Nape na Makamba mjue kujaribu kumshusha thamani Hayati Magufuli, ni sawa na kumfuata mamba kwenye kina kirefu cha maji

Nape na Makamba mjue kujaribu kumshusha thamani Hayati Magufuli, ni sawa na kumfuata mamba kwenye kina kirefu cha maji

Kinachopikwa ndani ya chama tawala kwa sasa ni chakura cha kuliangamiza taifa

Ikiwa kama team ccm inategemea uwezo wa mchezaji mmoja mmoja

bila ya unafiki wala kupepesa macho magufuli alikuwa ni kiungo mhimu sana ndani ya chama wakati wa enzi yake

Hii iko wazi hata kwa wanaopinga na bahati ya watanzania ipo sehemu moja tu

Mwamba aliacha miradi isiyokwepeka faida ni pale tu

Hata wanaompinga watanufaika na hiyo miradi
 
Eee hicho Cha kwako ndo cha Kwanza kukiona.
Hata kiswahili hujui, anyway japo ni ujinga lakini ni fungu ulilojichagulia mwenyewe. Amini nakwambia hakuna nchi yoyote isiyokuwa na watu kama wewe.
 
Sidhani kama Nape alifikiria hizi hoja zako..
Nape pamoja na January, kama wanataka kuwa credible politicians for a very long time, waache kushughulika na personal or petty issues. Wahangaike na mambo ambayo yatawabeba wao mbele ya wananchi.
JK aliwahi kushindwa na Mkapa 1995. Hata siku moja hakujaribu kudharau yote yaliyofanyika. Alijua ingekuwa suicide mission.
Unaanzaje kudharau project kubwa kama ya bwawa la umeme halafu ukafikiri utaeleweka?
 
Hata kiswahili hujui, anyway japo ni ujinga lakini ni fungu ulilojhagulia mwenyewe. Amini nakwambia hakuna nchi yoyote isiyokuwa na watu kama wewe.
Narudia tena huenda ukanielewa kichwa Cha Kwanza Cha maji kukiona ni Cha kwako!
Hapo vipi?
 
Jizi la kura lina legacy gani? Tunashukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi dhalimu bila damu kumwagika.
Haitabadilisha fact kwamba kufuta legacy ya jiwe ni kupoteza muda, watoto wadogo walikuwa wanasalute jeneza lake, mnapaswa mfahamu jamaa ameacha wafuasi mob.
Mtapambana na maiti yake mpaka mtakapomfuata
 
Si watoto wa hao aliowapa madaraka kwa shuruti ndio walikuwa wanapiga saluti. Isitoshe kupigiwa saluti ndio nini?
 
Si watoto wa hao aliowapa madaraka kwa shuruti ndio walikuwa wanapiga saluti. Isitoshe kupigiwa saluti ndio nini?
Endeleeni kujidanganya, eti watoto wa hao walio pewa vyeo, as if hakuna raia wa kawaida ambao hawakupewa cheo ila wanamkubali, nakwambiaje mkuu, unapoteza muda kupambana na marehemu, wapo watu kibao tulimkubali na tunataka kiongozi mwingine kama yeye.
 
Fedha zote alizokopa Magufuli zinaonekana kupitia kazi kubwa aliyoifanya. Fedha walizokopa na kupewa msaada awamu ya nne mpaka leo hazijulikani zimeenda wapi (Ukiacha zile za wizara ya ujenzi)!
The devil is in the detail. Ukiondoa awamu ya Nyerere, matumizi makubwa ya serikali tokea awamu ya pili yamegubikwa na giza la ufisadi bila maelezo ya kuridhisha hadi leo hii.

Uamuzi wa Magufuli kubana uhuru wa media, shughuli za upinzani na hatimaye kudhibiti ukaguzi (audit) wa miradi ya kimkakati ndio uliashiria kabisa nia yake kutotaka matumizi makubwa ya serikali yafahamike kwa wadau. Ukiondoa uwazi (transparency) kwenye shughuli muhimu za umma unakaribisha maswali na hoja nzito kuhusu unachofanya na lengo lako hasa la kutaka details za matumizi zifichwe.

Kazi nzuri za serikali haziwezib kuonekana wala kupimwa kwa macho pekee. Km, unawaonyesha wanakijiji gari zuri la wagonjwa ulilowanunulia lakini hutaki wajue kuwa umetumia shilingi 1.0 bilioni toka kodi zao katika ununuzi huo. Akitokea wa kuhoji unamfokea kwa nini halioni gari na ubora wake? Au ametumwa?

