Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

nimeshangaa joka la mcheza ngoma lilivyotaka kummeza mcheza ngoma kimzaha mzaha!!!! majoka wameyafuga wenyewe na kuyafundisha mbinu za kuwabinya adui leo joka limembadilishia gia mtunza joka!!!!!!!!!!!
 
Kuna mwingine akikosa hako ka upendeleo ka ukuu WA MKOA basi itakuwa mwisho WA dunia !!
 
Kwa maoni yangu kikubwa kinachomsumbua Nape Nnauye ni kutokuubali ukweli kwamba muda wake ndani ya CCM umekwisha au niseme kwamba ulikwisha siku ambayo Mwenyekiti mpya wa CCM alipochukuwa kutoka kwa Jakaya Kikwete, sasa kwa hali ya kawaida ilipaswa Kikwete na Timu yake wote waende na watoe nafasi kwa Mwenyekiti mpya kuunda Timu yake, Kikwete alifanya hivyo alipochukuwa ktk kwa Mkapa na Mkapa alifanya hivyo hivyo alipochukuwa ktk kwa Mwinyi!

Sasa kinachomsumbua Nape na timu yake ni kukubali hilo kwamba, kuna wakati unafika inabidi ukubali na kulet go!

Kwa nini nimetumia mfano ya maisha ya Binadamu? Hapa Duniani kila baada ya miaka 100 kizazi kipya huja, na kile kilichopo hupotea na haijalishi kama wewe ni drug dealer, hardcore criminal au Binadamu mzuri unayestahili kupewa Utakatifu lkn wote baada ya miaka 100 huenda kama vile Maji ya bahari yaoshapo mchanga ufukweni ndiyo maana Kijana aliyezaliwa mwaka 2000 don't give a shit abaout Nyerere atakwambia Nyerere ndo nini? Lkn waliozaliwa nyuma ya hapo wanamjali na mnaweza kukosana ukimuongelea vibaya Nyerere, vivyo hivyo CCM imejiwekea huo utaratibu kwamba kila baada ya miaka 10 Timu mpya huingia, na iliyopo hukabidhi na kupotea kabisa, sasa huu ni ukweli ambao Bw.Nape nafikiri unampa shida kuukubali jana alikuwa kama Mfalme akienda mahali ni kama Raisi kaingia, ukitaka Cheo Kikubwa CCM na Serikalini ni lazima umlambe miguu, ukigombana naye ndiyo mwisho wako na ajira yako itaota majani, hiyo ni power kubwa sana na leo hii ni no body sasa ni ngumu adjust kwenye maisha mapya nionavyo mimi na ndiyo maana anatoa maneno kama sijui nimepigania chama tangu Baba yangu sijui blah blah hakuna aliyepigania Chama kama Nyerere, Kawawa, Kingunge, Msuya, &Co. kama ni kuwa mtoto wa mkubwa hata Watoto wa Kawawa, Nyerere, Kingune au hata Mwinyi na Mkapa pia wanaweza kusema hivyo hivyo so no big deal, lkn wanajua kwamba muda wao umepita na wame let go!

Hivyo Nape kubali kwamba CCM iko hivyo, watakupump, watakushawishi na kukusifia lkn ukweli ni kwamba sasa hivi uwezo wako uko limited maadamu hauna mtu aliye nyuma yako ambaye anaongoza Dola, hivyo wanakudanganya tu kama siyo kukutumia!

Magufuli ataunda Timu kama vile Kikwete alivyounda yake wewe ukiwemo na siku itafika Magufuli itabidi yeye na Timu yake wakabidhi pia, na cycle kujirudia upya kama na wao wakitaka kuingilia Timu mpya yatawakuta yaliyokukuta ...

Kila La Heri Nape!

Huyo mwanaccm anayesema "Nyerere ndiyo nini?" hana tofauti na kijana ambaye anatembelewa na baba yake mzazi. kijana huyu anamwangalia baba yake aliye kikongwe, hajijali tena kama zamani, akili zake kama zimepungua kidogo, anaongea mambo ya "kizamani" , anaishia kumwambia baba yake mzazi "baba ndiyo nini".

