Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye amewatoa wasiwasi wakazi wa Bukoba na wanachama wa CCM kuwa Mbunge wao Stephen Byabato atashinda uchaguzi ujao na hakuna mwingine.

"Matokeo ya kura siyo lazima yawe yale ya kwenye box, inategemea nani anahesabu na nani anatangaza. Unajua kuna mbinu nyingi za uchaguzi, Kuna halali, nusu halali na haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe" alisema Nape.

Aliyesema hayo katika Soko la Kashai jana Julai 15 usiku alipoalikwa na Mbunge Byabato kushuhudia ramani na michoro ya Soko jipya la Kashai linalotarajiwa kujengwa.
 
MKONO WA MUNGU utaendelea kutumika.
 
Ndiyo mbinu za CCM kura ni kiini macho
 
Mojawapo ya mawaziri bora kabisa katika serikali tukufu ya mama. Tuendeleeni kupambana na mabando ya Voda. Unanunua GB 10 na kabla hujafanya cho chote Voda wanapita nazo. Na hakuna kitu utafanya. Waziri mhusika ndo kwanza yupo anapigia debe bao la mkono! Beautiful Tanzania!

 
Temu hii haibiwi mutu kura atapigwa mbwa na MFUGA mbwa kwetu Wana SEMA tera embwa inwe amazi
 
Mungu anadhihakiwa mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…