Nape: Kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu

Maneno Kuntu.
Ujumbe murua kwenye zama hizi ambazo taifa lipo kwenye sintofahamu
 
Asante, yule kima hajaacha legacy yeyote zaidi ya kuharibu nchi yetu nzuri kiuchumi na mahusiano ya kimataifa.

Legacy haigombewi, huonekana kweupe tu
 
Inasemekana mkuu wa jeshi ndio aliomkingia kifua Mama, vinginevyo walafi wa vyeo walitaka kuharibu kabisa hali ya hewa baada ya kifo cha JPM.
Frankly speaking..hao jamaa wangefanya nini hata kama cdf asingestep-up?..
 
Tunaelekea kuelewa yupi ni yupi yuleeee. Sidhani kuna mstaarabu anayekataa kukosoa kwa lengo la kusonga mbele. Issue ni namna ya ukosoaji na wakati wake. Mlikuwepo kwenye chama mlikwama wapi kukosoa?
Ukitengeneza mazingira rafiki utapata kukosolewa na kusikia mawazo kinzani. Ila ukiwa mbabe unatishia maisha ya watu na kujiona wewe unajua kila kitu watu watakupa sifa nyingi sana.

Viongozi wa namna hiyo hata kwenye vitabu vya kale walikuwepo na waliishia pabaya.
 
Tunataka maendeleo maana CHADEMA walichelewesha maendeleo hatutaki blablaa nyiiiiingi mpo wenyewe wana ccm ktk vikao vya chama hilo sio bunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…