Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Ndio maana kichwa cha nepi kimefanana na sabur kumbe ndio akili ilipohamia?vuvuzela una ushahidi au unaropoka kama unakata gogo?poor nepi.......
 
Ndio tatizo la hizi degree za madesa. Eti jamaa nae ana masters! Kweli hivi vyuo walivyosoma huyu jamaa na Lyatonga Mrema, ni kiboko!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums


Ndio tatizo lilipo kaka kwani Mkuu wa Magogoni kafanya kila kitu kuwa rahisi hata Urais siku hizi ni rahisi tu..
 
Albino na sisi ni watu tunaostahili heshima,,we mwendawazimu unayetutumia kama tusi kwa Nape Ukome kabisa.....
 
anadhani badi tuko enzi za udanganyika.
kama kiongozi mkubwa CCM anaongea pumba kiasi hiki je anaowaongoza?
hayo ni maneno ya mfa maji
 


"nasikia wamepewa mabilioni " alisisitiza Nape.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi?"

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga" alisema Nape.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko"

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!
Hiki ni kituko cha mwaka,jamaa anabwabwaja kama kakurupuka usingizini.
 
mbona maneno yako hayana mtiririko unaoeleweka. unarukaruka tu! mara hili mara lile. subiri viroba vimalizike kichwani ndiyo uchangie


Sawa Mliberali, kachukue buku 7 zako Lumumba tayari umechangia.
 
Inatia aibu sana, kiongozi wa chama anapotoa mambo ya kufikirika kwa kuunganisha matukio.
Nape alikuwa wapi kuueleza umma wa Watanzania kuhusu hizo fedha kabla ya vurugu za bungeni?!
Siasa ya bongo ni kuunga kuunga maneno tu......Aibu
 
Ili ujue kwamba nape ni hamnazo,anasema kwamba ''Nasikia wenzetu wamepewa fedha''anasikia kutoka kwa nani? Je amefanyia uchunguzi wa kina hilo swala?...katibu uenenezi unapanda jukwaani kwa maneno ya kusikia! Kweli nape kaishiwa anasubiri matukio ili apate la kusema.
 
~ Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ Aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga
~ Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.

"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza Nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema Nape

Nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.

Nape alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji Nape.

Akiendelea kufafanua Nape anasema,"Katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!
Huwa sijusumbui kusoma utumbo wa KILAZA aitwaye NEPIIII !! Crazy Idiot!!
 
Asa kama ndo ivo na wao ndo wanajua miamala yote ya pesa pesa izo zinapitia wapi!?! Basi hawako makini.....! Kama ndo ivo bas uwanja wa ndege pale wameweka vivuli. Ujinga wa NAPE ndo unaifanya CCM ionekane imechoka kupita vile nnavoweza kuielezea!
 
Pesa za wazungu ndo zinazoendesha nchi yetu sababu hata mwenyekiti wa ccm huwa anatuaga kwenda huko huko kwa wazungu kuhememia. Ungeanza kumkataza mwenyekiti wako ndo uwaseme chadema ingekua na mantiki kidogo vinginevyo ni zengwe la kisiasa tu.
 
Piga ua hakuna mtanzania wa leo anayeweza kukubaliana na madai ya Nepi, hata magamba wenyewe akina HK, MN wanajua Nepi kaingia cha kike!!
 
Mahitaji ya kambi ya upinzani kuhusu mswada wa katiba ni ya msingi kabisa,haihitaji propaganda kuwa kuna msukumo wa fedha toka kwa wafadhili.
Ni hoja dhaifu sana kwa na inashangaza kwa mtu wa hadhi ya Nape kutoka kihivo anajichora sana.
Asamehewe bure maana hajui atendalo.
 
Nape umeanza tena kuropoka jamani?unajuaje mwisho wa cdm we ni nabii utaweweseka sana cdm 2unasonga mbele
 
Back
Top Bottom