Kitendo cha Kaka Nape NNAUYE kuomba radhi kwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kimeonesha ukomavu wa Kisiasa wa Kaka Nnape na Ukomavu wa CCM. Kwakweli Nnape ni mwana ccm kindakindaki aliyepambania mabadiliko ndani ya Chama kwaajili ya maendeleo ya Taifa. Binafsi nilisikitishwa na uamuzi wa Nape kwenda kinyume na mwenyekiti wa Chama mwenye nia, hali na moyo wangu kukijenga Chama kwa maendeleo ya Taifa.
Nape, Mwigulu na Makamba ni watu muhimu sana kwa Chama na serikali kutokana na mioyo yao ya kizalendo, uchapakazi, ubunifu na maendeleo.
Tunapopambana kuifikia Dira ya maendeleo ya Taifa, 2025, hivi vichwa vitatu ni muhimu sana kwa Chama na serikali.
Naamini makosa waliyoyafanya, muda waliokaa benchi, wameelewa mtizamk, msimamo, nia na matarajio ya kocha mkuu katika kuliletea Taifa Maendeleo.
Uamuzi huu wa Leo alioufanya Nape mwana wa Nnauye ni pigo kwa vibaraka wa mabeberu na ushindi kwa Chama , serikali na Taifa.
Kijana hawa watatu, wanakifahamu Chama, serikali na nahitaji ya sasa ya Taifa.
Nawasihi msirudie makosa kwa kurubuniwa ili mlisaidie Taifa.
Hongera Nape, Hongera January, Hongera Mwigulu, Tuungane sasa kama Timu moja kwa maendeleo ya dhati.
Mheshimiwa Rais, nakuomba kwa dhati uwatumie zaidi hawa vijana ili kufanikisha malengo, mipango na mikakati yako , serikali na Taifa.
Nakupongeza Kocha na Mentor wangu JPM kwa kuwarejesha kundini washambuliaji wetu. Sasa ni total football kwa maendeleo ya Taifa.