Nape Nnauye: Anaachwaje kichaa mmoja hivi anasema ‘Mama hatukuelewi’?

Nape Nnauye: Anaachwaje kichaa mmoja hivi anasema ‘Mama hatukuelewi’?

Halmashauri ya wilaya, mji mdogo, mji au manispaa na jiji hazina akaunti youtube, facebook pages au instagram pages hao maofisa habari updates za kazi za serikali wanawapaje wananchi wao au wapowapo tu
Kwa akili yako habari mpaka ziwe huko ulipopataja ndio waandishi wazipate? Hao watakuwa waandishi au copycats?

Mwandishi anatakiwa azitafute habari kwa kukutana na "reliable sources".
 
"Kama hawamwelewi si uwaeleweshe tu, sasa makasiriko yanini..."

Alisikika mlevi mmoja akibwata
Si waseme ni nini wasichokielewa. Tuwaeleweshe.

Sijamuona kuwa kakasirika naona kuwa anawashangaa.
 
mimi mojawapo simuelewi mama yako. pili vyombo vya habari havikufungwa na jpm ulivifunga wewe kwa kujipendekeza kwa jpm na kumpa ushauri kuwa mzifunge leo unamlaumu na nyinyi ndio mlijifanya kumpa maelezo na ushauri mzuri kumbe unamponza alikuwamini sababu ulikuwa ccm nafasi kubwa kumbe kichwani huna kitu nape nnauye
 
Hatumuelewi mama kwa yafuatayo;
1. Mfumuko wa bei umekuwa juu kuliko wakati mwingine wowote hivyo kuathiri maisha ya mtu mmoja mmoja kwa asilimia 100.
  • Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.
  • Vyakula vimepanda bei...
2. Amekuwa mtu wa too tu;
  • Tozo za miamala zunaumiza sana raia, anayetuma pesa anakatwa kodi+tozo, anatetoa pesa the same.
  • Tozo ya tsh100 plus ongezeko kubwa la bei ya mafuta vinamuumiza mwananchi kwa kiasi kikubwa mno. Hakuna subsidies kutoka serikalini kumsaidia mwananchi?
3. Kuna upigaji na uzembe, business as usual. Mianya ya kuchapa rasilimali za nchi imerudi, matokeo ywke tutayajua in the near future.
4. Nchi imerudi kwa wachache, the elites..the chosen ones huku mamilioni wakihisi wametengwa na serikali yao.
5. Anasisitiza-na bado, bei za vitu zinazidi kupaa, maisha yatazidi kuwa jiwe.

She simply doesn't have a road map in her leadership, yupo tu..nchi inaenda tu.

Simuelewi...

rostam azizi kula nchi kwa kishindo
 
Jamaa amemjibu Nape. Kwa hiyo ni Kichaa Mmoja 2: Nape 1.
Je, Nape ataweza comeback?
 
Kuna mtu ameanza kulewa kimpumu
Endelea kuramba vya kuramba mtoto wa muasisi oopos sorry ni wa muimba solo
 
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama?,
wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara?,mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"

~Nape Nnauye

----
View attachment 2218275

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.

Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:

“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.

“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.

“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.

“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.

“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?

“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”

Chanzo: Maelezo
Mama tuna mwelewa vizuri. Wasiomwelewa ni roho zao tu
 
kwa vile maslahi yake yanapatikana anataka kila mtu amwelewe? mimi mwenyewe simuelewi hata kidogo
 
Anaachwaje Mh mmoja ambaye kamba yake ni urefu wa kurushia tiara na end product ya huu urushaji tiara mahali pengine ni LOAD FEED FORCE /LFF?
 
Back
Top Bottom