Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Mwanasiasa haaminiki hasa katika ulimwengu huu wa tatu, tunataka siasa za hoja,sio majungu, siasa ya uwazi na ukosoaji wa uwazi na uhuru kwa kila anayekosoa kistaarabu. Msamaha wa kweli pale kunapotokea kutofautiana maana wote tunafikiri kwa ajili ya nchi Kwanza sisi baadae
 

Mzee Makamba alisema kweli huyu atakuwa anabatiza kwa moto tena mbele ya kamera
 
Sijaelewa kinachoendelea ndani ya jahazi ila tunaweza kusema ni taarifa kwa wale wanaodhani jahazi linaingia maji na linaweza kuzama ilihali maji yanaingia na kutolewa.

Kwa lugha yetu wakongwe huwa tunasema
(mtoto kashika adabu) maana mmoja mmoja anaenda nyumbani na kukiri.

Ila kwa muktadha huu wa kupigwa masnap kutokea juu tena popote unapotokea huku jasho likimwagika sijaelewa mantiki yake!!.








 
Utusamehe sisi wakosefu ndio picha inachojaribu kueleza hapo
 
Katika kinachoonekana ni kuipigia salute njaa baada ya kusota mitaani bila kazi ya kumfanya atembelee magari ya kifahari .

Nape ameanua kujisalimisha rasmi kwa yule anaye toa ridhiki yaani rais Magufuri na kuomba msamaha .Amakweli hakuna mwenye jeuri juu ya njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…