Nape: Magufuli aliposema Mwanza wasibomolewe kwa sababu ya kura alikuwa anatania

Nape: Magufuli aliposema Mwanza wasibomolewe kwa sababu ya kura alikuwa anatania

Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!
UTANI AU DHIHAKA ?

Maneno haya mawili hayafanani
Moja linawakilisha dharau lisipotumika vizuri ama kwa matamshi au wakati muafaka
 
Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!
Kaka najua una maana kwamba kauli ya Rais huwa haitaniwi, na kama mtu anabisha basi ajaribu kuifanyia utani kauli ya Rais yoyote ile ili ahakikisha maneno yangu.

Nape kwa hili kachemka, nafikiri bado hayupo sawa, ile kalinye kalinye iliyomkumba haikuwa ya kitoto.
 
Mpaka watakapobomolewa ndio tutajua ulikuwa utani, ila mpaka sasa bado hawajabomolewa kwa sio utani ni amri
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akiwa anahojiwa na DW amesema kitendo cha rais Magufuli kusema watu wa Mwanza wasibomolewe kwa kuwa walimpa kura ilikuwa ni utani sababu rais ni mtu anayependa kutania

Amesema pia ameshangazwa na bomoabomoa iliyofanywa kwa wananchi ambao serikali ilikuwa imewarhusu kujenga na kusema jambo hilo halifai

Ameseendelea kusema pia hana mpango wa kuhama CCM lakini hawezi kuapa kama hatahama chama hicho


Ila ninajiuliza, Nape ni msemaji wa serikali?
 
Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!
Ni wakati gani rais anatania au yuko serious? Yaani Rais akikosea anakuwa anatania, who knows? Hebu acheni unafiki
 
Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!
Mh, Mkapa kweli aikuwa na ethics za uongozi. Kuna siku nyuma huko akiwa Rais wa JMT, nilisikia maneno yake akiwa na watu wake wa karibu, wakimshauri aongee kitu fulani hivi. Yeye aliwaambia kuwa mimi ni Rais na nikiongea kitu chochote kinakuwa sheria, kwa mantiki hii lazima nichunge vitu vya kuongea hadharani. Sasa sijui kwa Pombe, ina maana yeye hajui kama ni Rais au?
 
Seriously, nanyi 'wasomi' mnashabika hili?! Acheni utani please! Basi mwambieni yeye kama kiongozi asilete matani kwenye maisha ya WaTz.
Oh Lord have mercy on you na Nape
Unbelievable
Nini mnatafuta ukuu wa wilaya mkoa au wenyeviti wa vijiji
Magu anaponzwa na wengi
Nchi za wenzetu huwezi kusema utani wa kipuuzi kama huu juu ya maslahi ya Taifa na watu wake

So Petro na Nape mnabariki Double Standards shame on you
Mwambieni Mkulu blue ni blue sio nyeusi

Tatizo mlienda TUITION hamkwenda SHULE
HII NI SAWA NA DEREVA WA GARI ALIOLETEA DRIVING LINCENCE NYUMBANI NA ALIEFUNZWA NA AKAFUNDISHIKA AKAPEWA DRIVING LINCENCE

KWANINI UNAMNUKUU VINAYA NAPE???lazima uelewe nini maana ya SIASA hilo la kwanza
Anaposema nadhani atakua anatania tu
Kwamba kura kapigiwa huko ni kitu kisichowezekana kusema hivyo kutokana na KUTOKUFAHAMU NANI ALIEKUPIGIA KURA

Pia kasema kua yeye ni miongoni mwa watumishi husika ktk swala la ARDHI
Na SWALA LA BOMOABOMOA WALISHA LIONGELEA SAANA,,sasa kwa msemo wa RAIS alivosema MWANZA,,huo UTAKUA NI UJUMBE KWA TANZANIA NZIMA
KWASABABU WALIOJENGA WALIPEWA VIBALI NA SERIKALI NA HII SERIKALI NI YA CCM
Sasa mkuu ulikua umeielewaje hio clip??????hadi ukamahutumu NAPE??
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akiwa anahojiwa na DW amesema kitendo cha rais Magufuli kusema watu wa Mwanza wasibomolewe kwa kuwa walimpa kura ilikuwa ni utani sababu rais ni mtu anayependa kutania

Amesema pia ameshangazwa na bomoabomoa iliyofanywa kwa wananchi ambao serikali ilikuwa imewarhusu kujenga na kusema jambo hilo halifai

Ameseendelea kusema pia hana mpango wa kuhama CCM lakini hawezi kuapa kama hatahama chama hicho


Angekuwa jasiri asingejibu swali hilo, halimhusu.
 
Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!
Mkuu usilete masihara kwenye kauli za Rais wa nchi.
Mnataka kudhoofisha heshima ya kauli za raisi. Kwa maana nyingine kauli zake zisitiliwe maanani? Mbona mengi ayasemayo
kama kutumbua watu hadharani hamsemi kuwa alikuwa anatania.
He knows what he says and why he says that at such a particular place and at that particular time.
Don't enjoy watanzania.
 
Nakubaliana na Mbunge Nape Nnauye. Ule ulikuwa utani wa Rais kwa wananchi wake. Lakini,kauli za Rais ni very sensitive!

Mkuu Petro, sentensi yako ya mwisho ni angalizo la msingi, si kwa Rais tu ila viongozi wote, hasa wa kisiasa, ili kulinda ustawi wa kijamii katika maelewano na ushirikiano.

Hoja ya Mh Nape kwamba kauli ya Rais ilikuwa utani lakini tukaichukulia kuwa ni agizo sensitive ni hivyo hivyo matamshi na kauli za viongozi wa kisiasa (km uongozi wa hovyo hovyo, udikteta uchwara, serikali ya mauaji, nk) zinavyochukuliwa kuwa ni sensitive. Hivyo basi, kuikuza hiyo kauli ya Rais peke yake tu kisiasa, kunahatarisha amani katika jamii.

Mimi naamini kauli ya Rais haikuwa utani ila agizo sahihi lilitolewa wakati mwafaka, kwa jamii husika lakini yenye ujumbe mpana unaogusa maeneo yote yanayovamiwa, na wavamizi wote ni wapiga kura. Ukiisikiliza hotuba yote, hasa kuhusu bomoabomoa, tafsiri inayotolewa siyo sahihi kabisa. Hata juzi Kagera karudia wito wake ule ule kuachana na bomoabomoa zisizo na utaratibu.
 
Back
Top Bottom