Elections 2015 Nape: Fisadi akipitishwa na CCM nitaongoza kundi la vijana kumpinga

Elections 2015 Nape: Fisadi akipitishwa na CCM nitaongoza kundi la vijana kumpinga

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Akiongea leo jijini Mwanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa kamati kuu ya CCM ndugu Nape Nnauye amesema kuwa hana msalie mtume na wanaotumia fedha kununua uongozi.

Aidha Nape Nnauye ameweka wazi kuwa endapo CCM itampitisha fisadi kuwania uongozi wa juu kwa tiketi ya chama hicho basi ataongoza kundi la vijana kumpinga.

Nape ametahadharisha kuwa anayetumia fedha kusaka uongozi ili kuwaaminisha wana-CCM kuwa anakubalika hana nafasi kamwe. Nape ameonya kuwa anayetumia fedha kusaka uongozi akishaupata ataanza kurudisha gharama alizotumia kwanza.
 
Namuunga mkono nape nami ntaungana naye kupinga hao mafisadi hatutaki hata kuwasikia wakale hizo pesa walizoiba inatosha sasa.
 
kama maneno ya Nape ni kweli kwa nini asituwekee wazi hao mafisadi ili sisi wananchi tusimuunge mkono kwenye udhamini? au ndio mtindo huohuo kama wa kinana anapolalamika kwa utendaji mbovu wa viongozi wa serikali lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa anabaki kupiga kelele kama kasuku
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Tutakuunga mkono Nape sie tunamtaka mzalendo Makongoro

juzi usiku nimemwona makongoro mitaa ya ufipa,sijui anataka kukimbia ccm!!halafu tabia yake ya kupiga misele na lile vx la east africa aache,yani mateja ya pale american chips kinondoni ndio washikaji zake...
 
kama maneno ya Nape ni kweli kwa nini asituwekee wazi hao mafisadi ili sisi wananchi tusimuunge mkono kwenye udhamini? au ndio mtindo huohuo kama wa kinana anapolalamika kwa utendaji mbovu wa viongozi wa serikali lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa anabaki kupiga kelele kama kasuku
Wanafahamika ni pamoja na Lowasa na kundi lake la mafisadi.
 
juzi usiku nimemwona makongoro mitaa ya ufipa,sijui anataka kukimbia ccm!!halafu tabia yake ya kupiga misele na lile vx la east africa aache,yani mateja ya pale american chips kinondoni ndio washikaji zake...

Unataka kusema nn ndugu
 
Kwanini watanzania wachache hawataki kuamini kama mafisadi wapo ccm !!!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Nape anatetea kibarua chake lakn maji yameshazidi unga ajiandae kwenda mipasho ama taarabu sababu kibarua kitaota mbawa muda si mrefu
 
Back
Top Bottom