Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Polepole aweza kuwa mzuri katika administration,lakini si kazi za majukwaani,hana mvuto,havutii wasikilizaji inshort anabore,

makonda tatizo kubwa ni dharau,kebehi,ngebe na umuchknow fake hawezi kufanya uenezi,

nape ile kazi ilikuwa imemfit hasa.

Ile kazi hata ole sendeka angechemsha 2020
 
Sisi wapinzani hakika tunaumia sana,nadhani ni wakati sasa nanyi mkaona ubaya wa matumizi mabaya ya vyombo hivi vya ulinzi kwa umma wenye nia njema.
 
Nape yuko vizuri sana kwa uenezi, hakuna kama yeye kwa zama hizi.

Ccm wamuombe msamaha, in one way or another, watapoteza mtu muhimu sana kwao
 
Namkumbuka sana Jakaya Kikwete kwa haya majanga yanayotukuta WaTZ natamani arudi kidogo ayaweke sawa kisha akapumzike
 
____________________
Pongezi kiduchu zimfikie Nape Nnauye kwa kuonesha kuwa kinyume na ufedhuli, lakini pongezi hizo kiduchu na hatua yake ya kuwa kinyume na ufedhuli, havifuti ufedhuli wake. (Nape ni fedhuli anayevuna alichopanda).

Kwa maneno machache tu;

1. Nape na vijana wenzake wa CCM ndio waliozunguka nchi nzima kumtukana Lowassa, ambaye wakati huo alikuwa moja kati ya watu muhimu ndani ya Chama chao. Lakini kwa sababu ya kutumikia makambi na makundi ya chama, wakazunguka kutukana na kupakaza uongo kwa manufaa ya kundi fulani.

2. Nape ndiye aliyetangaza ushindi wa CCM hata kwa goli la mkono, akijua kabisa ni kinyume cha demokrasia.

3. Nape ndiye aliyewatolea maneno machafu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, waliodai uchaguzi ulikua na mapungufu mengi.

4. Nape ndiye aliyetangaza kulifungia MILELE gazeti la Mawio, kwa madai ya uchochezi, kwa sababu tu liliandika habari zisizowafurahisha watawala.

5. Nae mdiye aliyelifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 (miaka mitatu) kwa madai ya kuandika habari zenye kumchafua Naibu waziri wa Ujenzi Edwin Ngonyani.

6. Nape ndiye aliyefungia Radio Magic Fm na Radio Five Arusha kwa madai ya uchochezi, kisa tu radio hizo zilikua zilitoa nafasi kwa viongozi wa upinzani kuongea na wananchi.

7. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kufuta bunge Live, na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kufuatilia kazi za viongozi wao bungeni.

8. Nape ndiye anayedaiwa kuagiza Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi Selemani Mathew afungwe gerezani kwa kufanya mkutano bila kibali, kwa sababu Mathew alimshinda kwenye kura za maoni jimbo la Mtama mwaka 2015 akakatwa, na kwenda Chadema.

9. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ndiye aliyesema CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa vipande vya karatasi.

10. Nape ndiye aliyetengeneza propaganda ya kusema Lowassa ni mgonjwa na hafai kuwa Rais. Propaganda hiyo ilitumika na viongozi wa CCM kumchafua Lowassa na kumpunguzia kura.

11. Nape akiwa mkoani Ruvuma kwenye ksmpeni za uchaguzi, alimuita Magufuli Rais hata kabla ya uchaguzi. Yani alijiona kama Mwenyekiti wa Tume ya ucjaguzi mwenye uwezo wa kupanga matokeo na kuamua nani awe kiongozi.

12. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa NEC na mjumbe wa Kamati Kuu ndiye aliyewasilisha azimio kwenye Kamati ya maadili la kumkata Lowassa katika hatua za awali za mchujo. Azimio hilo liliungwa mkono na wajumbe wengine na Lowassa hakupita hata kwenye 5 bora.

13. Nape ndiye aliyeshawishi wafuasi wa Lowassa waliobaki CCM watimuliwe akiwemo Mhe.Sophia Simba ambaye amevuliwa uanachama na kupoteza ubunge wake na uenyekiti wa UWT.