Kuna tatizo kubwa sana, kwamba ninyi mnaojiita wana CCM wa kisasa, hamtambui kabisa kwamba historia ni muhimu sana. kujua unatoka wapi, inakusaidia kutambua ulipo na hivyo una nafasi nzuri sana ya kupanga uende wapi. na wala haishangazi kwamba hiyo CCM tunayoiongelea hivi sasa, wala siyo ile CCM ambayo tuliijua, na wengine kama sisi tukaichezea gwaride kali ilipozinduliwa mnamo 1977, kwa kuunganisha TANU na ASP. nakumbuka wakati huo tukiimba "Mimi ni Chipukizi wa TANU, nitakitumikia chama changu cha TANU. Sitakuwa na fikra za kibepari wala kikabaila....saa yoyote, Mungu nisaidie".

Mojawapo ya Imani za TANU ni kwamba "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja". wakati huo usingeshuhudia operesheni za kufukuza "wasio watanzania". maana TANU ilitambua kwamba mipaka imewekwa na mkoloni ili kututawala. tunaiheshimu kwa sasa lakini lengo letu ni kuungana. sasa hebu angalia CCM ilivyopoteza mwelekeo hivi sasa. hakuna principles. ndio maana kila kitu ni halali. na hata wale wanaounga mkono au kupinga, hawaoneshi ni kwa misingi gani hiki ni sahihi na hiki siyo sahihi.

CCM tunayoijua haikuwa hivi ilivyo sasa, kwamba ukifika muda watu wa timu ya zamani wanaondoka na ndiyo basi tena imekula kwao. ndiyo maana Nyerere kuanzia miaka ya 90, miaka zaidi ya 5 toka alipoondoka madarakani na kujiuzulu nyadhifa zote, alirejea ulingoni na kuiongoza Tanzania katika maandalizi ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. aliilazimisha CCM kufanya maamuzi mengi tu, ambayo wanaccm wakati huo hawakuwa wakiangalia maslahi ya taifa bali maslahi ya matumbo yao. na tokea amefariki, hili ndio limekuwa tatizo la CCM. kujali matumbo badala ya maslahi ya taifa.

Nape ameangalia maslahi ya taifa, na kwa kuwa serikali ya CCM kwa sasa inaangalia zaidi maslahi binafsi kuliko ya taifa, ndio maana ameishia hapo alipoishia. lakini kumbuka kwamba kwa kujitoa kwake, ameweka chachu zaidi katika mabadiliko. mwenyewe alitamka kwamba kutetea haki za watu kuna gharama. kama hakuna watu ambao wako tayari kubeba gharama hizo, kama Mandela alivyobeba kwa kukaa jela miaka 27, basi tumekwisha kama taifa
 
Pigilia Mstari kabisa hayo ndo majibu sahihi. Sasa tafakari kina Lema & Lissu huwa inakuwaje huko mafichoni? Je, Dr Ben Saa8 anafanywaje huko mafichoni?

Nyerere aliwahi kutahadharisha juu ya mamlaka ya Rais, pia alionya kuwa siku akapatikana Rais dikteta lazima namba isomwe.
 
Huyo mwanaccm anayesema "Nyerere ndiyo nini?" hana tofauti na kijana ambaye anatembelewa na baba yake mzazi. kijana huyu anamwangalia baba yake aliye kikongwe, hajijali tena kama zamani, akili zake kama zimepungua kidogo, anaongea mambo ya "kizamani" , anaishia kumwambia baba yake mzazi "baba ndiyo nini".

Kuna tatizo kubwa sana, kwamba ninyi mnaojiita wana CCM wa kisasa, hamtambui kabisa kwamba historia ni muhimu sana. kujua unatoka wapi, inakusaidia kutambua ulipo na hivyo una nafasi nzuri sana ya kupanga uende wapi. na wala haishangazi kwamba hiyo CCM tunayoiongelea hivi sasa, wala siyo ile CCM ambayo tuliijua, na wengine kama sisi tukaichezea gwaride kali ilipozinduliwa mnamo 1977, kwa kuunganisha TANU na ASP. nakumbuka wakati huo tukiimba "Mimi ni Chipukizi wa TANU, nitakitumikia chama changu cha TANU. Sitakuwa na fikra za kibepari wala kikabaila....saa yoyote, Mungu nisaidie".

