Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Yaani hivyo viguzo vyenu viwili mlivyobakiwa navyo ndo mnapiga kelele namna hii???!!!
Kama mna Nguvu kweli mngekaa kimyaaa huko angani akaavyo mwewe tayari kututia makuchani.
Hiyo mikelele yenu ya majukwaani ni dalili kwamba mmejaa hewa mwashuzi ovyo.

FEDHA na BUNDUKI za UWT na JWTZ ndo zinawafanya mjiamini kiasi hiki??
UWT mnawamwagia fedha JWTZ wamechoka mlo uko kwa mabrigedia tu wengine wamejaa viraka ni walala hoi kuliko mlalahoi wa kawaida.
Tanzania siyo Zimbabwe wala Kenya msijidanganye na msidanganye watu wengine.
Hatusambaratiki, hatutawanyiki wala hatusambazwi.
waje UWT,JWTZ wote kwa pamoja watashindwa mbaya ndembe.

CHADEMA,We are here to stay and get rid of CCM,democratically,no matter all the evil ways CCM have used and those that will use to try to cling on POWER.

Nape anarudia tu kukisema kile ambacho watanzania wanakijua kuhusu chadema.
Kama walivyofanywa MDC kule zimbabwe, ndivyo watakavyofanywa chadema hapa.
2015 ni mwisho wa zama za CHAGA BOYZ katika siasa za tanzania.
Time is running out for you palz
 
Nape waambie watanzania kwamba una mashaka kwamba CHADEMA wamepewa hela ya kuwasaidia wauza madawa ya kulevya wapitishe madawa JKNIA bila kuonekana, waambie pia kwamba CDM wamepewa hela na wazungu ya kuwaajiri akina Kinana kuua Tembo. Waambie pia kwamba CDM wamepewa hela ya kufanya umeme uzimike na kuwasababishia wananchi mgao. Waambie kwamba fedha hizo walizopewa na wazungu wanazitumia kufelisha wanafunzi wa Form Four. Waambie pia kwamba hizo hela wamezitumia kufukuza wafanyakazi wote wa TAZARA na kuisababishia nchi hasara na usumbufu mkubwa kwa wasafiri. Waambie pia kwamba fedha hizo wamezitumia kumwajiri Mwigulu atengeneze video za ugaidi na kutengeza kesi ambazo zimeishia kufeli vibaya.
Mwisho waambie kuwa CDM wanatumia fedha za wazungu kukupeleka semina ya kusema uongo bila kumwogopa Mungu na kukunulia sindano ya ganzi ya kukufanya uone uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Vipi ile kombati yako umenunuliwa na CDM pia?
Jibu hoja ndugu.mbona unarukaruka kama umekalia sindano????
Huu ni mkakati mpya kuelekea 2015. Kuwabomoa hadi mbaki vumbi.
Na cha msingi ni kwamba ccm wanawajua zaidi watz na nyie mnawajua zaidi wachaga ambao ni miongoni mwa watanzania.
Kufikia 2015, mtakuwa dhaifuuuuuu na baada ya uchaguzi, chadema itakuwa historia.
Vipi mbona hamuongelei matokeo ya chaguzi za vijiji na serikali za mitaa hivi juzi??? Nina hakika mngepata japo 6% ya kura mngepiga filimbi mpaka pasingekalika.
Statistically, mmeshapigika na mikakati yenu ya nchi kutotawalika ime-fail vibaya sana na zaidi imewaweka uchi mbele ya jamii na kutoaminika tena
 
Jibu hoja ndugu.mbona unarukaruka kama umekalia sindano????
Huu ni mkakati mpya kuelekea 2015. Kuwabomoa hadi mbaki vumbi.
Na cha msingi ni kwamba ccm wanawajua zaidi watz na nyie mnawajua zaidi wachaga ambao ni miongoni mwa watanzania.
Kufikia 2015, mtakuwa dhaifuuuuuu na baada ya uchaguzi, chadema itakuwa historia.
Vipi mbona hamuongelei matokeo ya chaguzi za vijiji na serikali za mitaa hivi juzi??? Nina hakika mngepata japo 6% ya kura mngepiga filimbi mpaka pasingekalika.
Statistically, mmeshapigika na mikakati yenu ya nchi kutotawalika ime-fail vibaya sana na zaidi imewaweka uchi mbele ya jamii na kutoaminika tena

Jina zuri "Notradamme"
Hoja inafaa kwa malipo halali 7,000/= za Tanzania toka idara ya propaganda pale Lumumba.
Ongeza bidii hoja zako zaweza kufikia thamani ya Tsh 10,000 kila moja.
 
