Pre GE2025 Nape Nnauye: Nashangaa Watanzania wanaokwenda kusikiliza upuuzi wa Lissu. Tumkemee, tumtenge na tumlaani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu hawezi kulaaniwa na wananchi wenye akili. Wewe Nape ( Siandiki ubini wako unaoutumia kwani inajulikana marehemu Moses Mnauye sio baba yako)! Wewe ndio ulaaniwe kwa kukosa adabu na heshima kwa kuwatukana viongozi wa nchi kupitia handle yenu ya KIGOGO wewe na genge lako!
Hustahili hata Chembe kupewa nafasi ya uongozi katika serikali yeyote makini ya nchi hii.
 
Samahani mkuu hizo ajira alizotoa mama haziwahusu wa znz? Yaani wanaajiriwa wa bara pekee?
 
Nape Nauye ni Moja Kati ya Wanaume wadhaifu Tanzania. Ni mtu abayetega mwiba alafu unakuja kumchoma.
Mimi nikiwa mtoto wa Nape siwezi jivunia mbele za watu Eti Nape is my Dady
Nape ana siasa za kichawa tu
 
Mbona hujawahi kulaani mawaziri wanaotukana na kumlipa mange amtukane Raisi au ni venye Malaya wa kisiasa
 
Kauli ya makonda kuhusu wanaomlipa mange amtukane bi mkubwa bado inamtesa mwamba huyu
 
Nape, kuandamana ni haki ya kikatiba, siyo hisani. Wewe chawa huwezi kufikiri zaidi ya kutetea tumbo lako.

Kwanini bandari za zanzibar hakuziuza kwa waarabu? wazaznzibari hawataki mapesa ya waarabu. Una akili za uchawa
Hivi huyo Nape aliponaga magoti baada ya kuyatembelea kwenda kuomba poooh/msamaha kwa marehemu?Maana unaweza kukuta anaongea huku anakuna vidonda magotini na kukosa umakini wa kuchagua maneno ya kuongea.
 
Wadau ule useme wa "NYANI haoni KUNDULE" hatimae umetimia.Sikutarajia mtu kama NAPE Atamnyooshea kidole Mh Tundu Lissu.
NAPE ni mmoja wa Watu Waliowatukana Viongozi wetu bila kujali Umri wao na madaraka na Michango yao kwa Taifa.
NAPE alimtukana sana Hayati Magufuli mara baada ya kufukuzwa UWAZIRI
NAPE alimtukana sana Hayati LOWASSA Waziri Mkuu Mstaafu bila kujali michango yake ktk Chama na Serikali
Je Leo NAPE Ana usafi gani wa kumnyooshea kidole Mh.TUNDU LISSU?
NAPE aache UNAFIKI
 
Kati ya Nape na Lissu nani ni mpuuzi?
 
Nape ,Nape nampa siku 14 akatubu vinginevyo nitafunga siku 14 kwa ajili yake na Mungu atashughulika nae ,labda kama hili taifa sio la Mungu na yeye sio mtanganyika
 
NAPE AMVAA LISU KUTUMIA MANENO YA KIBAGUZI KWA RAIS SAMIA

“Watanzania asilimia 70 mpaka 80 tumezaliwa baada ya muungano, kwa hiyo hatujui kule nyuma sisi tunajua muungano wetu, ndiyo maana ni muhimu sana Watanzania tukahamasishana kuulinda na kuutetea kwa wivu na nguvu kubwa sana” Nape

“Kumeanza kutokea wanasiasa wenzetu nadhani kwa kufilisika kisiasa wameanza kutomasatomasa utamaduni wa kuheshimu katiba yetu, utamaduni wa kuheshimu muungano wetu, na wanatumia maneno ya ‘hovyo’ kidogo ambayo tukinyamanza tukayavumilia kidogokidogo utamaduni utaporomoka tutaliangamiza taifa letu , muhimu tuwakemee” Nape

“Yuko mjomba wangu mmoja anaitwa Tundu Antipas Lissu juzi akiwa Babati Manyara amesimama mchana kweupe akaanza kukosoa baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita, kukosoa siyo tatizo lakini alikuwa anakosoa akisema ‘haya mambo yamefanywa kwa sababu Rais aliyeko madarakani ni Mzanzibari’, hili tukilinyamazia litaota mizizi litabomoa taifa letu, hatuwezi kukubali mambo ya mtu mmoja kalewa na akaleweshwa na utu, ubinadamu, uzalendo na uungwana na huyu anayemwita Mzanzibari” Nape.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye wakati akichangia hoja ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Jumatatu Aprili 29, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…