Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Mambo yanayoendelea Ni vigumu kuahamini kwamba Tanzania ni Nchi huru
 
Dah!

Mimi si mpenzi wa CCM na si shabiki wa Nape ila hicho nilichokiona kwenye hiyo video sijakifurahia.

Kwangu haki ni haki tu.

Ni nini hasa kilipelekea yote hayo?

Kuna anayejua humu anieleweshe zaidi?
Ni kweli ulichokisema.

Lakini mwanausalama alikuwa 'calm' tena aliongea kwa upole 'Mheshimiwa rudi kwenye gari..', Wakati huo Mh. Nape akiwa amevaa shati bila kuchomekea na ameweka mikono yote mifukoni (kulia na kushoto); baadaye anasikika (Nape) akimwambia mwana usalama " ....usinishike hivyo Bwana, ondoka" wakati huo anamsukuma mwanausalama kwa mkono wa kushoto lakini mkono wake wa kulia ukiwa bado humo mfukoni; kwa akili za kawaida...askari lazima ajihami maana huo mkono wakulia wa Nape ambao umo mfukoni hajui umeshika nini. Na hata Nape alivyosukumwa sukumwa hakutoa mkono huo wa kulia mpaka (labda) alipohakikisha kuwa sasa mfuko wa kulia wa suruali lake umezibwa na gari ndipo alipotoa mkono mfukoni. Na watu wakaongezeka pale...!

Naliona hivyo tukio hili. Lakini maelezo mazuri anaweza kuyatoa mwanausalama mwenyewe kwa nini alifanya vile.
 
Soma post # 423 ya uzi huu.
 
Hili genge lote ni waandishi wa habari? au na vibaka walikuwemo? kweli ipo haja ya kuifanyia mabadiliko taaluma ya uandishi wa habari imekuwa ya kihuni mno.
 

Kwa kweli sidhani kama macho na masikio yangu yamenidanganya hapo.

Nape hakuwa belligerent hata kidogo.

Na huyo jamaa, whatever he is, hakuwa kabisa na sababu kutoa silaha yake na kumtishia Nape.

Halafu, hivi kosa la Nape hapo lilikuwa ni lipi hasa?

Kuongea na watu/ waandishi wa habari imekuwa kosa siku hizi?

Utadhani tupo North Korea!
 
Habar za usiku wazee.
Tukiunganisha matukio yanayoendelea kutokea nchini kwetu na ukiyatafakari kwa kina unashindwa kupata majibu yakukufanya uone mambo yapo sawa.
Sijui kuna nini
Ila lazima kutakua na kitu ambacho tunatakiwa kujua jama raia.
Tuvute subra tuone kesho Mh.Rais atazungumza nini kuweka sawa hii hali iliyopo
 
ameitia aibu tasinia husika

hasira za nini bila kutumia akili? anataka kuua mbele ya kamera? it was suppose to be professional

duh kumbe wahuni vile..........

ninaimani hawajatoka nyumba nyeupe wale jamaa (Nyumba nyeupe takatifu)

mungu mbaliki raisi wetu
 

Attachments

Wapuuzi fulani wale waliomtetea bashite kwenda kwenye kituo fulani na armed gang watakuambia hakutolewa bastola [emoji849][emoji849][emoji849]
 
Ha ha ha
ni muendelezo wa kauli za kibabe tu.
Kingine ni kusisitiza makondo piga kazi
 
nimefurahi sana maake harmorapa haya ndiyo magape yake
 

Onyo na hatua kali za kinidhamu na za kisheria zichukuliwe dhidi ya askari aliyemtishia Nape kwa bastola.
Onyo la nini?.....unadhani huwa wanabeba kama mapambo...kwa taarifa yako hakuna silaha inayotengenezwa kwa ajili ya mnyama huwa ni kwa ajili ya binadamu!
 

Kwa akili ya kawaida waziri aliyesimamishwa kazi masaa 24 yaliyopita ameitisha press atoe bastola ampige mtu/mwana usalama?never Nape hawezi kufanya hivyo,kiongozi wa serikali akishampiga risasi na yeye maarufu unadhani ujinga huo anaweza kuufanya ,pale mwana usalama anajua kabisa hawezi kudhuriwa hata na kiwembe na nape ,mwana usalama alipoona nape mbishi na yeye kapewa kazi nape asizungumze akaamua atumie nguvu na vitisho ili kiongozi huyo a-surrende

Nape alivyoshikwa alimuuliza kitambulisho kipo wapi ndipo yule mwana usalama akatoa bastola ,

Maneno ya usinishike toka bwana ni pale alipokuwa amesukumizwa hatua chache kwenda kwenye gari..mkuu umechakachua Maelezo ya tukio

Mwana usalama hakuwa threatened na nape na hata wenzake hawakuwa na wasiwasi wowote ule waliokuwa wakimshinikiza nape aingie kwenye gari
 
.....

Maneno ya usinishike toka bwana ni pale alipokuwa amesukumizwa hatua chache kwenda kwenye gari..mkuu umechakachua Maelezo ya tukio

....
Nimeitaza iyo clip mara ishirini na saba....ndiyo nikatoa maelezo hayo hapo juu. ebu angalia vizuri hiyo clip mwanzoni mwana usalama anaamfuata Nape mpaka hatua ya askari kuamua kujihami.
 
Hawa maaskari tumesoma nao vichwani hamna kitu eti ndo wanapewa silaha watulinde duuuh fafafafaa tu hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…