KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni wenyewe wanaoumiliki ndio wameufunga, wanafunga kwa baadhi ya nchi, hasa za kiafrika, wameona hauna faida, na mwaka Jana wamepata hasara sana, nasikia Wana mpango wa kuuza, lakini hawajapata mteja...
Acha ujinga kwani wanaingia free si ma bando yao?
 
Sasa kama hadi uwashe vpn ndio unapata sasa nape kafungia kitu gani? Ingekua ni mimi ningefungia popote watu kama Lissu fatma karume na maria sarungi wanapata fursa kusema uongo na kupotosha hali halisi ya siasa na haki za binadami Tanzania.
Hao wanaosema uwongo wanawapigania watoto wako tatizo ww siasa za maccm zinakunufaisha
 
Huyu jamaa inshu za kufungia fungia anazipenda sana

Ananishitua pale anaposema kuwa anataka azikaze kabisa tusizipate tena porno websites kirahis
 
Sina uhakika kama ni kweli lakini nimeona kule twitter alivyojibu message ya Elon Musk kuhusu Starlink nikajua kichwani hana kitu zaidi ya hewa
 
Nape alituambia kwamba Mungu aliamua ugomvi, kwa maana Magifuli kuna watu alikuwa na ugomvi nao ila Mungu akaingilia na kuondoa uhai wa Magufulu na hivyo hao maadui zale wakawa washindi...
....naongeza....Nape, Tundu Lissu, Mbowe na Waliominywa mirija wako sambamba katika kueneza uwongo na upotoshaji uliojaa chuki binafsi.

Nape kama kiranja wa habari Nchini ameachia Wananchi, pamoja na Familia ya Magufuli kufanyiwa Ugaidi pasipo hata n kuwa washiriki wa aina yeyote na hayo wanayodai walifanyiwa na Hayat Rais.

Ugaidi huu ni hatari kwa afya ya jamii kwa ujumla. lakini pamoja na Nape kujua hayo, ameachia vyombo vinavyoeneza habari hizo za unyanyasaji, ukimbari na yote yanayofanana nayo ilimradi tu wapate kulipiza kisasi.... waendelee bila ya Serikali kutoa tamko, kwa nini? Je ni kwa sababu tu Hayat Rais hakumwachia avimbe kwa bao lake la mkono, au kwa sababu hakuachia nadharia inayojengeka/iliyojengwa kuhusu nani haswa aliyehusika katika lile tukio? pamoja na CHADEMA kutengeneza mazingira za kuichafua Serikali?

Hakika sijui ni nini haswa kilichopeleka mtandao huo kutopatikana, na hivyo basi, siwezi dai hata kwa sumni kama mada inasimama.

Ila naweza sema kuwa, kama mada inasimama na taarifa zake basi hiyo itatosha mimi kusema ...anajali zaidi Nguvu za dola,(power) anajali zaidi tumbo lake(maslahi binafsi) pamoja na kukumbatia uhasama hasi ulioelekezwa kwa Wananchi na Familia ya Hayat Rais hususan mjane wake na watoro wake....kwa visasi vyake....na vile vya watajwa juu na vilevile kwa sababu anajua kudondoka kwa CCM ndio utakuwa mwisho wa Legacy ya NNauye.

Nape atuwekee filter ya maudhui ya upotoshaji(mis-information) maudhui ya ukimbari na unyanyasaji(dis-information) aweze kuokoa Vijana wa Kesho.

Kama kiranja Mkuu wa Habari atujuze hapa, kwani upo uwezekano ana vibaraka wake humu jamvini. Watujuzee! Kulikoni Club House?
 
Unaongelea wananchi gani?

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Msilalamike kwani nyie wenyewe mnapenda mtawaliwe na familia zilezile za babu, bibi, mtoto na mjukuu, analinda himaya yao.
 
Nani anapenda?
Hujui kuwa wana vijana wao wabeba mitutu wanawalinda pindi wakipora chaguzi?
Wanawalinda dhidi ya nani? Mwaka juzi tundulissu alipoporwa kura 87%/13% akakuamrisheni mhamie barabarani yeye akahania Ulaya mbona hukuenda barabarani, mbona hatukuona mitutu? Nenda Kenya wanaume hawaogopi mitutu.

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Si tuliambiwa awamu hii tunafungulia kila kitu. "Mmefungia fungia kila kitu bila sababu" leo imekuwaje tena? Au ndo tulitaka tu kufuta ya magufuli?
 
Wangeingia barabarani wangeuawa wote. Wao wana vifaru, bunduki na risasi wakati wananchi wana mawe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…