Mojawapo ya Imani za TANU ni kwamba "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja". wakati huo usingeshuhudia operesheni za kufukuza "wasio watanzania". maana TANU ilitambua kwamba mipaka imewekwa na mkoloni ili kututawala. tunaiheshimu kwa sasa lakini lengo letu ni kuungana. sasa hebu angalia CCM ilivyopoteza mwelekeo hivi sasa. hakuna principles. ndio maana kila kitu ni halali. na hata wale wanaounga mkono au kupinga, hawaoneshi ni kwa misingi gani hiki ni sahihi na hiki siyo sahihi.

CCM tunayoijua haikuwa hivi ilivyo sasa, kwamba ukifika muda watu wa timu ya zamani wanaondoka na ndiyo basi tena imekula kwao. ndiyo maana Nyerere kuanzia miaka ya 90, miaka zaidi ya 5 toka alipoondoka madarakani na kujiuzulu nyadhifa zote, alirejea ulingoni na kuiongoza Tanzania katika maandalizi ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. aliilazimisha CCM kufanya maamuzi mengi tu, ambayo wanaccm wakati huo hawakuwa wakiangalia maslahi ya taifa bali maslahi ya matumbo yao. na tokea amefariki, hili ndio limekuwa tatizo la CCM. kujali matumbo badala ya maslahi ya taifa.

Nape ameangalia maslahi ya taifa, na kwa kuwa serikali ya CCM kwa sasa inaangalia zaidi maslahi binafsi kuliko ya taifa, ndio maana ameishia hapo alipoishia. lakini kumbuka kwamba kwa kujitoa kwake, ameweka chachu zaidi katika mabadiliko. mwenyewe alitamka kwamba kutetea haki za watu kuna gharama. kama hakuna watu ambao wako tayari kubeba gharama hizo, kama Mandela alivyobeba kwa kukaa jela miaka 27, basi tumekwisha kama taifa

Ndiyo nikakupa mfano ya Maisha ya Binadamu, hubadilika baada ya muda mtoto anayezaliwa leo hii hata ufanye nini hawezi kumjali Nyerere kama unavyomjali wewe, utamuimbia nyimbo zote utakazo lkn mazingira anayokulia ni tofauti na hayaruhusu kuelewa kuhusu Nyerere kama ulivyoelewa wewe ndiyo maana Mzungu anayezaliwa leo AK anajichanganya na Waafrika kuliko Wazazi wake, au mtoto wa AK mweusi anayezaliwa leo hii hajui na wala hajali kuhusu Apartheid kuna mambo mengine anayojali zaidi kama ajira, usalama n.k. na ndiyo maana Vijana AK wanavamia wageni Waafrika ktuoka Afrika na siyo Mzungu mkabulu, sababu ndiyo hiyo kwamba huyu Mzungu kwa sasa siyo tatizo lake, taizo lake ni Mnigeria anayechukuwa kazi zake, anayeuza drugs kwa watoto wake n.k. na hayo ndiyo maisha yalivyo hauwezi kubadilisha hilo!
 
Bahati mbaya mnao mkejeri nape ni vijana wadogo ambao hata hamuifahamu ccm vizuri!
Mnaamini watu kama akina makonda ndio watawavusha awamu hii ya mparaganyiko_!

Ni suala la muda tu
 
Sijapinga wala kukataa mchango wa Nape CCM, ana mchango mkubwa tu kama vile Mzee Mwinyi, Mkapa, Mangula, Kinana, Kawawa, na wengineo, lkn pia muda wa yeye kwenda umefika na yeye kuna aliyowakuta na walimuachia na kwenda zao!
 