Miradi iliyoanzishwa na kufanyika chini ya Magufuli imeacha maswali kibao. Ingekaguliwa na “details” zote kuwekwa wazi si ajabu hata watu kama mimi tungebatizwa upya na kuwa waumini wa legacy yake. Sasa hivi naamini nchi ilipigwa na inaendelea kupigwa kichizi kupitia miradi hiyo. Km sikutegemea serikali inaweza kirahisi kabisa kununua ndege za kibiashara kwa fujo tena kwa “cash money”. Makomredi wenzangu katika field hapa Afrika wanashangaa sana kinachoendelea Tz.
 
Hii awamu ya sita wajitenge tu na Mwendazake,tuone ubavu wao.
Ndo watajua hii nchi inaishi kwenye kivuri Cha Mwendazake.

Mwendazake alisema chanjo hazifai na huyupo,wamejaribu kuwaaminisha watu ziko salama wameangukia pua.
Uvaaji barakoa vilevile wameula wa chuya.

Nape na January ni wepesi Kama karatasi,hasa kwa uombwe la kukatika umeme,mpaka atajua nyau siyo mboga.
Shukuru tu kuwa watu wa pwani ni vigumu kwao kuacha ustaarabu ndio maana bado Mama anamuenzi JPM. Angeweza kumponda mwendazake hadharani na kufanya yake.

Hakuna Mtanzania mwenye ubavu wa kuleta fyokofyoko mbele ya Rais wa JMT. Labda vichokochoko. Kama ni kura ni kiasi cha kujiamulia tu ajipe ngapi na wengine awapimie vipi. Ushindi kwake ni lazima.
 
Kumbe!!! Unawakumbuka Joyce Banda na Edgar Rungu?
 
Watu wanaingiza hasira za kutemwa kwenye teuzi au kuvuliwa uongozi kwa mgongo wa kujifanya wazalendo
 
Endeleeni kujidanganya, eti watoto wa hao walio pewa vyeo, as if hakuna raia wa kawaida ambao hawakupewa cheo ila wanamkubali, nakwambiaje mkuu, unapoteza muda kupambana na marehemu, wapo watu kibao tulimkubali na tunataka kiongozi mwingine kama yeye.

Ni kweli, si unajua akija kiongozi mwingine kama yeye lile kundi lenu la watu wasiojulikana litarudi.
 
Endeleeni kujidanganya, eti watoto wa hao walio pewa vyeo, as if hakuna raia wa kawaida ambao hawakupewa cheo ila wanamkubali, nakwambiaje mkuu, unapoteza muda kupambana na marehemu, wapo watu kibao tulimkubali na tunataka kiongozi mwingine kama yeye.
Kiongozi kama yeye wa kukopa dola bilion 9?huku akijitapa HAJAWAH KUKOPA?HAKIKA HATUTAMPATA KIONGOZ KAMA HUYO[emoji3][emoji3]
 
Kama mnampenda sana huyo dikteta si mfanye maombi mfululizo mpaka afufuke? He is gone for good. No matter how mtakavyojihangaisha, hatorudi. MTAPATA TABU SANA [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yupo Gwajima ni miongoni mwao, na yeye amekuwa akijinadi kuwa ana uwezo wa kufufua wafu, sasa si wampelele pale Chato akafanye kazi ya ufufuo ili "shujaa" wao arejee?
 
Kila mtu atakwenda for good
Ukilijua hili huwezi kuua raia wema bila sababu kama alivyofanya JPM, hakika alikuwa na roho mbaya na isiyo ya kibinadamu kabisa, tazama Mungu alivyo wa ajabu, apamoja na mavifaru lukuki, mibunduki kila kona na kuagiza akina LISSU kunyeshewa mvua ya risasi, Been saa nane na Azory Gwanda walipotezwa kabisa bila hata ndugu zao kujua walipo, lakini Mungu kwa miujiza yake na yeye analiwa na funza huko Chato!

Tuishini kibinadamu na kuacha kiburi na majivuno ya madaraka, wote tutakufa tu!
 
Kama mnampenda sana huyo dikteta si mfanye maombi mfululizo mpaka afufuke? He is gone for good. No matter how mtakavyojihangaisha, hatorudi. MTAPATA TABU SANA 🤣🤣🤣
Kwani unadhani jamaa yako mr #dishlimetilt anayeshikishwa ukuta na wazungu kule mamtoni yeye ataishi milele?
 
Back
Top Bottom