Nape: Hata kama jina langu litakatwa sitakufa njaa kwa sababu nina elimu ya uhakika

Nape: Hata kama jina langu litakatwa sitakufa njaa kwa sababu nina elimu ya uhakika

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbunge mtetezi wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amesema haogopi jina lake kukatwa kwa sababu amesoma vizuri na ana elimu ya uhakika.

Akiongea kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape anasema yeye siyo mnafiki na yeyote atakayemletea " za kuleta" kwenye kampeni za Ubunge atamshughulikia hapo hapo.

Maendeleo hayana vyama
 
Sina shaka na elimu yake ya uhakika lakini mtaani kuna wenye elimu ya uhakika pia na wanakufa njaa. Yeye angeongeza kusema ana elimu ya uhakika, connection ya kutosha na ameshavuna mtaji wa kutosha kuendesha maisha kwa njia mbadala.
Ndio maana yake bwashee!
 
Huyu Nape ashukuru tu Mali alizochuma kupitia siasa kwa mgongo wa baba yake na CCM iliyombemenda tangu akiwa kinda.

Kuhusu elimu hana elimu ya kutosha labda awatishie kijijini kwake mtama,na itoshe kusema tu alionyesha upunguani baada ya sauti za ku 'msnitch' Jiwe kuvuja na kwenda kuomba msamaha huku kamasi zikimtoka njia nzima.

Huyu Ni mfu anayejizoazoa kisiasa.!
 
Mbunge mtetezi wa jimbo la Mtama Nape Nauye amesema haogopi jina lake kukatwa kwa sababu amesoma vizuri na ana elimu ya uhakika.

Akiongea kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape anasema yeye siyo mnafiki na yoyote atakayemletea " za kuleta" kwenye kampeni za ubunge atamshughulikia hapo hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Waajiri wengi au business partners wengi siku hizi hawapendi kufanya kazi/biashara na wanafiki.

labda ahamie sayari ya Mars!
 
Back
Top Bottom