Kama weledi wa jeshi letu la polisi ni huo basi tuna Safari ndefu sana
Alitakiwa Nape baada ya kuachishwa uwaziri na kubaki mbunge tu alitakiwa akafanye siasa jimboni kwake walikomchagua sio dar yeye sio mbunge wa dar. Kajisahau anafikiri yeye bado waziri. Waziri ni mwakyembe yeye kwa sasa ni mbunge kama godbless lema au msigwa siasa na Press conference azipeleke jimboni kwake alikochaguliwa kinondoni alipofanyia Press conference amwachie mbunge wa kinondoni.Kasahau kuwa ukiwa mbunge siasa kafanye kwenu ulikochaguliwa hili ni kwa wote wabunge wa CCM na upinzani. ndio maana polisi walimdhibiti
 
Unamsifia lakini alivyowafungia binge mlimtukana sana, alivyomtusi Lowassa wenu mlimsema maneno yote ya hovyo eti leo mnamwita shujaa wenu. Mnapoteza dira
 
Huyo Nape asijifanye hajatendewa haki, hivi majuzi tulikuwa tunazungungumzia mamlaka makubwa ya rais kwenye katiba, yeye akawa anapita huko vijijini kuwaambia wananchi eti shida yao ni maji, umeme, barabara nk na wala sio katiba mpya. Hivi majuzi wamekwenda huko Dodoma wakapitisha eti rais aliyeko madarakani apite bila kupingwa na wote wakaaunga mkono wakidhani ni jambo la maana wanafanya. Ngoja sasa waone rangi halisi ili huko mbeleni wakiambiwa waache kuunga mkono kila jambo la kipuuzi ifikie mwisho.
 
Nawashangaa watu wengi waliokuwa hawampendi Nape Nnauye sasa hivi mnamuona shujaa. kwangu mimi naona ni bora mara kumi RC Makonda a.k.a Daudi Albert Bashite kuliko huyu Nape ambaye alikuwa mwiba mkubwa kwa upinzani. Huyu ndo aliyesababisha ubaya wote ulioonekana kwa Lowassa, hivyo amesababisha kwa kiasi kikubwa watu kumtilia mashaka ENL (Lowassa).
Huyu mtu kama atatoka CCM asipokelewe kabisa upinzani. Hivyo nampongeza Magufuli kwa kumtumbua huyu mshenzi. Bora Bashite anafanya kazi kwa "kiki" pamoja na kuwa cheti fake lakini ana kauli nzuri za kazi kuliko domo kaya la Nape...mara bao la mkono sijui nini...
Sidhani kama watu wanamuona Nape ni shujaa. Kinachoendelea kwa sasa watu wanafurahi kuona Nape is facing the reality now. Wakati wenzake wakadai Live coverage ya Bunge, wakati akina Lisu wanashikwa kwa uchochezi kila week, wakati akina Lema wanaswekwa ndani kwa miezi minne ... huyu Nape hakujua kuwa nao walikuwa wanapigania haki yao.

Sasa leo ukiangalia key sentences za Nape zinaanza kushabihiana na wapinzani!!
  1. Nimekuwa mungwana kwa nchi yangu
  2. Nimekuwa maungwana kwenye chama changu
  3. Unalipwa kwa kodi ya kwetu wavuta jasho
  4. Kuna gharama katika kusimamia haki za watu
  5. Nitasimamia ukweli
  6. Nitapigania haki
Labda hiI ndiyo Karma anayoizungumziaga Paskali......!!
 
Naomba nikiri ndani ya miezi michache nimegundua Tanzania haina tofauti na upuuzi mwingine tunaouona Africa
Ilifika mahala nikadhani na tumekuwa tukiaminishwa kwamba kuna watu special tusiowajua wanaweza hata kumzuia Rais kufanya mambo ya kipuuzi
Kwamba Tanzania ipo unique sana na ndo maana haina vurugu lakiniw api bwana,Utawala huu umeiacha nchi uchi,hata wale vichaa wanaookota makopo wanajua vituko vinavyoendelea sasa hivi
Kumbe yale ya zamani ni kutokana na hekima za watawala waliopita labda na IQ zao ,Mungu tusaidie tu maana unaweza kuwashangaa wanaochinjana wenyewe kwa wenyewe kumbe vifua vinavumulia mengi mpaka vinasema enough is enough liwalo na liwe
 
Usishangae Nape uje huku maana huko peke yako. Wengi wanakuja ondoa shaka hio ndio ccm. Wakishakutumia unakua km toilet paper. Hawana jema hao. Utadaiwa kodi ya afya yako uilipie.
 