14. Nape ndiye aliyekuwa injinia wa kupitisha muswada wa sheria mbaya kuliko zote ya habari, ambao tofauti na lengo linaloelezwa, ukiisoma sheria ile na kuielewa, utagundua sio tu inaminya uhuru wa kupashana habari lakini pia inapingana na stratejia za kupambana na ufisadi, stratejia ya 'Whistle blower policy' inayotajwa kuwa bora kabisa katika kupamabana na ufisadi, inawekewa ukinzani na sheria ya Habari ambayo Nape alihusika moja kwa moja katika kuipitisha.

15. Nape ndiye aliyepigania sheria ya mitandao ipitishwe akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ili kuzuia nguvu ya vijana wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

16. Nape ndiye ameongoza juhudi za waandishi kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa. Hakuna kipindi waandishi wameishi kwenye mateso kama kipindi cha utawala wa Nape.

17. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kutaka vyombo vyote vya habari (Radio na TV) vijiunge na TBC kila siku saa 2 usiku kwa ajili ya taarifa ya habari.

18. Nape ndiye aliyepitisha muswada wa habari (ambao kwa sasa ni sheria) ya kulazimisha waandishi wote wa habari kuwa na degree moja kabla ya mwaka 2021. Mwandishi ambaye hatakuwa na degree wakati huo HATATAMBULIKA kama mwandishi wa habari.

Huyo ndiye Nape Moses Nnauye ambaye leo kuna watu wanamuona shujaa, kwa sababu amevuliwa uwaziri. Hivi yeye ni mtu wa kwanza kuvuliwa uwaziri? Mgogoro wake na Makonda haumfanyi kuwa shujaa.

Kuna watu wanasema ni shujaa eti kwa sababu ya kuunda kamati ya Uchunguzi uvamizi wa Clouds. Lile ni jukumu lale kama Waziri. Na asingefanya hivyo umma ungemiwajibisha. Sasa mnamuonaje shujaa mtu aliyetimiza wajibu wake? Hivi housegirl wako akideki nyumbani utamuona shujaa wakati ametimiza wajibu wake?

Labda tumpongeze kwa ujasiri wa kujitokeza hadharani na kupinga udikteta wa Rais wake. Udikteta ambao Lissu ameupinga kwa muda mrefu. Wakati akina Lissu wanaongea akina Nape walidhani hawahusiki, kwa hiyo wakakaa kimya. Leo yamewakuta wanataka kufanya ni msiba wa kitaifa.

Yani wakati Lema anakamatwa na kudhalilishwa akina Nape walikaa kimya. Lissu kukamatwa na kudhalilishwa Nape kimya. Vijana wa upinzani kunyanyaswa, kupigwa (refer Mdude), kufungwa magerezani (refer Mwaifunga) na wengine kupotezwa (refer Ben Saanane) Nape na wenzie walikaa kimya kama vile hayawahusu, leo yamemkuta yeye anaonekana shujaa?

Ukweli ni kwamba Nape hajawahi kuwa mtu muhimu kwa taifa, bali amekuwa mtu muhimu sana kwa CCM. Ameisaidia CCM, ameipigania CCM alijitoa kwa ajili ya CCM. Alifanya kila aliloweza kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Nape, January na Mwigulu ndio waliomuweka JPM madarakani kwa kutumia mbinu halali na haramu. Bila hawa watu watatu pengine tungekuwa tunsongea mengine kwa sasa.

Kwahiyo kinachomtokea Nape ni matokeo ya kile walichokitengeneza wenyewe. Anavuna matunda ya ufedhuli wake. Nape kafanya uovu mkubwa sana kwenye nchi hii ili kuisaidia CCM. Ni uovu wenye manufaa kwa CCM, sio kwa Taifa.

Kwa hivyo, ikiwa Nape anahitaji huruma, basi atahitaji zaidi kuonewa huruma na a wanaCCM wenzake kuliko watanzania aliowanyanyasa, kuwakebehi na kuwadharau kwa muda mrefu.

Ushauri wa bure: Nape kama mwanasiasa mwingine yeyote ana tamaa ya madaraka makubwa zaidi kuliko aliyowahi kushika. Kwahiyo ni veama akawa mkimya kwa kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile. Akae kimya, arudi kuwatumikia watu wa Mtama. Asome kitabu cha Robert Green; 48 laws of power, aangalie amekosea wapi.

