Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Hwkima nzuri,hwshima nzuri.Rais wangu mungu akutunze Sana.
 
Hongera sana kwa MH. Rais Magufuli, nampongeza sana yeye kwa huruma yake, angeweza mpuuzia lkn amemridhia na kumsamehe.
 
Ndogo ndogo za kitaa zinadai Bugiri ndiye aliyemualika Nape Ikulu.

 
Eti kuna watu ndani ya JF walishabikia misimamo ya watu hawa. Uzembe wao ukageuzwa kuwa ushujaa. wakawa ni kigezo cha ubora wa rais. Kwa ujumla kama kawaida yangu, nawakumbusha, kuweni makini na wanasiasa wetu ambao wengi ubora wao uko chini.

Baada ya kuwa na viwango duni vya wanasiasa kwa miaka zaidi ya 20, tunashindwa kuvumilia au kuelewa uwezo mkubwa wa rais. Hawa watu hawana pa kwenda nje ya siasa. Bado wale wapiga kelele wa upinzani ambao nao ni kama vijana wa foolish age.
 
Ndogo ndogo za kitaa zinadai Bugiri ndiye aliyemualika Nape Ikulu.
Boss, hebu rudia kusoma msg zako juu ya sifa ulizomwaga kwa Nape ukiamini ni shujaa. Hata kama kaitwa je, yuko kiwango cha chini kiasi cha kuambiwa maneno ya kubembeleza? Kama wasemavyo waingereza, ukitaka kujua wewe ni nani, angalia unaowaunga mkono walivyo.
 
Ukishasema sanduku la kura, Nape alibebwa! Nape siyo mbunge wa mikoa ya kusini, ni mbunge wa jimbo moja tu! Sifa za Nape unazozitoa ni zile za toilet paper.
 

makufuli hamuhitaji nape kabisa . kaa ukijua makufuli ana wananchi wengi wanaompenda wanaomchukia ni wale waliobanwa na pili hata kama tanzania nzima usimpigie kura lakini atashinda
 
mkuu mpaka leo unafatilia katiba ya Tz, huyo haondoki hapo ikulu labda akipenda au afe mwenyewe akipenda pia.

usijidanganye kuwa ataachia madaraka. kamwee
 
January alikua hajamwambia Nape kama yeye kashaomba msamaha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nape baada ya kusikia kumbe wenzie wameomba msamaha ikabidi na yeye ajiongeze. Kujifanya kichwa nazi halafu ukose ubunge 2020
 
Hahahha awamu hii tumepatikana...."yani amehangaika kweli ameenda kwa mzee Mangula, mama Maria...." huu ni msamaha au kuaibishana
 
Mie kumsifia Nape? 😳😳😳😳😳
Eti ni shujaa? Ushujaa kwenye lipi? Hebu weka ushahidi wa kuthibitisha kauli yako.

Alichokifanya nape baada ya Clouds kuvamiwa ni wajibu wake ili kufanya uchunguzi kabla ya kuchukua hatua.

Nasubiri ushahidi wa niliyoyaandika.

 
Kitendo cha mbunge wa jimbo la Mtama mh Nape Nnauye leo kwenda kuungama dhambi zake zote kwa Rais Magufuli kumeacha dilema na maswali yasiyojibika vichwani mwa wafuatiliaji wa siasa za chama tawala na za upinzani nchini.

Je, maungamo na kukiri toka moyoni alikokufanya leo Nape ni majuto kweli ya makosa na fedheha alizomfanyia Rais Magufuli au ni kujikosha tu baada ya kubaini wenzake kina Makamba na Ngeleja walienda kuomba msamaha na wakasamehewa?

Je, kambi ya upinzani iliyokuwa ikiwatetea Nape na wenzake, hivi sasa inasemaje baada ya kuona baba na mwana wamepatana?

Tujadili kwa pamoja.

 
Issue ya wana CCM waomba 'msamaha' 1 yr kabla ya uchaguzi inafikirisha sana.....

Mtu akifikiria kujiajiri anapoteza usingizi saa 8 usiku.. duh
 
Sisi wakristo ungamo letu linalazimisha kutaja dhambi zote unazozikumbuka na mwisho tunasema ".....kwa dhambi hizi na nyingine zote nisizozifahamu ..." Kisha Padre anakutangazia msamaha na kukutaka usitende dhambi tena.

Kwenye kutaja dhambi unaweza kulazimika kuwataja na wengine mlioshirikiana kutenda dhambi hizo na hapo ndio napata wasiwasi kwamba huenda kukawa na foleni endelevu ya watakaomba msamaha.

Chukulia mfano kama William alikuwa wa kwanza kukiri kosa na kuomba msamaha atashindwa kuwataja aliokuwa anaongea nao kweli?!

Mbarikiwe sana.
Maendeleo hayana vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…