Nape Nnauye: Nilikatazwa Kwenda kuchunguza Uvamizi Clouds, niliambiwa nitafukuzwa kazi

Nyie mnao semaga mbona hukusema wakati yupo huwa nawaona mnaakili ndogo sana sijui kwanini?
Sasa si achukue hatua, afanye uchunguzi, clouds wapo, aliyevamia yupo, yeye kama waziri yupo, muda upo, raslimali zipo, sheria zipo, nini kinamshinda sasa hivi kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kuchukua hatua?
 
Clouds hawawezi kurudi kivingine kama wale wengine waliorudi kudai nyumba na magari yao?
Unafiki pro max makonda na clouds washayamaliza kitambo iweje uje leo kuropoka,tz kila mtu anajifanya anajua,hongera mwenye akili kubwa Kama kichwa chako[emoji23]
 
Katika hili, nilikuwa naomba nijaribu kumshauri Mh. Waziri aache kuendelea kuongelea mambo negative yanayomhusu Rais wa Nchi bila kujali ni Rais aliyepita, aliyepo au atakayekuja; assuming hatakuwa yeye , kwa sababu mpaka muda huu bado mamlaka hiyo hiyo ndiyo iliyomuona kuwa anafaa na hivyo kumpa heshima ya kuendelea kutumika chini ya mamlaka hiyo.

Mpaka muda huu, Mh. Waziri anatumika kwenye mamlaka ile ile; huku aliyebadilika kwenye mamlaka za juu akiwa ni mtu tu

Kwa Mh. Waziri kuendelea kuongelea maswala yaliyopita anakuwa kwa namna fulani haitendei haki mamlaka iliyopo sasa, na ambayo ndiyo bado anaendelea kutumika chini yake
 
Shirika la TTCL linakufa mikononi mwako fanya KITU KULINDA HESHIMA YAKO. Usituletee HABARI ZILIZOPITA HAPA
 
Nilikatazwa nilikatazwa, TTCL inakufa mikononi mwako!
Tafuta jinsi ya kuinusuru.
 
Kwa nini hakujiuzulu kuonyesha msimamo wake?
 
Hilo lina msaada gani kwetu sisi katika ugumu huu wa maisha ??

Atutolee ujinga wake hapa.

Watu kazi hawawezi wanangangania tu ofisi za uma kama ni za mama zao.
 
Uliwaona hao watu wenye silaha? Maana Video ilimwonesha akipita mapokezi tu na hakuna uvamizi wowote ule uliyoonekana. Hebu tuoneshe wewe ushahidi walikuwa na silaha
 
huyu jamaa kilaza sana!
hivi kwa nafasi aliyonayo ni wa kutueleza hayo? sisi yanatusaidia nini kwa leo hii? au anafikiri nafsi zetu haziumii kwa yeye kukumbatia makampuni ya simu?halafu huyu anafikiria katika mawazo yake anaweza kuwa waziri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…