Zaidi ya hayo, amtafute mzee Lowassa amuombe msamaha na kuomba somo zaidi la siasa. Ajifunze kwa nini Lowassa bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa pengine kuliko aliyemteua na kumtumbua. Alamsiki.!
 
wewe nyamaza maneno gani hayo vyombo vina nini wewe unalindwa na nani ktk hii .acha post za kiupuuza kama huna la kuongea usitumue jukwaa kuleta chokochoko.
 
Alitakiwa Nape baada ya kuachishwa uwaziri na kubaki mbunge tu alitakiwa akafanye siasa jimboni kwake walikomchagua sio dar yeye sio mbunge wa dar. Kajisahau anafikiri yeye bado waziri. Waziri ni mwakyembe yeye kwa sasa ni mbunge kama godbless lema au msigwa siasa na Press conference azipeleke jimboni kwake alikochaguliwa kinondoni alipofanyia Press conference amwachie mbunge wa kinondoni.Kasahau kuwa ukiwa mbunge siasa kafanye kwenu ulikochaguliwa hili ni kwa wote wabunge wa CCM na upinzani. ndio maana polisi walimdhibiti
hahahahah kweli arudi lindi akaitishe press conference huko
 
.
Mara nyingi sana tumezomea kuona Jeshi la Polisi wakitumia nguvu kubwa sana kupambana na upinzani kuliko kutumia akili au njia sahihi katika kutimiza wajibu wao huo.
Kitendo ambacho kimefanywa leo na Afisa wa Jeshi la Polisi kuonyesha bastola hadharani kinatakiwa kulaani na kupingwa kwa nguvu zote.
 
Lowassa hana kinyongo ni mwanasiasa wa Kihistoria kupata kutokea Tanzania. Katika Historia ya siasa nchini hilo jina lisipotajwa bado historia itakuwa haijakamilika.
Tatizo la lowasa ni kutozingatia biblia kuwa patana na kumalizana na mshitaki wako kabla ya kuingia kwenye uchaguzi lowasa alijifanya kichwa ngumu akajifanya kumhujumu kikwete muda wote wa utawala wa kikwete akawa anajenga mitandao hujuma ndani ya serikali ya kikwete ili kikwete aonekane dhaifu kwa kila asemalo au kutenda yaliyomkuta lowasa haji sahau.Mungu kamlipa sawasawa na hila zake yeye na wapambe wake
 
68a264f5f80228796f8a5490efd86f5a.jpg
 
Nape gemu lake lilishanaswa

Akajisahau zaidi aliposifiwa Mtwara na Mh. Rais

Kumbe anaangaliwa, hivyo akajiona hawezwi kumbe mmmmh
Jicho la Mwewe, binafsi pale nilihisi kampamba tu Lindi, uwanja wa nyumbani, Nape akaona ye ni shujaa sababu, chadema na Mange walimpa sifa za kijinga, kumbe hizi sifa ni za siku Tatu baada ya hapo, Nape atachambwa na upinzani mpaka akome
 
Dhambi kubwa ni UNAFIKI.Ni punguani tu atakuelewa mh. Rais wa TLS. Kumbuka hii kauli, SISIEMU IMEMPA FISADI FOMU YA URAIS, NI HATARI.
Hii kauli itakuandama popote uendapo!
 
Hayo ni matokeo ya goli la mkono, ndo yanaanza kutoka. Mwisho wa ubaya aibu. Nape siyo wa kwanza na wala hatakuwa wa mwisho.
 
Wakuu amani iwe kwenu.. ..

Leo naomba nitoe ufafanuzi kuhusu tukio ambalo kaka yangu NAPE limemtokea na hii nikutokana na mkuu wa nchi kutaka sana mtawala katika serikali yake.

TOFAUTI YA KIONGOZI NA MTAWALA.

KIONGOZI

1. Ni mtu wa Watu

• Kiongozi kipaumbele chake ni watu

• Anakuna kichwa afanye nini ili watu wake waweze kuishi kwa amani na furaha.

• Kupenda kuwasikiliza watu wanasema nini, wanalia juu ya nini, wanacheka juu ya nini nk.

2. Hugusa Moyo wa Mtu

• Mkono wa kiongozi hugusa moyo wa wafuasi.

• Ushawishi wake kiongozi huwa sio wa akilini au kichwani bali hupenya hadi ndani ya moyo wa mtu.

