Nape: Kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu

Hapo ndo napowakubali CCM,ni wepesi kumaliza tofauti zao. vizavizabina watabaki wanaumbuka mchana kweupe.
 
Kumkosoa marehemu siku ya tatu akiwa kaburini baada ya ripoti ya CAG kuweka hadharani? Lazima baadhi ya walio fanya hivyo watalipia gharama ya kisiasa ni suala la majira na nyakati tu.

Kanuni hiyo ya CCM ya kujikosoa na kujisahihisha haikuweka hapo ili wengine wajivue utu na kujivika uhayawani.
 
Huyu mjinga naye hana lolote.
Si vizuri kum label mtu mjinga...

Lakini chamsingi hapa ni kuwa wanasiasa waelewe kwamba hii ni experience ya kwanza kufiwa na Rais madarakani.

Naamini wanaelewa nini maana ya ilani ya chama na kwamba hatukuingia kwenye uchaguzi mpya....Sasa kuanza kulinganisha moja kwa moja awamu zote as if zinafanana na hizi hapana si sawa!

Hii awamu inaendeleza kazi iliyokuwa imeanza lakini haikukamilika. Kwahiyo kama ni kuitafsiri katiba aawasawa kwa minajili hiyo ya mgombea mwenza kuchukua nafasi ni ili kutopoteza mwelekeo wa ile ilani iliyopigiwa kura na wananchi ambayo ndiyo mkataba wa raia na chama kilichounda serikali.

Hili tusilikwepe...Na mgombea mwenza aliinadi ilani hii, kwahiyo 2025 raia watakihukumu chama kwa kuangalia ilani ya uchaguzi na siyo kiongozi aliyeiongoza...Huu ni mtego wapinzani wana utega ili wapate agenda ya kukishinda chama kwenye uchaguzi ujao.

Mh. Rais ametumia akili sana kuzima hizi njama kwakuanzisha salamu yake ya "kazi iendelee" very intelligent mama Keep it up!
 
Hapo ndo napowakubali CCM,ni wepesi kumaliza tofauti zao. vizavizabina watabaki wanaumbuka mchana kweupe.
Naona umesalimu amri kwa kichaka cha 'kuzika tofauti'. Ulikuwa unapigana na njemba ukakomaa, lilipoanza kukuelemea ukaanza kuhimiza maridhiano
 
Tunaelekea kuelewa yupi ni yupi yuleeee. Sidhani kuna mstaarabu anayekataa kukosoa kwa lengo la kusonga mbele. Issue ni namna ya ukosoaji na wakati wake. Mlikuwepo kwenye chama mlikwama wapi kukosoa?
Acting smart, kumbe wana ulterior motives...Hawa watu ni kuwa nao makini sana...Watu ambao wapo kama popo usiku mnyama mchana ndege hawafai kabisa...Hawa sidhani kama wataweza ku withstand temptations wakiaminiwa kwenye mambo ambayo ni mazito na yanahitaji kujitoa kwaajili ya taifa...Ni mbegu mbaya kwa vizazi vyetu, hawa hata kwenye dunia ya walioendelea are not trusted ndiyo maana utakuta tunapewa masharti magumu kwakua hatuna misimamo!
 
......ndugu zangu legacy (alama) haitetewi inajitetea yenyewe.

Maneno muhimu
 
Hivi huyu sio yule Nape aliyepewa msamaha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…