Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Huyu si aliwahi funguliwa mashitaka kwa uropokaji? Au alihonga ile kesi.
 
Adui mkubwa kwa maendeleo ya Tanzania ni ukosefu wa elimu ya uraia na mambo ya msingi kwa wananchi walio wengi. Jaribu kufikiria hayo maneno ya Nape, sijui alikuwa anaongea na watu wa namna gani na si ajabu walikuwa wanampigia makofi. CDM ndio waathirika wakubwa wa katiba hii mbovu iliyopo na tunaona mchango wao mkubwa katika upatikanaji wa katiba bora kikwazo ni CCM hili liko wazi, leo Nape anawadanganya wananchi eti CDM wanavuruga mchakato wa katiba. Aache kutumia uelewa mdogo wa wananchi kwa kuwarubuni na kuwadanganya.
 
  • Thanks
Reactions: prs
tunamuomba chadema mmoja ajibu hayo maswali.
1.je ziara ya doctor ndio imepelekea kupata mbinu za ki mossad za kuinajisi katiba?
2.pesa za chopa mnazitoa wapi? na je zinauzalendo?
3.chagua taifa moja kati ya yale yaliotutawala kiukoloni kisha ujaze kwenye nafasi ilio achwa wazi na nape.
4.hivi ni kweli kwamba chadema mmebaki na protocal ya katiba as a last card?

yapo maswali 200 kwenye hili
sumu na titikali zenu hala hala.
 
tunamuomba chadema mmoja ajibu hayo maswali.
1.je ziara ya doctor ndio imepelekea kupata mbinu za ki mossad za kuinajisi katiba?
2.pesa za chopa mnazitoa wapi? na je zinauzalendo?
3.chagua taifa moja kati ya yale yaliotutawala kiukoloni kisha ujaze kwenye nafasi ilio achwa wazi na nape.
4.hivi ni kweli kwamba chadema mmebaki na protocal ya katiba as a last card?

yapo maswali 200 kwenye hili
sumu na titikali zenu hala hala.

Hapo kwenye namba 2 fedha tunapewa na Nape ndiyo maana ana uhakika na anacho kiongea vinginevyo aulizwe mwenyewe fedha huwa anazipata wapi? asije akawa anawakwapulia watz au ana dili la kuuza sembe.
 
Nape umesema kweli kabisa lakini hata ccm mmo pia. Pesa ndio mungu wenu na shetani wenu wanasiasa wa tz. Tuliwaambia kuwa tatizo letu kuubwa katika katiba mpya ni hizo serikali mnazogombea? Mchaga kaona siasa inalipa lolote atafanya. Ccm imeonya asali haitaki kuachia. Mmelaaniwa wanasiasa wa tz. Mungu awaangamize msifaidi hizo pesa ziwe moto kwen
duh kumbe fedha toka
ughaibuni ndizo zinarusha chopper angani?

Pamoja na anti-money laundering measures zote hizo pesa zinaingiaje hapa
nchini? Serikali si izi freeze kama kweli zinakuja kwa nia ya kuharibu
mchakato wa katiba.
 
Hapo kwenye namba 2 fedha tunapewa na Nape ndiyo maana ana uhakika na anacho kiongea vinginevyo aulizwe mwenyewe fedha huwa anazipata wapi? asije akawa anawakwapulia watz au ana dili la kuuza sembe.

je hizo pesa zina uzalendo?,
embu banjuka zaidi.
 
nape andaa mtu wa kuwa mkuu wa kambi ya upinzani 2015 kwani imebaki miezi ishirini ccm kuwa chama tawala
 
tunamuomba chadema mmoja ajibu hayo maswali.
1.je ziara ya doctor ndio imepelekea kupata mbinu za ki mossad za kuinajisi katiba?
2.pesa za chopa mnazitoa wapi? na je zinauzalendo?
3.chagua taifa moja kati ya yale yaliotutawala kiukoloni kisha ujaze kwenye nafasi ilio achwa wazi na nape.
4.hivi ni kweli kwamba chadema mmebaki na protocal ya katiba as a last card?

yapo maswali 200 kwenye hili
sumu na titikali zenu hala hala.

