Nape Nnauye: Kiroboto ulishindwa akiwepo godfather, utaweza leo?

Hii ndio hali halisi ndani ya CCM kwa sasa! Wapo vipandevipande vinavyohasimiana! Mwendazake alikimaliza chama kabisa bila kujua. Tutaona na kusikia mengi bado!
aliyekimaliza chama ni kikwete,enz zake chama kilinuka ufisadi na uchafu wa kila namna,Hadi ss wengine tulipata shida mtaani,yaani ukipita umevaa shati lolote la kijani aise raia wanatamani wakugawane onspot,watu walichukizwa na ufisadi wa serikali ya 4 kupindukia,akinamama zike kanga zao za kijani na njano waliogopa kuvaa kwa aibu ya ufisadi wa serikali ya awamu ya 4,chama kilioza na kuzaraulika kupindukia, kila mwana ccm enz hizo aliitwa ni fisadi hata Kama ni msafi,
 
Ila CCM hawajua kinachoendelea mtaani sio? Wafanye tafiti kuna chuki sana inajengeka...watakuja washangae akitokea mwanasiasa ana nguvu...watashangaa sana watu kama kina Nnape. Just someone to ignite
Hakuna lolote mkuu.

Watu tuliopo mtaani sasa hivi kwa amani kabisa Tunaangalia game ya Manchester United vs Norwich city.

Wewe unaongelea mtaa upi??
 
Huyu unayemwita mwendazake ndo aliirejesha ccm kwa wanachi wakaanza kuipenda .ili ccm ya kuvaa nguo yake ukaanza kuzomewa ilipotea .

Sent using Jamii Forums mobile app
😄😄 Kuipenda?Mnateka,mnaiba maboksi ya kura,mnanunua wapinzani,mnatumia tume na vyombo vyake kushinda kwa kishindo nchi nzima 😄😄 na mnasema mnapendwa Hamnaga aibu nyie.
 
Nimekupa "like" lakini hivi ni kweli hujui CCM ina wenyewe??

Haya maneno yamesemwa na Mkapa, Kikwete na Mheshimiwa Amani Abeid Amani Karume. Unataka ayaseme nani ili uamini CCM ina wenyewe???
 
Nape anajishushia anajishushia heshma zaidi na maneno na hizi tabia za kike.
Nape bado ni kijana sana na anamaisha mengi kwenye chama na siasa, nadhani anapaswa kuchunga kinywa chake.

Mbona Mkuu hujaniambia hiyo kauli inamanisha nini ??
 
Nakazia Sin

Mnaona raha kuukana wenzenu non sense, Huyu kweli ni muhuni huwezi tukana watu godfather, kama ulilelewa na wazazi.
 

Ni changamoto sana mkuu. Hapo tatizo linakuwa ni nini hasa ? Uchanga katika Siasa au ulimbukeni au Kukosa Busara ??
 
Umejibu kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ccm ya Polepole ni sukuma gang Na ya Nape ni Urojo Gang siyo? Haya tuone mwisho wa ccm hizi 2? Ila mimi am not happy with the way this Nape is behaving. Mama Ssmia please watch this guy he is very poisonous in this country if not well looked at and carefully handled we might end up splitting and or breaking up as a nation.

Please please handle him with care. We are not exceptional to other African countries.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…