• Anauhakika wa kuwa na watu nyuma yake kumfuata popote atakapo kwenda

3. Huuliza Kuna nini Moyoni

• Hutaka kujua nini kimeujaza moyo wako

• Mbona huna furaha moyoni kumetokea nini? Nifanye nini kukusaidia furaha ya moyo wako iweze kurudi.

• Mbona unafuraha sana leo nini kimetokea mpaka umekuwa mwenye furaha hivyo moyoni? Unahitaji kuendeleza hiyo furaha yako.

4. Hufundisha Watu
Kiongozi hufundisha watu na sio kufundisha somo
Kiongozi hutamani hata Yule mbumbumbu asiyeelewa darasani au kanisani ameelewa na kupokea kitu.

Huchukua juhudi za makusudi kufuatilia zaidi.
Kipimo chake cha uwelewa wa wanafunzi ni Yule mtu wa mwisho kuelewa darasani.

5. Ana upeo wa Kuona Mbali

• Huangalia faida itakayopatikana kule mbele sio lazima sasa.

• Anawekeza sasa kwaajili ya sasa na badae

• Anawekeza vikubwa anavuna vikubwa pia.

• Anafanya leo kwajili ya kesho

6. Ni Mbunifu na Muanzishaji (Originate)

• Anamawazo mapya

• Anabuni na kuwapa wengine

• Anaweza kubuni na kupitisha barabara katikati yam situ mnene mahali usingefikiri kamwe barabara ingepita

• Ni mvumilivu kusubiria matunda kwa wakati wake.

7. Hujiuliza Nini na Kwanini (What and Why)

• Ninafanya nini na kwanini ninafanya hiki.

• Huwa na sababu ya kutosha kumuwezesha kufanya anachokifanya kwa nguvu zaidi.

MTAWALA

1. Ni Mtu wa Vitu

• Kitu cha muhimi kwake ni vitu sio watu.

• Kama ni mmiliki wa basi, likipinduka chakwanza kuuliza gari imesalimika haijaumia?

• Akiambiwa mzee gari imepona ila watu wote wamevunjika vunjika na kufa atasema afadhali.

• Akiambiwa gari imesagiga sagika hakuna hata cha kuokota ila watu wote wamesalimika ataangua kilio kweli maana gari imekwisha.

2. Hugusa Vitu vya mtu

• Tofauti na kiongozi mtawala hagusi moyo anagusa vitu

• Mitambo au vitu nivyamuhimu sana kuliko watu.

• Chombo kikiungua ni hasara kubwa sana lakini mtu akivunjika mguu ni kawaida ajali kazini.

3. Huuliza Kunanini mfukoni

• Tofauti na kiongozi ambaye huuliza kunanini moyoni, interest ya mtawala nikujua kuna nini mfukoni.

• Hugusa pochi na sio moyo

• Hugusa kichwani na sio Moyoni

4. Hufundisha Somo

• Hufundisha somo watu na sio kufundhisha watu somo

• Hufundiaha kumaliza mtaala na sio kufundisha kuwaelimisha.

• Hufundisha kwa kuwapa wanafunzi taarifa, na sio badiliko la maisha.

• Teaching for information not transformation.

5. Ana upeo wa Kuona ya Sasa

• Hushughulika sana na ya sasa.

• Macho yake ni dhaifu hayana nguvu ya kuona ya mbele.

• Anataka kupanda leo na kuvuna leo.

• Hana mpango wa kuwekeza kwaajili ya baadae.

6. Huiga na kukarabati Kilichokuwepo (Immitate)

• Hana uwezo wa kubuni vitu vipya.

• Yeye huendeleza walivyobuni wengine

• Kama ni barabara hana uwezo wa kubuni barabara mpya ataziba tu viraka vya barabara aliyokabidhiwa.

• Kama ni kanisa akipewa hata kama likijaa hawezi kuja na mpango mpya wa kujenga linguine la kisasa bali atakuwa anabadilisha tu milango na kupiga rangi upya nk.

7. Hujiuliza Kivipi na Lini (How and When)

• Nitafanyaje hiki nilichopewa kiendelee kuonekana kizuri?

• Lini nitaweza kutekeleza hii kabla sijanyan’ganywa madaraka haya?

