Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ambaye ameshika nafasi mbalimbali ndani ya CCM na serikali kuanzia ukuu wa wilaya,Mwenezi wa CCM Taifa pamoja na UWaziri .
Ameibuka kibabe na kutoa uchambuzi wake mfupi na tathmini yake fupi juu ya nani anakwenda kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Ambapo amesema uchaguzi ni namba na kwa namba za sasa Amemtaja mshindi wa kiti hicho hata Kabla ya kufanyika uchaguzi. Ikumbukwe ya kuwa huyu Mwamba ni Miongoni kwa Waenezi wa CCM machachari kwelikweli kuwahi kushika nafasi hiyo na ambaye alijua kucheza na akili za upinzani na kugusa hisia za watu mpaka kuwabubujisha machozi ya furaha.
Huyu Mwamba alikuwa Mtata kwelikweli kwenye vimisemo vya hapa na pale ambavyo vimeendelea kubakia kama kumbukumbu katika uga wa siasa. Mfano wa kauli zake zilizotikisa ni kama ile ya Bao la Mkono. Huyu Mwamba alikuwa akishika Maiki inakuwa balaa kwelikweli.
Lakini pia huyu Mwamba wakati wake alijua namna ya kucheza na mitandao katika kukisemea chama na kukitetea ni wakati wake ambapo vijana wengi sana walijaa hapa jukwaani kukitetea chama na kukipigania usiku na mchana na ni wakati wake hadi kuliibuka jina la utani kwa wafuasi wa CCM humu jukwaani kwa kuitwa LUMUMBA BUKU 7😀😀.
Watu wakifikiria kuwa pengine vijana walikuwa wakilipwa kwa namna walivyokuwa wakichapa kazi bila kuchoka wala kupumzika mpaka upinzani hasa CHADEMA ukawa unafikia hatua ya kukata pumzi na kuanza kuporomosha matusi kama vichaa au wendawazimu.,
Watu wanashindwa kuelewa kuwa sisi wana CCM huwa tunafanya kazi za chama kizalendo kwa kujitolea kwa hali na mali bila kupewa malipo wala kuhitaji malipo. Maana vitu vizuri hujengwa na mioyo yenye kujitolea.ndio maana wengine hufikia hatua ya kufikiri labda hata mimi nalipwa kuwepo hapa jukwaani bila kujua ni misingi tuliyojengewa ndani ya CCM kukipigania chama chetu kwa jasho na kwa kujitolea bure kabisa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.