Nape: Hata kama jina langu litakatwa sitakufa njaa kwa sababu nina elimu ya uhakika

Nape: Hata kama jina langu litakatwa sitakufa njaa kwa sababu nina elimu ya uhakika

Mbunge mtetezi wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amesema haogopi jina lake kukatwa kwa sababu amesoma vizuri na ana elimu ya uhakika.

Akiongea kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape anasema yeye siyo mnafiki na yeyote atakayemletea " za kuleta" kwenye kampeni za Ubunge atamshughulikia hapo hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Sio kwamba akajiajiri??
 
Sio mbwembwe mkuu yan ipo hivi, leo hii mfano ww ukiwa na degree ya social work, ukabahatika kuchaguliwa na kuwa mbunge baada ya miaka mi5 ukaukosa ubunge huwez kukubali kwenda kuajiriwa popote na social work yako kwa level ulioifikia kwahyo wabunge wengi vijana ndio changamoto yao na inakuwa hamba namna zaidi ya kupiga magoti kwa mkubwa ili kula yako iendelee, tofauti ya wastaafu mfano watendaji akiwa mbunge ata siku akiikosa ubunge anaweza kutulia sababu unakuta anamafao kipindi ameajiriwa alishafanya mambo mengi ya kimaisha tokea akiwa mtendaji kwahyo ubunge kwake unakuwa km extra money so ata next time akiukosa hana pressure tofauti na kijana ambae starting point yake ilikuwa siasa(ubunge)
Zile ni mbwembwe tu za kisiasa. Kiki bwashee!
 
Huyu Nape ashukuru tu Mali alizochuma kupitia siasa kwa mgongo wa baba yake na CCM iliyombemenda tangu akiwa kinda.

Kuhusu elimu hana elimu ya kutosha labda awatishie kijijini kwake mtama,na itoshe kusema tu alionyesha upunguani baada ya sauti za ku 'msnitch' Jiwe kuvuja na kwenda kuomba msamaha huku kamasi zikimtoka njia nzima.

Huyu Ni mfu anayejizoazoa kisiasa.!
Ccm mbona mnazodoana badala ya kupeana pole?
 
Nape alikuwa mmoja wa makada machachari sana awamu ya 4 ila kwa sasa kazimwa kabisa.

Kweli kila kitabu kina kurasa zake ila huenda akarudi tena kwenye kilele chake maana siasa haina mwenyewe.
Hana uwezo huo alibebwa tu na mfumo corrupt. Yuko wapi mtaalam Makamba Jr??
 
Elimu gani alonayo? Ya chuo cha diplomasia aliyositishiwa ufadhili na JK pale alipokataa kuondosha jina lake ili Nchimbi apite bila kupingwa? Je, ashamlipa Ladwa kwa kumpa mafuta ya ile landcruiser.
Land cruiser...!!! Pole.
The smallest minds often come with the biggest mouths.
 
Kumbe kilichompeleka kwenye siasa ni njaa zake na ili asife njaa, a bogus politician katika ubora wake. Fikiria huyu kesha wahi kuwa mmoja wa viongozi waandamizi katika chama tawala/dola kwa maana hiyo katika taifa.

Ndio maana wengine tuna amini wako watu wazalendo na wenye uchungu na taifa hili walio kunywa maji ya bendera huko nyuma ya pazia wanao hakikisha taifa hili halipotei na kuangamia.
 
Kumbe kilichompeleka kwenye siasa ni njaa zake na ili asife njaa, a bogus politician katika ubora wake. Fikiria huyu kesha wahi kuwa mmoja wa viongozi waandamizi katika chama tawala/dola kwa maana hiyo katika taifa. Ndio maana wengine tuna amini wako watu wazalendo na wenye uchungu na taifa hili walio kunywa maji ya bendera huko nyuma ya pazia wanao hakikisha taifa hili halipotei na kuangamia.
Wanasiasa wote wana njaa bwashee!
 
Atulie aache woga, amepanic mapema sana.. ni vizuri akikatwa na aachwe arudi duniani huku kuonyesha mfano kwa kujiajili...
 
Karibu sana Kigamboni Mh Paul Makonda..
Bila shaka Mh Paul Makonda anakuja kupeperusha bendera Kigamboni..
 
Huyu Nape ashukuru tu Mali alizochuma kupitia siasa kwa mgongo wa baba yake na CCM iliyombemenda tangu akiwa kinda.

Kuhusu elimu hana elimu ya kutosha labda awatishie kijijini kwake mtama,na itoshe kusema tu alionyesha upunguani baada ya sauti za ku 'msnitch' Jiwe kuvuja na kwenda kuomba msamaha huku kamasi zikimtoka njia nzima.

Huyu Ni mfu anayejizoazoa kisiasa.!
Lile la kuomba msamaha limemuacha mtupu
 
Mbunge mtetezi wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amesema haogopi jina lake kukatwa kwa sababu amesoma vizuri na ana elimu ya uhakika.

Akiongea kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape anasema yeye siyo mnafiki na yeyote atakayemletea " za kuleta" kwenye kampeni za Ubunge atamshughulikia hapo hapo.

Maendeleo hayana vyama!
Nape anaweza ugomvi? Mbona alionekana mikono nyuma akielekea kwa mkulu?
 
Back
Top Bottom