Kwa maoni yangu kikubwa kinachomsumbua Nape Nnauye ni kutokuubali ukweli kwamba muda wake ndani ya CCM umekwisha au niseme kwamba ulikwisha siku ambayo Mwenyekiti mpya wa CCM alipochukuwa kutoka kwa Jakaya Kikwete, sasa kwa hali ya kawaida ilipaswa Kikwete na Timu yake wote waende na watoe nafasi kwa Mwenyekiti mpya kuunda Timu yake, Kikwete alifanya hivyo alipochukuwa ktk kwa Mkapa na Mkapa alifanya hivyo hivyo alipochukuwa ktk kwa Mwinyi!

Sasa kinachomsumbua Nape na timu yake ni kukubali hilo kwamba, kuna wakati unafika inabidi ukubali na kulet go!

Kwa nini nimetumia mfano ya maisha ya Binadamu? Hapa Duniani kila baada ya miaka 100 kizazi kipya huja, na kile kilichopo hupotea na haijalishi kama wewe ni drug dealer, hardcore criminal au Binadamu mzuri unayestahili kupewa Utakatifu lkn wote baada ya miaka 100 huenda kama vile Maji ya bahari yaoshapo mchanga ufukweni ndiyo maana Kijana aliyezaliwa mwaka 2000 don't give a shit abaout Nyerere atakwambia Nyerere ndo nini? Lkn waliozaliwa nyuma ya hapo wanamjali na mnaweza kukosana ukimuongelea vibaya Nyerere, vivyo hivyo CCM imejiwekea huo utaratibu kwamba kila baada ya miaka 10 Timu mpya huingia, na iliyopo hukabidhi na kupotea kabisa, sasa huu ni ukweli ambao Bw.Nape nafikiri unampa shida kuukubali jana alikuwa kama Mfalme akienda mahali ni kama Raisi kaingia, ukitaka Cheo Kikubwa CCM na Serikalini ni lazima umlambe miguu, ukigombana naye ndiyo mwisho wako na ajira yako itaota majani, hiyo ni power kubwa sana na leo hii ni no body sasa ni ngumu adjust kwenye maisha mapya nionavyo mimi na ndiyo maana anatoa maneno kama sijui nimepigania chama tangu Baba yangu sijui blah blah hakuna aliyepigania Chama kama Nyerere, Kawawa, Kingunge, Msuya, &Co. kama ni kuwa mtoto wa mkubwa hata Watoto wa Kawawa, Nyerere, Kingune au hata Mwinyi na Mkapa pia wanaweza kusema hivyo hivyo so no big deal, lkn wanajua kwamba muda wao umepita na wame let go!

Hivyo Nape kubali kwamba CCM iko hivyo, watakupump, watakushawishi na kukusifia lkn ukweli ni kwamba sasa hivi uwezo wako uko limited maadamu hauna mtu aliye nyuma yako ambaye anaongoza Dola, hivyo wanakudanganya tu kama siyo kukutumia!

Magufuli ataunda Timu kama vile Kikwete alivyounda yake wewe ukiwemo na siku itafika Magufuli itabidi yeye na Timu yake wakabidhi pia, na cycle kujirudia upya kama na wao wakitaka kuingilia Timu mpya yatawakuta yaliyokukuta ...

Kila La Heri Nape!
CCM haibadilishi uongozi baada ya miaka kumi!hilo siyo kweli.upngozi wa CCM huwa ni baada ya miaka mitano, wanachugua mwenyekiti kama Rais akiwa madarakani inapigwa kula ya ndiyo na sekeretarieti yenyewe inabadilishwa baada ya huo mda.Bila shaka yeyote Nape amepigania chama sana huwezi hata kulinganisha na Mtoto yeyote wa kigogo ndani ya chama hicho.kumbuka kijana alitokea Uvccm pamoja na kina Emmanuel Nchimbi.
 
Back
Top Bottom