Naomba nijibiwe maswali haya juu ya hili suala ambalo linaweza kuibua hisia Kali sana za wananchi katika taifa ambalo limejivunia amani miaka yote.
1.Nape amekosea kitu gani mpaka atolewe bastola hadharani?
2.Kuna kitu gani kibaya hasa kilichamfanya mwanausalama kutotambua wajibu wake juu ya matumizi ya silaha?
3.Ni sheria gani inayemruhusu mwanausalama kumtishia silaha raia tena kiongozi asiyebeba hata fimbo mkononi?
4.Kama ni hivi kwa mtu ambaye jana tu alikua kiongozi mwanamizi wa serikali itakuaje kwa raia wa kawaida?
5.Mtu anakuuliza kitambulisho wewe unamtolea silaha ya moto, ndicho alichokuuliza?
6.Hizi chuki zenye hasira za hali ya juu kiasi hiki zimeanza lini na nini hatima yake?
7.Wanaharakati wa haki za binadamu mnaliambiaje taifa juu ya hili?
8.Mh Nape ni mtoto wa kada na kiongozi aliyekua na mchango Mkubwa ndani ya CCM na aliacha historia, Je, ni kweli wa kumtishia bastola hadharani?
9.Huyu askari alitumwa na nani?
10. Mh Nape ana familia inayomzunguka anatishiwa silaha ya moto hadharani,ni taswira gani amejengewa mbele yao?
11.Nape pamoja na kua mchango mkubwa ndani ya CCM takribani miaka 8 mfululizo, nini amepandikiziwa kichwa ni mwake katika historia ya maisha yake yote ya siasa?