Nape Nnauye: Anaachwaje kichaa mmoja hivi anasema ‘Mama hatukuelewi’?

Nape Nnauye: Anaachwaje kichaa mmoja hivi anasema ‘Mama hatukuelewi’?

Elimu yake ya kuunga unga mara Mzumbe University mara India!! Amshukuru sana Mzee Mangulla alimuokoa kwa kumpeleka India kusoma mara baada ya Vasco Dagama kuukwaa Urais ; kwani wakati ule mkwere alikuwa na beef nae kinoma!!! Angemmaliza!
 
Hatumuelewi mama kwa yafuatayo;
1. Mfumuko wa bei umekuwa juu kuliko wakati mwingine wowote hivyo kuathiri maisha ya mtu mmoja mmoja kwa asilimia 100.
  • Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.
  • Vyakula vimepanda bei...
2. Amekuwa mtu wa too tu;
  • Tozo za miamala zunaumiza sana raia, anayetuma pesa anakatwa kodi+tozo, anatetoa pesa the same.
  • Tozo ya tsh100 plus ongezeko kubwa la bei ya mafuta vinamuumiza mwananchi kwa kiasi kikubwa mno. Hakuna subsidies kutoka serikalini kumsaidia mwananchi?
3. Kuna upigaji na uzembe, business as usual. Mianya ya kuchapa rasilimali za nchi imerudi, matokeo ywke tutayajua in the near future.
4. Nchi imerudi kwa wachache, the elites..the chosen ones huku mamilioni wakihisi wametengwa na serikali yao.
5. Anasisitiza-na bado, bei za vitu zinazidi kupaa, maisha yatazidi kuwa jiwe.

She simply doesn't have a road map in her leadership, yupo tu..nchi inaenda tu.

Simuelewi...
 
Nape ni akili ndogo sana ...
Makamba angalau anatunyamazisha wakosoaji wake.

January na Chande mnafanya poa sana TANESCO.
 
Tusimpe Rais wetu majina yasiyostahili. Tumpe heshima yake ni kiongozi wetu wa nchi kwa wakati wake. Pia waziri Nape sio lazima kumweka mkuu wa nchi ukutani ili hatimaye tuseme lolote jema au baya. Jaribuni kujibu hoja kwa hoja. Pale ambapo wanadhani hawaelewi ni haki yao kusema. Ni kazi yako kuwaelewesha wasichoelewa na pia ndio kazi za Msigwa kuwaelewesha pale ambapo panahitaji hilo. Usionekane kama vile unawatishia watu wasihoji mambo. Angalia usijepoteza sifa yako tena kama kiongozi wa wizara.
 
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama?,
wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara?,mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"

~Nape Nnauye

----
View attachment 2218275

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.

Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:

“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.

“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.

“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.

“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.

“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?

“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”

Chanzo: Maelezo
Nape nakuheshimu ila umeenda "utra- vires" kusema kwamba yule bwana ni kichaa!
Kwanza ibara 18 ya katiba ya JMT inampa Uhuru wa kutoa mawazo yake!
Pili wewe si daktari wa kuthibitisha kama yule bwana ni kichaa au la!
Viongozi chungeni sana ndimi zenu lakini pia vitu basic katika Sheria muwe mnavipitia pitia ili kutoa quality leadership.
 
Chadema hawamuelewi Mama, wakati Mbowe kaachiwa huru 100%, hivi mna matatizo gani nyie Chadema? Mnataka nini nyie? 🤔😳😡
 
Huyu chawa anaacha kupambana Na Bei ya vifurushi kupanda analeta uchawa kwa mama afunike mjadala wa wizara yake kufumbia macho kampuni za simu kupandisha bei kiholela
 
Kwa kumuita mwananchi "Kichaa Mmoja" tayari amevunja maadili ya uwaziri. Anajiona kama mwenezi hivi akiwajibu Chadema 2013.
Anatakiwa ajiuzulu kama hawezi kujibu kama waziri.
Mawaziri wote wakitumia lugha aliotumia , hii nchi itakuwaje?
 
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama?,
wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara?,mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"

~Nape Nnauye

----
View attachment 2218275

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.

Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:

“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.

“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.

“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.

“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.

“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?

“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”

Chanzo: Maelezo
Ww bana tetea ugali wako usilazimishe watu kuelewa hivi nikuulize mwananchi wa kawaida haya ulioyaeleza lipi hata moja linamuhusu?? Umezungumzia wauza magenge wanavyotimuliwa kila mahali?? Bidhaa za muhimu kupanda bei?? Au tutupie hapa picha yako ulipokua unaenda kwa mwenda zake kuomba samahani huku jasho linakuvuja?? Hii nchi yote sote bado tunamuelewa waziri mkuu alisema tuwe watulivu ndio maana tumetulia usitutibue naona unajisahau kama vile nchi ya kwako peke ako
 
Huyu naye ameshaanza kuvimbiwa asali ya Bibie.
Huwezi kulazimisha watu kumpenda Bibie. Wewe unampenda kwa sababu alikuokota kutoka shimoni hadi hapo ulipo.
Isitoshe wewe unakula vya mama, lakini watu mtaani ni hali mbaya kweli kweli kuliko wakati mwingine wowote ule.
JPM hakuongeza mishahara lakini alidhibiti mfumuko wa bei.
Bei za JPM sasa zimepanda kwa zaidi ya 110%.
Kumbuka, watumishi wanaoongezewa mishahara ni takribani laki tano, je, hawa milioni 60 watafaidi nini?
 
Back
Top Bottom