Yani wewe unatumia hoja za Nape kuliza maswali?..Utakua Na mapungufu mengi sana...
Huwa hatujibu maswali kutokana na Hisia za watu.. kama CCM
Kama una ushahidi weka hapa..
 
Pesa za EPA zilihamishwa kwa mabox toka BOT na nyingine zilihamishwa kwenda kwenye account mbalimbali,hizi za CDM wathibitishe zimeingiaje nchini,CCM wanamiliki dola na wana uwezo na nyenzo zote,wachunguze watuambie,zile zilizofichwa Uswisw mbona naona kama haziongelewi?Wakishindwa kututhibitishia wananchi nitaamini NEPI ana wivu wa kike.
 
Yani wewe unatumia hoja za Nape kuliza maswali?..Utakua Na mapungufu mengi sana...
Huwa hatujibu maswali kutokana na Hisia za watu.. kama CCM
Kama una ushahidi weka hapa..

ni kweli nauliza kutokana na hizo tuhuma za nape.lakini hata hivyo siyo wewe tu bali hakuna kasuku yoyote anaeweza kujibu.
 
Anaposema amesikia CDM wamepewa mabilioni amesikia kwa nani? Kwa nini asitaje hizo pesa nani kawapa CDM hata kama amesikia kutoka kwa Mwigulu?? Anachosahau Nepi ni kwamba CCM wala hawakuwa na mpango wa kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya, Hata babu yake Kingunge alisema hivyo hivi katibuni kwamba katiba mpya haikuwepo kwenye ilani ya CCM. Sasa itawezekanaje CDM ambao ndio walikuwa wanataka katiba mpya leo wawe wavurugaji? Mbona Nepi anachoongea ni kinyume chake? Mdomo wa Nepi na akili yake huwa havina ushirikiano kabisa, akipewa mic aongee lazima ajichanganye.
 
Naona Nape yale madawa ya kujichubua anayoyatumia (carolite) yamepenya kwenye ngozi ya kichwa na kuingia kwenye ubongo hivyo anafikiria kwa kutumia carolite na sio ubongo. Hivi mtu mwenye masters degree anaweza kweli kuongea pumba kama hizo mbele za watu?
 
~ adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, chadema waliyapanga
~ ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ asisitiza ccm kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ aonyesha madai ya chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


katibu wa nec ya ccm itikadi na uenezi nape nnauye amesema kinachowasumbua chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya shinyanga, simiyu na mara ya katibu mkuu wa ccm taifa ndg. Abralhaman kinana.

"wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka katibu mkuu wa chadema dk. Wilbroad slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema nape

nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"hili walilofanya chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema nape.

Nape alisema ndio maana ccm ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji nape.

Akiendelea kufafanua nape anasema,"katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama cuf, nccr mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!

sina mengi lakini tujue kuwa, debe tupu halikosi kutita!
 
Huyu nae cjamsikia siku nyingi kafufukia wapi?
 
Mara nyingi fikra za mtu aliyemo kwenye box ,hutegemea ukubwa wa box alilomo. hayo ndiyo mawazo ya box alilomo Nape na msimlaum kwa lololte huo ndio uwezo wake ktk kuingamiza ccm na vilevile mjue madhara ya kitu cha kupewa bure bila jasho hakisaminiki na mpokeaji cku zote na ndiyo maana ataendelea kuharisha kwenye vyombo vya habari bila kukarishwa na chama chake.
 
Nape sisi si wajinga, kwa taarifa yako we ndiye mjinga na mchonganishi kama mwanamke, hongera sana kwa kujitahid kupotosha umma jinga kubwa we.
 
Wahenga walisema Waarabu hujuana kwa viremba!.

CCM wanawafahamu vizuri wahisani wa CHADEMA, na CHADEMA pia nao wanawafahamu vizuri wahisani wa CCM.

Hawa hawa kila siku huwa wanajaribu kutuaminisha kama watapelekana mahakamani kwa kashfa lakini matokeo yake hakuna kinachofanyika zaidi ya funika kombe achilia mbali mbunge yeyote wa CCM, CHADEMA au serikali kupeleka mswaada bungeni ili kudhibiti political donations.

Kitakachofuatia hapa ni CHADEMA na wawo kuja na santuri kuhusu CCM donors.

Hizi ndizo siasa za Tanzania.
 
Back
Top Bottom