Nape Nnauye: Anaachwaje kichaa mmoja hivi anasema ‘Mama hatukuelewi’?

Feedback is the food for the champions. Power corrupts.
 
Huyo mama yenu haeleweki, anaharibu kwenye mipasho yake hasa,
Mara kuleni kwa urefu wa kamba zenu, Mara nikune nikukune, Mara nidhamu ya awamu ya tano kazini ilikua ni ya uoga Ila kwake yeye nidhamu hakuna kabisa.

Kingine no teuzi zake, kipara, Hiyo nnawie,mwigulu na wengine wengi wa awamu ya nne.

TISS tuokoeni na balaa
 
Wanaolalamika wengi "A bunch of useless misukule, toxic people na wafuasi wa wanasiasa na wanaharakati"

Hakuna mtu mwenye akili timamu analalamika sana
Wewe wa kupimwa akili.... haya ona hizi
1. Unaijua bei ya mbole ahadi sasa?
2. Mafuta ya kupikia bei yake unaijua?
3. Sukari unaijua bei yake?
4. Vifaa vya ujenzi, bati la geji 30 unaijua bei yake kwa sasa?
5. Pembejeo za kilimo unajua bei zake kwa sasa?
6. Mafuta ya magari na mashine mbalimbali ndo hayooo...!!!
7. Nauli si umeona? Na kwingine hadi migomo ilitokea
 
Nape naona umenza kujisahau!
Hivi watu kuelezea hisia zao ni dhambi?
Unajua kweli yanayoendelea mtaani au umeshashiba ?
Mambo ya ajabu sana haya, halafu tunatarajia watu kama hawa wamsaidie mama kututoa hapa tulipo! sidhani!
 
Kwani lazima kila raia amwelewe?
Tena Nape mwenye kasema wale waliokuwa na vyeti fake, nusu wamerudishwa kazini, sasa anategemea hao nusu waliobaki kitaa WANAMUELEWA MAMA?

ALitakiwa aufanyie kazi ushayri, si kuitana vichaa wakati mtu kaongea vya msingi.. Yaani kwa vile kasema usichokipenda ndo ukichaa? Kwani yeye ni daktari hadi aseme jamaa ni kichaa?
 
Nape naona umenza kujisahau!
Hivi watu kuelezea hisia zao ni dhambi?
Unajua kweli yanayoendelea mtaani au umeshashiba ?
Mambo ya ajabu sana haya, halafu tunatarajia watu kama hawa wamsaidie mama kututoa hapa tulipo! sidhani!
Watu kama akina Nape ndo wanomwambia mama kuwa mabo yapo safii.. Kumbe huku kitaa tunateseka haswaa..!! Niliupenda ushauri wa jamaa aliyeitwa kichaa kuwa.. MAMA ASIWAPE WATU MASIKIO, AENDE MWENYEWE DUKANI AKAJIONEE HALI HALISI
 
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama?,
wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara?,mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"

~Nape Nnauye

----
View attachment 2218275

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.

Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:

“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.

“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.

“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.

“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.

“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?

“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”

Chanzo: Maelezo
kwani kunakosa gani mtu kueleza hisia zake.
 
Hata hao anaongea nao inaonekana hawamuelewi wengi wana huzuni, sijui shida iko wapi nchi hii
 
Mbona kaongea vizuri tu kuwa kwa sasa mtajibiwa kwa facts, ila wana harakati wamezidi
 
Huyu jamaa hua anahisi hii nchi ni mali ya familia yao amejaa majivuno na kibri ya madaraka!
 
Wanaolalamika wengi "A bunch of useless misukule, toxic people na wafuasi wa wanasiasa na wanaharakati"

Hakuna mtu mwenye akili timamu analalamika sana
Duh bado haujapona depression, usichukulie poa tafuta tiba stress za maisha zitakuua
 
Siyo kichaa mmoja.....wasioelewa ni wengi na siyo mmoja acheni mapovu. Fanyeni kazi ambayo watu wataielewa siyo kulazimisha waelewe
 
"Tulifungia vyombo vya habari, tumevifungulia bila masharti, je hawamuelewi mama?,
wafanyakazi wa Umma walikaa miaka mingapi bila kupandishiwa mshahara?,mama juzi kasema jambo lenu lipo, halafu anakuja mtu anasema mtaani watu hawamwelewi mama?"

~Nape Nnauye

----
View attachment 2218275

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumza kuhusu kauli ya ‘mama hatukuelewi’ ambayo anadai kuna watu wamekuwa wakiitumia wakimaanisha hawamuelewi Rais Samia Suluhu.

Huyu hapa Nape akizungumza katika Ufunguzi wa Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mei 9, 2022 Jijini Tanga katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera:

“Mtu mmoja nimeona amerekodi video anasema ‘Mama huku mtaani watu hawakuelewi’, inawezekana wapo kweli ambao hawamuelewi, lakini nikajiuliza wale waliofukuzwa kwa vyeti feki wamerudishwa kazini.

“Watoto waliofukuzwa kwa ujauzito na walioacha shule kwa sababu mbalimbali wameruhusiwa kurudi shule.

“Kuna watu wamefunguliwa akaunti za biashara zilifungwa kwa sababu mbalimbali, bado unasema watu hawamuelewi, lakini kwa sababu hajibiwi inaonekana ni kama kweli watu hawamuelewi.

“Nilikuwa Karatu wakati nakagua mradi wa Anwani za makazi, wakaniambia kuna wakati ulikuwa ukitoka Karatu kwenda Arusha hukutani na magari ya watalii, lakini sasa hivi yanapishana tu magari ya utalii.

“Tumefungua vyombo vya habari bila masharti, wafanyakazi wa Serikalini walikaa miaka mingapi bia kupandishiwa mshahara, mama ameshasema jambo lenu lipo, hao nao hawamuelewi mama?

“Anaachwaje mtu kichaa mmoja hivi anasema ‘unajua huku hawakuelewi’, nawapa changamoto maofisa habari, unapokuwa afisa habari wewe ni katibu Mwenezi wa Serikali, wajibu wako ni kuwafanya wananchi waielewe Serikali.”

Chanzo: Maelezo
Mimi namuelewa mama lakini siwezi kusimama mbele ya Umma kuwabeza wanaosema hawamuelewi.

Ninanchokifanya ni kuwaelewesha kwa nafasi na level yangu
 
Back
Top Bottom