Ha haa haa haa......

Kama kweli Chadema inapata hela toka uzunguni na zinaingia nchini kiholela,basi hiyo ni moja ya dalili kuwa Serikali ya CCM iko hoi na nchi haipo salama.

Kwa nchi iliyo makini na imara haiwezekani ishindwe kudhibiti fedha chafu kama hizo halafu ibaki inalalamika kuwa Wapinzani wanapewa hela na Wazungu.

Serikali ina vyombo na mifumo inayoweza kutambua na kudhibiti upokeaji na utumiaji wa fedha hizi kama BOT.

Sasa Nape kutuambia kuwa Chadema wanapewa hela na Wazungu ni kutaka kutuhadaa tu Watanzania,ni kutaka kutuaminisha kuwa Serikali haina uwezo wa kudhibiti upokeaji na matumizi ya fedha hizo.Na kama kweli Serikali yetu haina uwezo wa kudhibiti fedha hiyo basi ni ukweli usiopingika kuwa Serikali ya CCM haina uwezo tena wa kulinda uchumi na maslahi ya Watanzania na hivyo iwaachie wanao:target:weza kudhibiti uchafu huu waongoze Nchi
 
We nape acha kuweweseka,watu wenyewe watachagua watu wanao wataka.unajuaje kama CHADEMA wamepewa pesa na wazungu?,kama sio unafiki huo? acha usamaki wewe!
 
inakuwaje cdm wavuruge katiba wakati ndiyo vinara wa kutaka katiba mpya!ama kweli muda wa kudanganya
sio huu,labda nape aliangalia hadhira aliokuwa anahutubia,siamini kauli kama hii anaweza kuitoa kwa watu wan
aoelewa!zama za kudanganya zilishapitwa na wakati.
 
Sijui ni Wachagga wangapi walimpa Ushindi wa Kishindo SUGU na ZITTO.
Tatizo la Ku copy and Past hata wakati wa kufikiri ndo hili.
Mpanda wamechagua Chadema, Iringa mjini wamechagua Chadema Tarime wamechagua Chadema.
Wachagga ni moja ya makabila yaliyotawanyika sana lakini Population yao si kubwa.
CDM kingekuwa chama cha WASUKUMA na WANYAMWEZI ningetamani kuamini maneno na ndoto zenu.
Akianzisha Chama mchagga ni cha wachagga akianzisha Muislamu hata akiwa mchagga ni cha Waislamu.
Watu mna ukosefu wa vitamini ya mishipa ya fahamu na ubongo.
Mapambano ni hatua na hatua zenyewe tulikwisha anza siku nyingi, ndiyo maana kule Bungeni kuna viti vyenye SUPA GLUU wenyewe wakikaa hawanyenyuki kama kiti cha Mamvi na Capteni Komba na vingine vina MBIGILI wakikaa wenyewe wanasimama kama cha Ndungai.

Nani kaweka Gluu na Mbigili kwenye viti???? CHADEMA.

Jibu hoja ndugu.mbona unarukaruka kama umekalia sindano????
Huu ni mkakati mpya kuelekea 2015. Kuwabomoa hadi mbaki vumbi.
Na cha msingi ni kwamba ccm wanawajua zaidi watz na nyie mnawajua zaidi wachaga ambao ni miongoni mwa watanzania.
Kufikia 2015, mtakuwa dhaifuuuuuu na baada ya uchaguzi, chadema itakuwa historia.
Vipi mbona hamuongelei matokeo ya chaguzi za vijiji na serikali za mitaa hivi juzi??? Nina hakika mngepata japo 6% ya kura mngepiga filimbi mpaka pasingekalika.
Statistically, mmeshapigika na mikakati yenu ya nchi kutotawalika ime-fail vibaya sana na zaidi imewaweka uchi mbele ya jamii na kutoaminika tena
 
Mawazo ya kitoto kabisa.... haya ni matusi mengine tena kwa watanzania.
 
Nape anatakiwa kujua na kuelewa kwamba Mtanzania wa mwaka 47 siyo mtanzania wa leo.Asome tu alama za nyakati.Ifike mahali siyo kila siku jumatatu.Na pia asiwe kama yule kipofu alipoonyeshwa TEMBO ikawa kila kitu kikubwa kama TEMBO!Watanzania wengi wameelimika kwa sasa.
 
~ Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ Aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga
~ Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.

"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza Nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema Nape

Nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.

Nape alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji Nape.

Akiendelea kufafanua Nape anasema,"Katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!

- Sasa nimeelewa kumbe ndio yamekuwa haya, I mean haingii akilini na mafuta wanayochoma na helikopta mahali ambapo magari yanafika kwa urahisi lazima ni mapesa mengi waliyonayo, hapa mjini wamenunua watu wengi sana tusiokubali kununliwa tunakuwa wauza unga na mashoga, hawa jamaa bwana sometimes huwa wananichekesha sana how they operate maana inajisema yenyewe kwamba wana mapesa ya bure huwezi kwenda na helikopta kuhutubia tu wananchi bila uchaguzi something is not very right na matumizi yao ya mapesa!!, Wanayatoa wapi?

Le Mutuz
 
Well said Nganasyo.

Like Makaburu wa Afrika kusin, then had HIRED SOLDIERS to fight for them.
CCM in twenty first century has HIRED DECEIVERS.
They get paid Handsomely by CCM to spread lies while swearing to GOD that they are telling the truth.
Guess who is Funding CCM???? Wazungu Wa Unga!!!!

Kama FEdha ndo ingekuwa kila Kitu Saudi Arabia ingekuwa First World.


inakuwaje cdm wavuruge katiba wakati ndiyo vinara wa kutaka katiba mpya!ama kweli muda wa kudanganya
sio huu,labda nape aliangalia hadhira aliokuwa anahutubia,siamini kauli kama hii anaweza kuitoa kwa watu wan
aoelewa!zama za kudanganya zilishapitwa na wakati.
 
Watanzania wa leo sio wa enzi za 80`s.watu wana uelewa mkubwa sana.Nape anavyoona watu wametulia wanamsikiliza anafikiri wanamkubali!!watu wametulia wanataka majibu ya hali ngumu ya maisha iliyosababishwa na CCM-bei duni ya pamba,wizi ktk vyama vya ushirika,kodi ya mifungo,huduma duni za afya,maji,elimu,watanzania wa leo katiba mpya maana yake ajira,bodi ya mikopo(HESLB) itoe pesa kwa wote bila upendeleo,mfumuko wa bei udhibitiwe,pembejeo,majosho n.k maskini NAPE auishi dunia tunayoishi sisi
 
Katibu wa Itikadi na uenezi wa Ujinga, sijui kama atafika mbali kwa Hoja zake za kuokoteza
 
Huyu Nape akili mbovu tu kama za Ritz na post yake ya uongo jana kuwa Dr. Slaa anakwepa kodi.
Hovyo kabisa mtu mzima tena mwanaume unakuwa mmbeya! Kwahiyo ndio CDM walimroga Ndugai akawa mpuuzi na kutoa maamuzi ya kijinga kama yale? Aisee....Ndio maana alifeli Civics huyu.

​Mkuu, unaweza kutupatia ushahidi hapo kwenye red ili tujiridhishe wenyewe?
 
Mtoto wa kambo wa Makamba huyo! kama anayesemekana aliyekuwa babake alikuwa fundi wa kupiga kinanda na kukesha usiku iliyokuwa magot lazima mwanae awe vuvuzela!Like father like son.
 
- Sasa nimeelewa kumbe ndio yamekuwa haya, I mean haingii akilini na mafuta wanayochoma na helikopta mahali ambapo magari yanafika kwa urahisi lazima ni mapesa mengi waliyonayo, hapa mjini wamenunua watu wengi sana tusiokubali kununliwa tunakuwa wauza unga na mashoga, hawa jamaa bwana sometimes huwa wananichekesha sana how they operate maana inajisema yenyewe kwamba wana mapesa ya bure huwezi kwenda na helikopta kuhutubia tu wananchi bila uchaguzi something is not very right na matumizi yao ya mapesa!!, Wanayatoa wapi?

Le Mutuz

Huu ndio mwisho wako wa kufikiri @Le Mutuz! Eleza fedha hizo ziliingia nchini lini? Aeleze majina na nchi walikotoa hizo fedha. La sivyo wewe nawe utakuwa una akili ndogo kama za panzi.
 
Back
Top Bottom