Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ndugu Nape alipohojiwa kuhusu vuguvugu la kumuongezea Rais Magufuli muda wa utawala wake amesema haya yafuatayo.
1. Kwanza anashangazwa na kwamba ndiyo kwanza miaka mitano ya muhula wa pili wa utawala wa Rais Magufuli umeanza halafu watu wanaanza kuzungumza ya baadae, wakati haya waliyoomba kura kwayo hawajayamaliza.
2. Pili anashangazwa na watu wanaowaza utadhani wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuhusu kujua nani atakuwepo kesho na nani hatakuwepo.
3. Anasema, Kilicho cha msingi ni kujenga mifumo imara ili hiyo mifumo iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana na tusigeuze mtu kuwa ndo mafanikio yenyewe maana watu huja na kuondoka na Mungu ndo anapanga uhai wa watu.
MY TAKE
Msimamo wa Nape ni msimamo mzuri, wanaotaka Magufuli abaki madarakani kinyume cha katiba ya sasa hao wanajali maslahi yao binafsi na si ya nchi yetu. hawana tofauti na wale ambao Nyerere alisema kila alipotaka kung'atuka walimwambia Mzee endelea bila wewe nchi itayumba kumbe ikaja kugundulika walikuwa wanajali matumbo yao binafsi, walikuwa hawana uhakika kuwa akitoka madarakani basi Rais ajaye atawalindia nyadhifa zao!
Msikilize wewe mwenyewe hapa:
MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUONGEZA MUDA NI HUU HAPA CHINI