mdogo. kitendo cha kukigomea kiti HAKIKUBALIKI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nape ni vuvuzela wa ccm. Hana jpya hapa. Maneno ya Nape yangetolewa na karani tu wa John Mnyika, saa hii angekuwa central kuutoa ushahidi, lakini kwa kuwa yametolewa na Vuvuzela wa ccm, hakuna anayemwona kwani hiyo ndio sera yao.
Kwa nini Usalama wa Taifa wanajifedhehesha hivi? Yaani mabilioni yaingizwe nchini, sijui kwa mabox au kwenye account gani lakini mshindwe kuuliza walizipata wapi? Mpaka Nape amewaamsha lakini bado hamjachukua hatua?? Kweli dunia mhhhh.
Afadhali Nape hakusema Dr. Slaa alikwenda kuuza kitu huko amesema alienda kuomba msaada, Mwenye kiti wa ccm anazunguka kwenda kuomba Neti za kuzuia nzi wale wakubwa akaambiwa ati ni za kuzuia mbu. Jamani, namwonea huruma.
Pita mitaani, watu wamezifanya za kuzuia kuku wasiliwe na mwewe. Dah!
Pole sana Nape.
CCm mnawalinda wauza Sembe, waziri anasema, Hakuna mbunge wa ccm atakayepona wakitajwa! Maajabu gani haya??
nji hii.

Bandari ya Tanga imetajwa katika ripoti ya umoja wa mataifa kua ndo njia ya Mihadarati kubwa Kwa Africa mashariki! Leo Nape na yeye anatusaidi kutoa Ripoti Yake ya kuingizwa Fedha kwa minajili ya kufadhiliwa Cdm! Ikumbukwe kua aliwahi kuja na tuhuma za Cdm kuingiza silaha nchini na alipobanwa sana na kutaka kufunguliwa mashitaka na Cdm akawa kimya! Swali ni kwa hapo badae atakuja na Habari gani tena mpya?
 
Huyu ndio tegemeo la ccm kilaza nape nafikiri hata mkewe anafikira zaidi kuliko yeye
 
mbowe alidhihirisha kuwa kuishia form 4 ni tqtizo kubwa. alionesha jinsi uelewa wake ulivyo mdogo. kitendo cha kukigomea kiti HAKIKUBALIKI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Umelewa na buku7 wewe! Umeshapata viroba vingapi na jamaa yako Naibu spika na Nape wenu a.k.a Vuvuzela?
 
Katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nauye amedai kuwa fujo na vurugu zilizotokea bungeni pamoja na mikutano ya CHADEMA iliyokuwa ikifanywa kwa Helkopita,chanzo chakeni Pesa mabilioni yaliyotolewa na nchi za magharibi(Wazungu)kwa chama cha CHADEMA ili kuwawezesha kuvuruga mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya!

Source; Magazeti karibu yote ya leo.

Namuuliza NAPE kama Chadema wamepewa fedha na vipi kuhusu Cuf na Nccr?

Ni kweli maana Cdm hawakugoma bungeni peke Yao! Nccr na Cuf pia waligoma na kutoka nje! Sasa Nape atumbie hizo pesa wamepewa Cdm tu!?
 
Kwan nyie mafisadi hampewi fedha na wahsani pamoja na kutuibia wanyonge
 
Duh kumbe fedha toka ughaibuni ndizo zinarusha chopper angani?

Pamoja na anti-money laundering measures zote hizo pesa zinaingiaje hapa nchini? Serikali si izi freeze kama kweli zinakuja kwa nia ya kuharibu mchakato wa katiba.

Pole Kimbunga. Kwa uwezo wako, umefikia hatua ya kushindwa kuhoji akili ndogo kama ya Nape!?!?
 
CUF na NCCR je wamepewa hela pia kwenye hili?
Kweli CDM kiboko yao.

Ndio tatizo la hizi degree za madesa. Eti jamaa nae ana masters! Kweli hivi vyuo walivyosoma huyu jamaa na Lyatonga Mrema, ni kiboko!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kijana kama nape anaonekana kuwa ni muelewa ila nafikili kwa nafasi aliyo pewa aitendei haki nafsi yake maana HUU NDO UJINGA MKUBWA AMEWAI KUONGEA KULIKO WOTE ALIO WAI KUONGEA, ni kutokana na maneno yake yanaweza kuleta madhara makubwa nchini sema wao wanafikilia ccm tu awawafikilii watanzania wanaona wanaweza kuongea chochote.
 
Haaa haa haa ivi huyu Nepi cjui pampers alizaliwa akiwa katibu wa ccm au maana nimefikiri wee nimeshindwa pata jibu kua ilikuaje kati ya magamba woote tuliopo tukaona huyu kioja ndo apewe hicho cheo(jamaa anatia aibu kwa pumba zake isee)
Kila kukicha CDM wameingiza mabilioni sasa najiuliza wakati yanaingizwa serikali ilikua wikend ikila bata au?? Au yeye anataka labda wayapeleke Uswisi??
Nawalaumu wananchi wa Kahama kukaa wakimsikiliza huyu mtu muongo kutoka katika chama chetu badala ya kuendelea na shughuli zao!Kweli chama changu kimezeeka tujiandee tu kufunga safari iyo 2015
 
ni bora wanao pewa kuliko nyie mnao haha sasa hivi na SEMBE ili mpate pesa za uchaguzi 2015.
harafu hata kama wanavuruga wanalodai na kulivurugia lina mashiko kwa watanzania wengi

Kumbe amesikia "HEARSAY EVIDENCE IS NOT ADMISSIBLE"
 
Katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nauye amedai kuwa fujo na vurugu zilizotokea bungeni pamoja na mikutano ya CHADEMA iliyokuwa ikifanywa kwa Helkopita,chanzo chakeni Pesa mabilioni yaliyotolewa na nchi za magharibi(Wazungu)kwa chama cha CHADEMA ili kuwawezesha kuvuruga mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya!

Source; Magazeti karibu yote ya leo.

Namuuliza NAPE kama Chadema wamepewa fedha na vipi kuhusu Cuf na Nccr?
Ukabila ukashindwa,udini ukashindwa,ugaidi ukashindwa,ukanda ukashindwa,sasa wameibuka na jipya la ufadhili kutoka kwa wazungu sijui nalo itakuwaje?
 
Hahahaha tanzania eh!mwanangu kuwa uyaone ..nchi hi mkikubali kuendeshwa na wanasiasa tutakwisha wakati wakubwa wanapanda chopa wanasepa...hzo hela znazotumiwa kutembea na chopa c musaidie wenye shida...BLOODLY FOOL ...(cdm,ccm)
 
Kwa kiongozi mwenye hadhi ya kitaifa kuja na madai kama haya inatia mashaka sana hasa kutokana na nchi kwa sasa kukumbwa na wimbi la usafirishaji na utumiaji wa dawa haramu za kulevya sio ajabu wengi tumeshahathirika bila kujijua!
 
Ni aibu kwa kiongozi kama Nape kutoa shutuma kwa kudhani, eti atuambie alienda nje kufanya nini? Nape njoo na ushahidi ndiyo hoja yako itakuwa na mashiko. Vinginevyo mnapoteza pesa na muda kujalibu kuwahadaa wananchi.
 
Back
Top Bottom