Nape: Kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu

Kama mtu alikuwa dhalimu, na kufanya mauji, kuwabambikia kesi, kuhujumu shughuli zao wote wanamkosoa, unataka mbwembwe gani za kumkosoa? Anayetawala kidhalimu, anakosolewa bila kubembelezwa.
Shida ya MATAGA, hayataki kuamini kama zama za meko, zimekwisha, wanafikilia kuwa labda ni kama vile anaumwa hivyo mama samia amemshikia tu!!!kwa hiyo hana uwezo wa kufanya anayotaka yeye!ili mwenyewe aje aendelee tena!!!ila yataelewa tu.
 
Hawa watu huwa system ikiwatekeleza ndio akili zinawarudi.Mtu ambaye akili haijawahi kurudi hata akitelekezwa ni Bwana Lameck Madelu tu.Huyu ni bingwa wa kulamba miguu,nafikiri anayo PhD ya kulamba miguu 🤣
Huyu amelaaniwa
 

Na kukusolewa
 
Hata yeye mwenyewe alipojaribu kupinga mambo ya bashite nadhani hakuna asiyejua kilimtokea nini. Kuna watu wanaongea kama vile kipindi cha nyuma walikuwa wamezimia ndo wamezinduka baada ya mwendazake kwenda
 
Hivi nani alikuwa anapigia debe bao la mkono? Tuachane na hayo mwambie kama ana namba ya Kigogo2014 anitumie
 
Kama vile ya Nyerere wala haina mjadala lakini hii ya kulazimisha ya Mwendazake inatumia nguvu nyingi sana.

Maana hata shughuli zilizoamzishwa na JK na yeye kumalizia wanazihesabu ni legacy yake
Wala hakuna chochote kipya, labda kuiharibu tu nchi yetu, kitaifa na kimataifa kwa kauli tata!
 
Alianza Makamba kutandika jamvi la ukosoaji au kwa maneno mengine kusafisha njia, leo Nape na wengine watakuja kupita mulemule. Hiki ndo kizazi cha awamu ya 4. Kwa mujibu wa katiba yetu Rais Samia anao uchaguzi, ingawa ni mwembamba, wa kwenda na kizazi cha awamu ya 4 au 5. Ila awamu tano imefanya mambo iliyo yapigia debe vizuri na kuyaona kwa sasa uambiwi tazama la hasha.
 
Wanaojirudi kwa sasa na kukubali ukweli hata Mungu anawasemehe ubaya ni wale wanaoendelea kulazimisha mabaya kua ni mema.

Nimeelewa Legacy inajitetea kwa nini kutumia nguvu nyingi kuitetea ya awamu iliyokomea njiani?
Kila zama na kitabu chake yes.

Tukubali siku tutakua na Ilani ya Taifa na siyo ya chama ndipo tutasonga mbele kama taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…