Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

[HASHTAG]#KutokaBungeni[/HASHTAG]: Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.

Kwa hiyo????!!!!!
 
Kama ilivyo kuwa katiba mpya, hili nalo litapita2
 
[HASHTAG]#KutokaBungeni[/HASHTAG]: Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.
Ndiyo ajue kuwa ilani si katiba na haitekelezeki isipokuwa mipango yake ikipitishwa bungeni au baraza la madiwani na kufanywa mipango ya serikali. Watu wanapiga kelele kila siku kuhusu utekelezaji wa ilani kana kwamba ni automatic. Ilani si chochote isipokuwa kama imeridhiwa na vyombo vya dola kutekelezwa kama mpango wa serikali.
 
Bila kumng"unya maneno Nape sasa amekuwa barrier kwa policies na mtazamo alio nao Rais JPM. Hapana shaka tangu atenguliwe kwenye nafasi ya uwaziri kwa kiasi kikubwa has positioned himself as an agent of the opposition ndani ya chama chake tawala. I wonder, CCM kama chama kina mtazamo tofauti na JPM kuhusu mradi wa Stigler's as long as ni mradi as maendeleo. Inatosha to conclude bila chembe ya aibu kwamba matamko na critics za Nape kuhusu maamuzi ya Rais ni issue ya personal grudges towards the president. And as such, ningetamani kuona anawajibishwa accordingly.
 
Basi ata stiegler gorge ilikuwepo tokea enzi za Nyerere pia mkuu.

Nape kaonesha dhahiri ana chuki dhidi ya Mheshimiwa tokea afutwe Uwaziri.
Stiegler gorge hata kipindi cha JK iliongelewa sema haikuanza kutekelezwa tu, nadhani Nnape angeuliza tu kama suala la gas limeachwa au vipi? Maana kama tumeachana na mradi wa gas kweli basi tunafanya makosa makubwa sana. Ni bora tungemaliza mradi wa gas kwanza then tuanze na stieglers gorge. Tunahitaji umeme wa kutosha hasa if we real want an industrialised Tanzania.
 
Bila kumng"unya maneno Nape sasa amekuwa barrier kwa policies na mtazamo alio nao Rais JPM. Hapana shaka tangu atenguliwe kwenye nafasi ya uwaziri kwa kiasi kikubwa has positioned himself as an agent of the opposition ndani ya chama chake tawala. I wonder, CCM kama chama kina mtazamo tofauti na JPM kuhusu mradi wa Stigler's as long as ni mradi as maendeleo. Inatosha to conclude bila chembe ya aibu kwamba matamko na critics za Nape kuhusu maamuzi ya Rais ni issue ya personal grudges towards the president. And as such, ningetamani kuona anawajibishwa accordingly.
Nadhani sio yote aliyoongea ni ya hovyo, tuchukue yale mazuri tuyafanyie kazi na yale ya hovyo tuyaache. Kwanza ni vyema tukajua je ni kweli issue ya gas imewekwa pembeni? If not then ajibiwe tu. Je issue ya mbaazi na korosho ni kweli? If not ajibiwe tu. Ila kusema stieglers gorge haikuwepo kwenye ilani so isitekelezwe hapo ni kupitoka, rais akitekeleza ya kwenye ilani na akaenda extra mile inapendeza so long as ni kwa maswali mapana ya nchi. Na pia kama kuna miradi ambayo ni white elephant projects akaamua kuiacha hata kama ipo ndani ya ilani sio kosa kabisa, kosa ni pale kama ataacha miradi yenye tija na maslahi mapana kwa taifa na kutekeleza miradi isitokuwepo kwenye ilani na haina tija wala maslahi mapana kwa taifa.
 
Malaika mtukufu hana miradi mikubwa so kaamua atekeleze miradi yake naye aache sifa kuwa alifanya kitu hii ndio trend ya viongozi wetu akija mpya anakuja na yake hatuna continuation
 
Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.
Huyu hajui kuwa UMEME wa gas ni very expensive sana, UMEME wa maji ndo mpango mzima Dunia nzina, wanategemea UMEME wa maji, makaa ya mawe, wind turbine, nuclear energy, UMEME wa gas ni kwa ajili ya emergency tu.
 
Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.
Huyu mbunge kwa sasa naona angeendelea kukaa kimya. Kwenye ilani ya uchaguzi kulikuwa na kipengele cha kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima pamoja na vijijini. Hivyo basi kutokana economic projection inayohusiana na nishati imeonekana ni busara kutap cheap hydro electric energy ya Stiglers' ambayo imekuwa kwenye makabrasha miaka mingi na ilishindikana kwa sababu ya raslimali fedha. Kwa sasa pengine serkali imeona ni wakati muafaka kutekeleza mradi huu ambao utaongeza nishati hii rahisi maradufu ili iendane vizuri na sera ya viwanda.
 
Mhe. Nape labda ana hoja. Ni kweli wawekezaji wanaikimbia Mikoa ya kusini. Juzi nimeshuhudia kupitia luninga kuwa kwa sasa mahoteli ya Mtwara yanajaza kwa asilimia 15% mpaka 20% kinyume na hapo mwanzo. Pili hoja ya Stieglers Gorge nayo ina mashiko. Nadhani CCM ina ilani na kama mradi huo haupo kwenye ilani ana sababu zote za kuhoji.
 
Kwani kuhamia Dom ipo kwenye ilani, Nape anazidi wehuka.
Hii la hiyo stigler ilikuwa planned since Nyerere era, likewise kuhamia Dom.
Bora lakini kaonyesha his real colors
bora walivyomvua uwaziri tumemjua.
 
Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.
Huyu dogo apunguze unafki na hasira za kupigwa chini uwaziri. Kimsingi tangu atenguliwe uwaziri haishi visirani vya kipuuzi.

JPM alishasema, linapokuja suala la maendeleo, Serikali yake haitojali suala la Chama, kama mradi wa Stigler's George umeonekana ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa Nchi, uachwe kufanyiwa kazi eti kwa kuwa tu haupo kwenye ilani ya CCM?

Huyu dogo kama bado ana visirani na haridhishwi na mwenendo wa CCM na Serikali yake si atoke tu!

Mipango ya maendeleo itaendelea kutekelezwa na hakuna kitu cha muhimu kitakachoachwa kufanyiwa kazi eti tu hakipo kwenye ilani ya CCM, mimi si CCM lakini nilimpigia kura JPM kwa sababu niliamini uwezo wake na 'energy' aliyokuwa nayo katika kusimamia mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom