I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama? Wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara? Mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"
~Nape Nnauye
----
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.
Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:
“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.
“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.
“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.
“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.
“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?
“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”
Chanzo: Maelezo