NB: VIONGOZI WENGI TUNAO WAITA “VIONGOZI” KIUKWELI SIO VIONGOZI NI WATAWALA

Nape kamwambia onyesha kitambulisho katoa bastola, sasa akiambiwa onyeahe cheti si atatoa BOMU?

Karibuni kwa mawazo.
 
​

Heshima Kwenu wakuu,

Leo nmeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.

Karibuni.

=======

UPDATES;


=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.

1415hrs: Nape amekuja lakini akazuiliwa na Askari(Wanausalama(?) ili asifike sehemu ya tukio, akaamua kushuka ili aje kwa mguu, wakaanza kumvuta kumrudisha kwenye gari. Walikua maasikari kama wanne. Ilikuwa sio mbali kutoka Sehemu waandishi wa habari walipokuwa, Sema walikuwa kwa ndani.

Aliyewajulisha Wandishi wa habari kwamba Nape kazuiliwa nje ni dereva wa Nape aliyeanza kupiga honi ya gari kwa nguvu kitu kilichowastua waandishi wa habari na kuwafanya watoke nje. Walipotoka nje wakakuta nape anavutwa aingie ndani ya gari ila Waandishi walipofika Askari wakapunguza kasi

1428hrs: Nape anaongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli akiwa juu ya gari.

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu

Mimi ndo nimekuwa mzalendo kwa CCM, ambayo niliikuta ikiingia kwenye shimo inakwenda, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, na nilichokisiamamia juzi ni kusema kweli, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, kamaninachokiamini kitaleta matatizo mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepanda mbegu ya kupigania haki hakika itaota, Tanzania ni yetu nchini yetu. Vijana hamna la kuogopa simamieni mnachokiamini Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.

Sisi pia tutaondoka suala la kujiuliza tutaawaachia watoto wetu nchi ya aina gani, hilo ndio kubwa,uamuzi ni wa kwetu wenyewe

Lengo la kuja hapa ni kumshukuru Rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.

Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli ndiye rais tuliyenaye na kudumisha umoja na mshikamano.

Tumefanya kazi pamoja na nimefurahi sana kufanya kazi na nyie
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia.

Niliomba kazi ya Ubunge na sio uwaziri, sasa narudi kuwatumikia wananchi wangu wa Mtama

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni

Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena

​


View attachment 485542

View attachment 485512

Nape akasome kitabu cha 48 Rules of Power. Pia atambue yeye bado ni kijana na ana safari ndefu kisiasa, ajifunze kutumia mdomo wake vizuri na aache tabia ya kulalamika lalamika (GRUMBLER) pembeni akidhani hawamsikii... hii rebellious behaviour haitamsaidia kisiasa, na kamwe huwezi kushindana na mwenye dola, utaumia tu. Jifunze kujua mipaka ya mamlaka yako na usifanye insurbodination kwa kigezo cha kutetea haki etc... hii haikubaliki kwa serikali yoyote duniani, mfano, TRUMP alimtoa kazini Mwanasheria aliyekataa kwenda Mahakamani kutetea sera ya uhamiaji ya kibaguzi (Huu ni mfano tu kwamba INSURBODINATION haikubaliki kwa Serikali yoyote). najua atatetewa sana hapa ila alichofanya Rais ni sahihi kabisa. Pia ujifunze kuwa humble.. unaposema ulikipigania chama siku 28 porini, ulikua peke yako??? chama ni tasisi na sio mtu mmoja. ulikipigania chama peke yako???? nadhani wapo watu wengi ambao hawaonekani kwa macho na hawafahamiki lakini kila siku hukesha na kuhangaika kuhakikisha TZ inakua salama na ina shamiri. Watu hao kwa kushirikiana na watanzania wengine ndio wanaifanya nchi yetu kuwa tulivu na kushamiri. Huu ni ushauri tu kwa Nape, sijatetea ya Makonda, ila namshauri Nape kama Mwanasiasa kujitafakari. Leo wanakushangilia kwamba wewe ni shujaa, wamesahau ya nyuma, ila kumbuka 2020 utaenda tena jimbo la mtama kuomba kura baada ya kuwa UMEPITISHWA NA CHAMA CHAKO KUGOMBEA!!!!!! Nenda Kawafanyie Kazi wana Mtama ili 2020 usikatwe. Kwaheri.
 
Back
Top Bottom